Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Hili nitatizo gumu kwani anassema umemkwaza roho yake, komaa naye mtoto asiondoke hapo, hakikisha kuwa mtoto ana vitabia vibaya, boardingi sio nzuri walitaka kuniaribia mtoto wangu,
Niambie ana miaka mingapi nikupe njia sahii
ana miaka mitano na mwezi mmoja
 
Moja kati ya mambo unayotakiwa kuyafahamu ni nafasi uliyo nayo katika familia yako.. Kama baba kama kicha cha familia unapaswa kua na maamuzi magumu tena ukiamin ww unaweza hata bila yy.!! Hata kama ni kulea
 
Moja kati ya mambo unayotakiwa kuyafahamu ni nafasi uliyo nayo katika familia yako.. Kama baba kama kicha cha familia unapaswa kua na maamuzi magumu tena ukiamin ww unaweza hata bila yy.!! Hata kama ni kulea
asante ushauri wako ntaufanyia kazi.
 
ana miaka mitano na mwezi mmoja

prospa usipokomaa mtoto wako atapata shida sana, hebu chukulia kwamba kesho haupo nani atamlea huyo mtoto? labda ungetuambia sababu ya wewe kuachana na mama yake, kwa vyovyote vile iwavyo matatizo atakayopata mtoto wewe na mama yake aliyemzaa mtastahili lawama, kwanini mzae mtoto bila malengo ya kuishi wote kwa pamoja? mtoto anateseka kwa upumbavu na uzembe wa wewe baba yake. Au unalishwa na kuishi kwa mkeo?
 
Last edited by a moderator:
Ukimsikiliza mkeo, basi hata watoto utakaozaa nae watajenga chuki kwa huyo mtoto wake wa kambo. Mimi nimeshuhudia jinsi wanawake wanavyopigwa na kuachika kwa sababu ya kuwanyanya watoto wa waume zao waliozaa na wanawake wengine.
 
HATUKO HIVYO BEST NI HUYO MKEO NDO YUKO HIVYO

YAELEKEA ALIKUWA HATAKI KUKWAMBIA MAPEMA KABLA HAMJAOANA KUWA HWEZI ISHI NA MTOTO ASIYEMZAA YEYE NDO MAAANA ALIKUITIIKIA TU ILI MFUNGE NDOA KISHA AONESHE MAKALI YAKE , HIVYO CHA KUFANYA WEWE KAA NA MSHENGA, NA WAZEE WAKUBWA WAELEZEE ILO JAMBO LILILOPO KWENU WAO WATAJUA NAMNA GANI YA KUMSHAURI

LINGINE PIGA MAGOTI MUOMBE MUNGU YEYE ATAFANYA KWANI UKIMSHIRIKISHA MUNGU MAMBO YAAKO YEYE ATATENDA NA KUMBADILISHA MKEO MOYO MBOVU ALIOKUWA NAO NA KUMPENDA HUYO MTOTO
HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA MUNGU YEREMIA 27:32
TAMBUA KUWA MTETEZI WAKO NI MUNGU HAKUNA MWINGINE YEYOTE AMBAYE ATAWEZA BADILISHA MKEO

KINGINE ONGEA NAYE LABDA ATAJIREKEBISHA :cool2:
Jamani wanajamvi msaada tutani , mke wangu ananishangaza sana.

Kabla sijamuoa nilimpa taarifa kuwa nina mtoto na akakubali kuwa atamlea kama mwanaye na akashauri nimchukue kutoka kwa mama yake ili tuishi naye sasa siku zikawa zinakatika mtoto umri umesogea na mda wa kwenda shule umefika ikabidi niende kumchukua.

Ila tukakubaliana kuwa nimwache kwa mama yangu kwanza , to cut story short nilikuta kwa mama mazingira si mazuri kwani mama ni mtu yupo bize sana na kazi zake ni mwajiriwa pia kilimo na mengineyo nikaona mda wa kumwangalia mtoto utakuwa mchache nikabadaili mawazo nikaja naye ninakoishi.

Nilipofika naye nikampa taarifa kwanini sikumwacha mtoto na kuamua kuja naye ikawa ni ugomvi kwenda mbele kila mtoto anachokifanya kwake ni kibaya.

Kila ntachomfanyia mtoto anasema namdekeza kwa kweli mimi kama baba naumia sana kwani sina hata nafasi ya kumsaidia mtoto wangu kumjenga kifikra na kimawazo.

Kwani nikitoka naye tu inakuwa nongwa nikaa naye kwenye kochi nongwa nikila naye nongwa , nina watoto wawili mmoja nimezaa naye na bado mdogo sana hajaanza kuongea na bahati nzuri wote wa kiume sasa nafikiria mambo mawili matatu ambayo ndiyo nahitaji ushauri kwenu.

1. Je nimpeleke mtoto boarding school mpaka mdogo wake akuwe ili niwe natoka / au nakaa nao pamoja kwan nataman kuwajenga wanangu kimaadili mapema?

2.Nimpeleke tu akaishi kwa bibi yake rejea hapo juu kuhusu mama yangu na ufinyu wa nafasi ya kulea mtoto mdogo kwan sisi wote watoto wake tushaanza kujitegemea?

3.Nivumilie tu labda ipo siku atajirudi kwan ashaniambia kuwa moyo wake umeshindwa kabisa kumkubali mtoto wangu huyu na anadai nimemsababishia shambulio la moyo kwa mawazo?

4. Naipenda familia yangu , nampenda mke na watoto wote sipendi kumpoteza hata mmoja, je nifanyeje wadau nipo njia panda?

Kwa hayo machache naitaji busara zenu zaid , hii sio hadith nio maisha halisi ya mtu hivyo utani tupa kule changia mawazo ya busara kama huna cha kuchangia naomba upite wima sio lazima kuandika.


ASANTEN KWA KUNISIKILIZA, NAWASILISHA.
 
Duuh sikutegemea mwanamke aliyezaa teyari kuwa na roho ngumu Kama hiyo ! Naamini ww ni baba na kichwa cha familia lazima utakayosema yazingatiwe weka msimamo thabiti wala usiyumbe mtoto alelewe kwako na mpe mwanao mapenzi yote na uwe mfatiliaji wa maisha yake Kabla ujapanda kitandani ujue mwanao amefanya nn kutwa nzima unatakiwa uwe mwangalifu sana
 
Mtoto anayekua anahitaji sana upendo toka kwa watu wanaomzunguka. Usimpeleke mtoto boarding, huko hatapata upendo wowote, na kwa kuwa bado ni mdogo atajiaona kama anatelekezwa. Hapo nyumbani kwako pia hapati upendo wowote, japo wewe unampenda upendo wako unafunikwa na unyanyasaji wa huyo mama. Hadi sasa huyo mtoto atakuwa tayari ameanza kuathirika kisaikolojia, akiendelea kubaki hapo athari zitakuwa kubwa zaidi na zitamwachia makovu ya kudumu katika maisha yake yote. Mrudishe kwa mama yake na mhudumie akiwa huko
 
Back
Top Bottom