prospa
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 554
- 156
Jamani wanajamvi msaada tutani , mke wangu ananishangaza sana.
Kabla sijamuoa nilimpa taarifa kuwa nina mtoto na akakubali kuwa atamlea kama mwanaye na akashauri nimchukue kutoka kwa mama yake ili tuishi naye sasa siku zikawa zinakatika mtoto umri umesogea na mda wa kwenda shule umefika ikabidi niende kumchukua.
Ila tukakubaliana kuwa nimwache kwa mama yangu kwanza , to cut story short nilikuta kwa mama mazingira si mazuri kwani mama ni mtu yupo bize sana na kazi zake ni mwajiriwa pia kilimo na mengineyo nikaona mda wa kumwangalia mtoto utakuwa mchache nikabadaili mawazo nikaja naye ninakoishi.
Nilipofika naye nikampa taarifa kwanini sikumwacha mtoto na kuamua kuja naye ikawa ni ugomvi kwenda mbele kila mtoto anachokifanya kwake ni kibaya.
Kila ntachomfanyia mtoto anasema namdekeza kwa kweli mimi kama baba naumia sana kwani sina hata nafasi ya kumsaidia mtoto wangu kumjenga kifikra na kimawazo.
Kwani nikitoka naye tu inakuwa nongwa nikaa naye kwenye kochi nongwa nikila naye nongwa , nina watoto wawili mmoja nimezaa naye na bado mdogo sana hajaanza kuongea na bahati nzuri wote wa kiume sasa nafikiria mambo mawili matatu ambayo ndiyo nahitaji ushauri kwenu.
1. Je nimpeleke mtoto boarding school mpaka mdogo wake akuwe ili niwe natoka / au nakaa nao pamoja kwan nataman kuwajenga wanangu kimaadili mapema?
2.Nimpeleke tu akaishi kwa bibi yake rejea hapo juu kuhusu mama yangu na ufinyu wa nafasi ya kulea mtoto mdogo kwan sisi wote watoto wake tushaanza kujitegemea?
3.Nivumilie tu labda ipo siku atajirudi kwan ashaniambia kuwa moyo wake umeshindwa kabisa kumkubali mtoto wangu huyu na anadai nimemsababishia shambulio la moyo kwa mawazo?
4. Naipenda familia yangu , nampenda mke na watoto wote sipendi kumpoteza hata mmoja, je nifanyeje wadau nipo njia panda?
Kwa hayo machache naitaji busara zenu zaid , hii sio hadith nio maisha halisi ya mtu hivyo utani tupa kule changia mawazo ya busara kama huna cha kuchangia naomba upite wima sio lazima kuandika.
ASANTEN KWA KUNISIKILIZA, NAWASILISHA.