Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

Hivi Wanawake wote mpo kama huyu?

watu8, amekwambia nampenda sana mkewe, najua hawezi kuongea nae nadhani pia kunakauoga fulani hivi anako kwa mkewe lkini pia akilazimisha huyo mtoto akae hapo atakaepata shida ni mtoto, ampleke kwa mama yake na huko atafute msaidizi wa kuwamwangalia mwanae coz bibi yuko busy

Kuyafanya haya yote bado hayabadilishi uhalisia ya kwamba huyo ni mwanao...

Wewe ni mwanaume na ni kichwa cha familia, kaa chini umuonye huyo mkeo ya kwamba aamue moja;

Kuishi kwa amani na 'mtoto wenu' au yeye aondoke
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa matatizo yako......huyo mwanamke mwanzangu ni kigeu geu kabisa na trust me ukilazimisha mwanao akae hapo basi ujue atateseka sana. Maadam kashakwambia "moyo wake umekataa kumkubali mwanao" basi ni lazima ufanye maamuzi magumu kwa ustawi wa mtoto wako. Ungekua hujamwambia habari ya mtoto wako kabla hujamuoa labda ningeweza kuelewa kwa nini anafanya hivyo japo isingekua kigezo cha kumchukia mtoto asiye na hatia.

Na kinachonishangaza zaidi na yeye ni mwanamke na amezaa......hivi kesho au keshokutwa na yeye akiwa hayupo na akisikia mtoto wake anafanyiwa hivyo anavyomfanya yeye mtoto wa mwenzie atajisikiaje.

Mi ninachoweza kukushauri kwa sasa kaongee na mama yako maana mzazi ni mzazi ili mtoto wako akae kwa mama yako na pia kwa sababu shughuli za mama yako ni nyingi mtafutie msichana wa kazi hapo ili kumpunguzia mama yako mzigo na uwe na uhakika mwanao anamtu wa kumuangalia mama akiwa kwenye mishe zake. Pia uwe unamsaidia mama yako juu ya malezi kwa pesa na pia uwe unawatembelea mara kwa mara.

Kuna baadhi ya wanawake hata sijui wanaroho gani yarabi..........Mungu atusaidie sana.
Nashukuru sana kwa ushauri wako nitaufanyia kazi
 
show her kwamba wewe ni kichwa cha nyumba na una say na power do what is right for your kid... usipay any sheeet to her she is stupid women..... alikuwa anakubali ili umweke ndani sasa kayakuta hataki... kama unashindwa kabisa mpeleke huyo mtoto boarding school na uhakikishe anapata huduma zote muhimu na wala usimsikilize huyo mkeo
 
Hapana sio wote kaka.... Kama vipi mpeleke boarding school,hatapata malezi yale uyatakayo but atakuwa katika maangaliz mazuri na atapata ku interruct na watoto wengine....#Mtazamo
Thanx but boarding kwa mtoto wa miaka mitano is it working dada yangu.
 
Huyo mkeo ana roho mbaya tu.

Mkumbushe ahadi yake na alijua una mtoto.

Je tabia za mtoto zikoje? Labda mkeo anahofia maneno maneno kutoka kwa mama mtu

Cha kufanya hakikisha mtoto anatumia muda mwingi shule....

Na anaporudi kuwe na mtu ( kama hamna dada ndio uajiri special kwa mtoto sasa)

Na mwenyewe uguatilie kwa karibu ukuaji na maendeleo ya mwanao

Mkeo muangalie kwa jicho la tatu

Ikishindikana kabisa msomeshe mtoto huko huko kwa mama yake...(mkeo mjinga kweli anatoa room ya nyie kukumbushia)
 
kwa asilimia kubwa wanawake wengi huwa ni shida kukaa na mtoto wa nje ya ndoa na wakampenda with the same love na watoto wao. Inahtaji mwanamke muelewa sana, mi naona kumuepusha mtoto na madhara yasiyokuwa ya lazima mpeleke kwa bibi alafu ukiweza mtafte mdada wa kazi muelewa akae na bibi amsaidie kucare lakin jukumu kubwa liwe ni la bibi.
Huyo ndo mama na umuhmu wa mama hauish anaendelea kulea hadi wajukuu hata kama ushakuwa na uwezo wa kujitegemea.
Nadhani bibi yake ukimweleza ukweli hatasita kumchkua huyo mjukuu
 
Mkanye mkeo....simama kama mwanaume na uwe na msimamo....maana atakupanda kichwani unajiona....
 
Kuyafanya haya yote bado hayabadilishi uhalisia ya kwamba huyo ni mwanao...

Wewe ni mwanaume na ni kichwa cha familia, kaa chini umuonye huyo mkeo ya kwamba aamue moja;

Kuishi kwa amani na 'mtoto wenu' au yeye aondoke
Unachosema kaka hujakosea ila kumbuka mimi ni mkristo as you know ndoa zetu hazinaga taraka na mbaya zaid nimesha zaa naye mtoto mmoja sasa huoni bado kuna tatizo la kuwatawanya watoto hapo pia mi bado kijana early 30's je nikioa mke mwingine nina uhakika gani kama hata kuwa kama huyu kwani hata mama wa mtoto wangu wa kwanza ashaolewa na mtu mwingine , yeye sikuwah kuishi naye before.
 
kuwa na msimamo mwanamke hatakuyumbisha na nyumba ya ghorofa haijengwi na msingi legelege what i mean anza kujenga msingi imara kwa ajiri ya mwanao aweze kuishi kwa amani hapo hapo nyumbani ukiyumba yumba hata wadogo zake watakuja kumbagua badae
Sure point taken
 
Wanawake hawawezi kabisa kuishi na mtoto ambao hawajamzaa,hata hapa watajidai kuwa hawapo hivyo na watamlaumu huyo mkeo kuwa na roho mbaya lakini ukweli ni kwamba ndivyo wote walivyo

Ukikutana na alie tofauti jua huo ni muujiza!
 
Mkanye mkeo....simama kama mwanaume na uwe na msimamo....maana atakupanda kichwani unajiona....

Wewe unaweza letewa bus.tard ukaishi naye kwa mapennzi yale yale kama watoto wengine..?

Ni ngumu....Apeleke huyo mtoto kwa bibi atafute msichana wa kazi alee mtoto...
 
Wanawake hawawezi kabisa kuishi na mtoto ambao hawajamzaa,hata hapa watajidai kuwa hawapo hivyo na watamlaumu huyo mkeo kuwa na roho mbaya lakini ukweli ni kwamba ndivyo wote walivyo

Ukikutana na alie tofauti jua huo ni muujiza!

Sawa kabisa..
 
Kama nimekuelewa vizuri umesema ulivyompeleka mtoto kwa mama ulikuta mazingira sio mazuri ukaamua umlete nyumbani ndio ukamweleza mkeo!
Ulivyokuta hali hiyo kwa mama je ulimpigia mkeo mdiscuss hiyo hali ili ajue mtoto anakuja? Au ulimstukiza na mtoto kashafika?
Kama ni hivi basi hapo ndio tatizo lilipoanzia. Je mkeo ana kazi? Kaa nae chini mzungumze kwa kirefu jaribu kuwa unawanunulia wote wa3 zawadi jaribu kumsaidia kazi zake. Kuwa karibu sana na mkeo na ajue unamjali then atapenda hata damu yako. Lakini aone unakaa kochi moja na mwanao wkt yeye hukai naye then hapo unaleta uhasama.

Ni ngumu sana kuwaelewa wanawake huyo wako hana roho mbaya ni umpende na umwonyeshe kwa vitendo ili asione huyo mtoto ni competitor!
Nikweli sikumueleza kuwa nakuja na mtoto ila alikuwa anajua kuwa nimeenda kumchukua, sikumueleza kutokana na mazingira nilijua anaweza kukataa sasa je angekataa harafu nikaja naye si ndo ingekuwa balaa thus y nilikuja naye bila kumwambia.
 
Mitazamo yetu inaendana my dia....ila mi naona kumpeleka mtoto boarding kama bado ni mdogo sana na hajajitambua. Akikua fine aende boarding. Mi wasiwasi wangu mtoto ataishi kwa mateso nyumbani baba yake akiwa hayupo na hiyo itamuharibia confidence kabisa maishani mwake. Wee mtu ata akikaa na mwanae kochi moja ni ishu leo eti umlazimshe, anaweza akakubali machoni na si moyoni na hiyo ni mbaya sana.

Nakuombea Mungu ufanye maamuzi sahihi kwa ustawi wa mtoto wako na wetu.

Yeah ni kweli mi nawaogopa sana wanawake wakishaamua na nimeona watoto wengi wakiteswa na step mother ila baba akija mama anaonyesha upendo baba akitoka mateso kunyumwa chakula na kutisha watoto na hi inaathiri mtoto kisaikologia anakosa confidence na mwoga hata akimtesa ana mtisha asimwambie mtu yeyote best solution mupeleke huyo mtoto kwa mamaako mzazi kama unamtakia mema mwanao akikua kidogo mupeleke boarding bila hvo mwanao atateseka
 
Huyo mwanamke roho ya ukatili ishamwingia sasa ukitumia ukali pia.....unaweza kuleta madhara zaidi kwa mtoto.....mtazamo wangu mrudishe mtoto kwa mama yake....mpaka pale mtoto atakapokuwa na akili za kutambua mazuri na mabaya ndo umchukue.....
 
Kaka angu si bora tu ungemuacha huyo mtoto kwa mama ake! Hata kama wangeishi kwa shida but upendo wa mama ake ungemsahaulisha hizo shida. Ukikubali matakwa ya huyo mkeo basi jua huko mbeleni ndo hutoamua chochote kuhusu mwanao. Mwambie mtoto wako hapo ndo kwao, kama hataki anaweza akaondoka tu. Kuwa na msimamo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
mama ake kaolewa na mwanaume mwingine sasa sijui kama mwanaume mwenzangu atakuwa na moyo wa kulea mtoto wa mkewe si unajua kimtazamo atasema huyu akikuwa ataenda kwa baba ye.
 
Back
Top Bottom