hivi wanaume ndivyo walivyo??

wakukae

Senior Member
Aug 30, 2012
104
225
Habari zenu wana Jf. Naomba ushauri wenu great thinkers.. Mimi nimeolewa yapata miaka 9 sasa nina watoto watatu. Mume amenizidi umri kwa miaka mitano. Ana watoto wa nje ya ndoa wawili ambao aliwazaa kabla hajaoa. Miaka minne baada ya ndoa yetu mume wangu alipata kesi ya kumpa mimba mwanafunzi. Mama wa mwanafunzi huyo aliwahi kuwa mpenzi wa mume wangu kabla hajaoa. Hapo kesi ilikua kubwa balaa. Baada ya denti kujifungua mtoto DNA ikagoma kusoma. Kesi ikamuepuka. Ilibidi tuhame ule mji. Mume wangu akapata kazi mkoa mwingine tukaishi kwa muda wa mwaka mmoja. Kwasababu za kikazi ilibidi mimi nihamie mji mwingine na watoto wakaanza shule. Yapata miaka miwili sasa tangu nihamie mji huu na wanangu, mume wangu hataki kabisa niende kumtembelea japo kwa siku mbili. Watoto wakifunga shule wanamuomba kwenda kumtembelea. Anakataa katakata. Kwakweli nashindwa kumuelewa. Mwanzo alikua anakuja kututembelea na hela za matumizi anatuma. Sasa hata hela hataki kutuma. Nikimuuliza anasema hana. Nashindwa kumuelewa kwa kweli. Nimevumilia mengi sana ukiwemo usaliti wa waziwazi. Nimeshafuma mesej za mapenzi mara kibao tu. Zikiwa na majina yao halisi. Sasa naona uvumilivu unafikia kikomo. Nafikiria kudai talaka. Washauri wameniambia eti wanaume wote ndivyo walivyo. Nisaidieni ushauri jamani.
 
kisukari

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
4,610
2,000
mmmh,pole,jamani mambo mengine huwa hayavumiliki.huyo ameshawahi kucheat,itakuwa ana mtu tu.ila ukisema uyachunguze sana,utaendelea kujiumiza bure.watoto wanahitaji matunzo ambayo mahitaji yake mengine ni hela.jamani si nasikiasiku hiziipo systemya wanaume kukatwa mshahara wao hela anapewa mama?kwa nini usijaribu system hiyo?maana huyo mume ana pepo la ngono,wee jilelee watoto wako usijitafutie pressure bure.
 
hosny

Senior Member
Dec 9, 2012
126
0
Pole sana,labda nikuulize ulishawah kumuweka kikao mumeo kwa wazazi wake?
 
StayReal

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
518
195
Yani kuna wanaume wengine kazi yao daily ni kuharibu reputation ya other good men!
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,794
2,000
Huna mume hapo dada (pole kwa makavu ya uso, ndo dawa itakayokuponya).
1 huruhusiwi kumtembelea wewe wala watoto
2 haji tena kuwaona
3 hatoi matumizi.

Ni nini kinachowafanya muendelee kuwa mke na mume?
Hatua ya kwanza ya divorce process ni kuishirikisha familia, then viongozi wa dini. Waeleze wazazi, kuwa hamna ushirikiano wowote, sio wa kihali wala wa kimali. Na muongee kuhusu child support. Weka mguu chini haswa, atakuwa.kawekwa kwenye rambo huyo. Akisikia unataka kumuacha ataanza kukimbizana na wewe utashangaa.
Kujibu swali lako, sio wanaume wote wako hivyo. Huyo wako tu mwenye kichwa kama doughnut tu.
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,709
2,000
Ingawa mmeo ni msiba na mbwaa usiwahukumu wanaume wote. Kama unayosema ni kweli basi mmeo ni mtu wa kuogopwa kuliko hata ukoma na ukimwi. Amelewa chupi kiasi cha kushindwa hata kujijua kama usemayo ni kweli. Kazi ni kwako kuchagua kusuka au kunyoa maana ameishatenda mengi yanayohitaji adhabu ambayo binadamu hawezi kuibuni. Kama unaona ana kuzuia kwenda kumtembelea kwanini usichukue watoto wake ukaenda kule kwa nguvu tena bila kumtaarifu ili ugundue kinachomfanya akuzuie. Uhitaji kuomba ruhusa kwenda kumuona mumeo wala watoto kwenda kumuona baba yao. Nadhani heshima na upole wako anavichukulia kama ujinga na woga kiasi cha kukuwekea masharti ya kipumbavu.Wewe naye ni mwili mmoja. Pia jitahidi uende mahakamani kutetea haki za watoto wako. Maana kama anazaa hovyo hovyo kama panya siku ya kufa utajikuta una utitiri wa watoto walio wake na wasio wake. Na kama utasema utumie kipimo cha DNA bado ni upotezaji pesa. Chukua hatua mapema. Kama utaona migongano haifai unaweza kuamua kuanza maisha yako na watoto wako na Mungu atakubarikini.
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Ukweli ni kuwa hapo huna mume.Ni jambo lisilopendeza kukuambia muachane lakini jikague unaweza kupata maradhi ya hisia!
"
Angalia faida na hasara za kuishi kwa aina hiyo.Jitahidi kutafuta suluhu kwa nguvu.
"
Waeleze wazazi na wengine walio karibu na ndoa yenu ili mpate ufumbuzi.
"
Ni lazima aitwe aeleze sababu.Akikataa huyo hana maana na hataki suluhu.
"
Hapo unaweza kuamua vinginevyo!
 
snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,151
2,000
KHEE!
mamii cha kufia nini?
cha kufia nini mpenzi wangu!
hebu endelea na maisha yako kwanza bora kama mpo miji tofauti na anavokukataza usiende anakuepusha na mengi sana mpenzi wangu!AKUWACHE UPUMUWEE!
mume wa aina hii hapaswi kujumuisha wanaume wote kuwa wanafanana!
kimsingi baki mwenyewe lea watoto wako,wawili tuuu na una kazi!FUNGA MKANDA JIKAZE NYANYUKA PIGANIA FUTURE YA WANAO!
mume mjaa laana hvo si mume ati!
 
Ameen. Ni kweli upole na heshima yangu anachukulia kama weekness point ya kuninyanyasa. Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
wakukae

Senior Member
Aug 30, 2012
104
225
Huna mume hapo dada (pole kwa makavu ya uso, ndo dawa itakayokuponya).
1 huruhusiwi kumtembelea wewe wala watoto
2 haji tena kuwaona
3 hatoi matumizi.

Ni nini kinachowafanya muendelee kuwa mke na mume?
Hatua ya kwanza ya divorce process ni kuishirikisha familia, then viongozi wa dini. Waeleze wazazi, kuwa hamna ushirikiano wowote, sio wa kihali wala wa kimali. Na muongee kuhusu child support. Weka mguu chini haswa, atakuwa.kawekwa kwenye rambo huyo. Akisikia unataka kumuacha ataanza kukimbizana na wewe utashangaa.
Kujibu swali lako, sio wanaume wote wako hivyo. Huyo wako tu mwenye kichwa kama doughnut tu.

Kweli usemayo mamii. Asante kwa ushauri. Nitafanya hivyo
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,818
2,000
kumtembelea mumeo unaomba ruhusa?
Hebu nenda ila jiandae maana utamkuta mwenio ndani.....

Ila huyo mwanaume hakufai atakuletea ukimwi....
 
wakukae

Senior Member
Aug 30, 2012
104
225
Ukweli ni kuwa hapo huna mume.Ni jambo lisilopendeza kukuambia muachane lakini jikague unaweza kupata maradhi ya hisia!
"
Angalia faida na hasara za kuishi kwa aina hiyo.Jitahidi kutafuta suluhu kwa nguvu.
"
Waeleze wazazi na wengine walio karibu na ndoa yenu ili mpate ufumbuzi.
"
Ni lazima aitwe aeleze sababu.Akikataa huyo hana maana na hataki suluhu.
"
Hapo unaweza kuamua vinginevyo!

Nimekuelewa mkuu.
 
wakukae

Senior Member
Aug 30, 2012
104
225
KHEE!
mamii cha kufia nini?
cha kufia nini mpenzi wangu!
hebu endelea na maisha yako kwanza bora kama mpo miji tofauti na anavokukataza usiende anakuepusha na mengi sana mpenzi wangu!AKUWACHE UPUMUWEE!
mume wa aina hii hapaswi kujumuisha wanaume wote kuwa wanafanana!
kimsingi baki mwenyewe lea watoto wako,wawili tuuu na una kazi!FUNGA MKANDA JIKAZE NYANYUKA PIGANIA FUTURE YA WANAO!
mume mjaa laana hvo si mume ati!

Sema wewe mamii nikisema mie wananambia ati utakimbia wangapi? Wanaume wote wako hivyo, aso hili ana lile.
 
Mjuni Lwambo

JF-Expert Member
Apr 25, 2012
6,551
2,000
USHARI WA BURE KWA WADADA.
Ukiona mwanaume kabla hata hajaoa amezaazaa ovyoovyo mara nyingi huyo ni mjinga gubegube, piga chini.
 
hosny

Senior Member
Dec 9, 2012
126
0
Asante sana. Sijawahi kushitaki upande wowote ingawa mwenye macho haambiwi tazama. Wanajionea wenyewe

Ok sasa fanya hivyo ingawaje mumeo hana anachojivunia zaidi ya kuwa si mwaminifu wala upendo wa dhati kwako watoto wako familia yako pia ndugu jamaa na rafiki zako tafuta mshenga kiongozi wa dini pamoja na wazazi woote wa pande mbili uwaeleze pia utoe msimamo wako wewe juu ya hili kumbuka maamuzi magumu yanahitajika.
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
11,904
2,000
eeh ndio tulivyo...mpango wa kando lazuma kabisaaa!! sasa wee kubali yaishe bwana. ka na watoto wako. hapo iliahakula kwako
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom