Hivi wanaume wote wako hivi?

Hivi wanaume wote wako hivi?

Utajulikana vipi kama ni bigwa wa kuzaa,Maisha ya karne hii watoto 6 ni wengi mno na huenda ndo wanakupa hayo mawazo.

Huo ni msalaba wako shurti uubebe wewe mwenyewe.
Kama vile unanikejeli
 
Kama vile unanikejeli

Hapana nakupa ukweli wa mambo

Kama sio kweli kwanini unakumbuka maisha yako ya zamani kabla hujawapata hao watoto

Majukumu yameongezeka maradufu.

Alafu umesema mkeo ana uja uzito wa miezi miwili bila shaka atakuwa mtoto wa 7.Muonee mkeo huruma jamani atakosa nguvu.

Alafu hivi mtu utakuwa na mawazo usijue yamesababishwa na kitu gani??
 
Sasa mimi hata sijaelewa anasema amekaa na mke wake vizuri kwa miaka yote, tatizo hajaeleza chanzo cha yy kutokuwa na furaha ila amesema tu mahusiano yamedorora kati yake na mkewe toka mwaka jana alichosema ni kuwa ana uwezo na watoto sita mhh kazi ipo hapa,i think we need to know more otherwise kila mtu atarely kwenye kuwa na watoto wengi as to me ukiwa pia una hela as you claim na watoto wengi sio tatizo cha msingi ni umejipangaje??
 
ukiona hivo ujue kuna upweke katika nafsi na unahimuhitaji YESU ili upate faraja katika nafsi lakini uhakika wa maisha ya milele baada ya haya ya duniani kuisha.

na mie nilikua hivo wakati niko ulimwenguni, nilivompa tu YESU maisha yangu, nina amani sana.

kwahiyo sasa umeondoka ULIMWENGUNI na UPO MBINGUNI AMA KIZIMU? Nyie ndo wale mnaoimba mapambio ya kiwafariji nafsi.zenu kama Ninaeleaelea nakwenda.mbinguni..sasa unaelea vip.wakat tunabanana hapa hapa duniani? angalia usijekua.kwenye kundi hili la walokole
 
hapo hakuna uchawi ,uchawi ni hiyo team ya basket uliyotengeneza hapo nyumbani kwa muda mfupi
 
hapo hakuna uchawi ,uchawi ni hiyo team ya basket uliyotengeneza hapo nyumbani kwa muda mfupi
Mbona watoto ni baraka sana hata Mali yangu inazidi kuongezeka kutoka na baraka ya watoto
 
Wala sijakosea watoto 6 ndani ya miaka 7 watano wakiume mmoja wakike,inawezekana ikawa nimajukumu yamekuwa mengi ndio sababu mawazo hayaniishi kichwani kwasababu huwa nakumbuka sana maisha ya zamani

Jibu liko hapo.
 
Mbona watoto ni baraka sana hata Mali yangu inazidi kuongezeka kutoka na baraka ya watoto

mali inazidi kuongezeka na akili inawaza sana kaka kumiliki timu ya basket at your age kama uko mjini sio kazi rahisi kihivyo labda uniambie uko kijijini mi nina wawili tu cha moto nakiona na nimekuzidi umri ,matunzo sio pesa tu kuna mambo mengi sana ,unatakiwa kuwa karibu na watoto wako wote plus wife na shughuli za uzalishaji ziendelee its not easy
 
asantee
 
Wewe lazima ni Mkatoliki haswa au Muislam haswa kwani kundi hizo hazina msamiati wa uzazi wa mpango
 
Nina miaka 33 nimeoa miaka 7 iliyopita nimejaaliwa watoto 6, hali yangu ya kimaisha sio mabaya ninao uwezo wa kifedha. Turudi kwenye topic nimekuwa nimtu mwenye mawazo kila wakati Nafsi yangu haina raha nasijui tatizo ninini, tuna maelewano mazuri sana namke Wanguu hatuna ugomvi, tatizo hili limeanza kama mwaka mmoja umepita nasiku zinavozidi kwenda ugonjwa huu naona unazidi kuwa Mkubwa kwangu. Situmii kilevi cha Aina yoyote ile Jamani embu nisaidieni natamani sana kufurahia maisha

Hongera 6 n counting.. hopefully in 2020 watakua wamefika kumi Na kitu.
 
ni nn ambacho kinakufanya ukose aman mbona hujasema, km pesa ipo watoto unao tena wakutosha mkeo waish nae vyma tatizo nn sasa
 
dah...naimagine unakaa nyumba ya kupanga...ni noma aisee...

Safi kabisa uko kwenye nyumba ya kupanga na watoto hao nadhani utaona kila rangi ya dunia hii na kumkufuru Mungu
 
Huwa nakumbuka sana maisha yazamani wakati kabla sijapata watoto,mapacha mara moja nahao wengine kila mmoja amezaliwa tofauti

Kwani maisha ya zamani yalikuaje mkuu?

Yaani unatamani ungekuwa single hadi sasa au?
 
kwahiyo sasa umeondoka ULIMWENGUNI na UPO MBINGUNI AMA KIZIMU? Nyie ndo wale mnaoimba mapambio ya kiwafariji nafsi.zenu kama Ninaeleaelea nakwenda.mbinguni..sasa unaelea vip.wakat tunabanana hapa hapa duniani? angalia usijekua.kwenye kundi hili la walokole

Amini nakuambia,ni heri ufe katika mwili,lakini roho yako&nafsi yako iwe salama.
Pia,tambua kuwa wanadamu duniani wanatofautiana,wapo walio gizani na wapo walionuruni,Je wewe u wapi ndg?
Je,bado unakimbilia waganga wa kienyeji?unaogopa wachawi?unaogopa majini na mapepo?unakiogopa kifo?huna amani?kwanini?
Kama unayaogopa hayo,unahtaji msaada wa YESU,na amini kuwa upo gizani!
 
Mkuu sverige awali ya yote Shikamoo.
Mi na wewe kiumri sidhani kama tumepishana sana ila tofauti kubwa ni hiyo ya watoto mkuu. Daaaah mi nna mmoja we una 6. Ama kweli spped yangu ni ndogo. Inanipasa kuongeza speed nadhani.
Turudi kwenye mada. nadhani hiyo ni stress tosha inayoweza kukukosesha raha kwa namna moja ama nyingine.
Labda kabla sijaendelea sana nikuulize tu we ni imani gani linapokuja suala la Mungu?
 
Last edited by a moderator:
Watoto 6?

Hawa kweli watasomeshwa wote mpaka level ya degree kweli?
 
Back
Top Bottom