wakukae
Senior Member
- Aug 30, 2012
- 109
- 48
Habari zenu wana Jf. Naomba ushauri wenu great thinkers.. Mimi nimeolewa yapata miaka 9 sasa nina watoto watatu. Mume amenizidi umri kwa miaka mitano. Ana watoto wa nje ya ndoa wawili ambao aliwazaa kabla hajaoa. Miaka minne baada ya ndoa yetu mume wangu alipata kesi ya kumpa mimba mwanafunzi. Mama wa mwanafunzi huyo aliwahi kuwa mpenzi wa mume wangu kabla hajaoa. Hapo kesi ilikua kubwa balaa. Baada ya denti kujifungua mtoto DNA ikagoma kusoma. Kesi ikamuepuka. Ilibidi tuhame ule mji. Mume wangu akapata kazi mkoa mwingine tukaishi kwa muda wa mwaka mmoja. Kwasababu za kikazi ilibidi mimi nihamie mji mwingine na watoto wakaanza shule. Yapata miaka miwili sasa tangu nihamie mji huu na wanangu, mume wangu hataki kabisa niende kumtembelea japo kwa siku mbili. Watoto wakifunga shule wanamuomba kwenda kumtembelea. Anakataa katakata. Kwakweli nashindwa kumuelewa. Mwanzo alikua anakuja kututembelea na hela za matumizi anatuma. Sasa hata hela hataki kutuma. Nikimuuliza anasema hana. Nashindwa kumuelewa kwa kweli. Nimevumilia mengi sana ukiwemo usaliti wa waziwazi. Nimeshafuma mesej za mapenzi mara kibao tu. Zikiwa na majina yao halisi. Sasa naona uvumilivu unafikia kikomo. Nafikiria kudai talaka. Washauri wameniambia eti wanaume wote ndivyo walivyo. Nisaidieni ushauri jamani.