Chama cha Mapinduzi mara tu baada ya kifo cha mwalimu kimekuwa mstari wa mbele kutekeleza uovu uliopindukia kwa watanzania. mathalan, CCM ni mafisadi, walinda mafisadi, dhurumati, wezi, wauaji, waongo, wazushi, wamejaa mawazo mabaya siku zote, wanafiki, wajenzi wa umasikini wa kielimu na kiuchumi kwa watanzania. Hebu fuatilia nukuu hizi za Biblia, Union Version uone jinsi CCM walivyo kinyume na Mungu wa Ibrahimu, Muumba mbingu na nchi.
- Mithali 12: 22 " Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA;Bali watendao uaminifu ndio furaha yake" na Mithali 15:26 "Mashauri mabaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maneno yapendezayo ni safi" Fuatilia kauli za Werema na Spika pamoja na mawaziri wote wa CCM bungeni.Ona kauli za Pinda bungeni na huko kwenye gesi huko Mtwara utabaini ninachokisema.
- Mithali 16:19 "Afadhali kuwa na roho ya uynyenyekevu pamoja na masikini,Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi" Ukiangalia vitendo vya serikali ya CCM kuhusu EPA, RICHMOND, DEEP GREEN, MEREMETA,meno ya tembo na meli za Kinana, miradi ya gesi huko mtwara, machimbo ya madini, aridhi inavyoporwa kwa wanyonge, watanzania masikini wanavyokamuliwa ili kutunisha mifuko ya mafisadi kupitia malipo ya umeme, bei za mafuta nk hutakosa kuona jinsi CCM walivyo kinyume na Mungu.
- Mithali 17: 15 "Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA" Tumesikia na kushuhudia jinsi serikali hii inavyopindisha sheria zake kila pale wakubwa wanapofisidi wanyonge. Ona migogoro kati ya wakulima na wafugaji inavyoamuriwa kwa kupindisha sheria.
- Mafisadi na wote mliojitajilisha haraka haraka kwa fedha za maendeleo ya wananchi katika halimashauri zetuy maandiko yanasema: Mithali 13: 11 "Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa" Kuna watu walitajirika sana kupitia mashirika na makampuni ya umma mfano, Shirika la Ugawaji, Bhesco, Nafco, RTC, Usahishaji, nk. leo hii wako wapi...! mali zilipukutika wengine wamepigwa na viharusi.
- Mithali: 3:33 " Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu; Bali huibariki masikani ya mwenye haki" Laana ya BWANA iko pia katika kila chama cha waovu. Nao hawatadumu wasipo tenda haki na kurudisha utajiri wa fedha na madini ya watanzania walioiba na kuificha nje na ndani ya nchi.
- Watu hawa juzi walimlinganisha Kikwetre na Muyngu aliyeziumba mbingu na nchi. Ole wao!
Kuwashabikia, kuwatetea, kujiunga nao, kuwa kiongozi wa waovu hawa, wanaoona ni sawa wagonjwa wanyonge wa taifa hili kukosa huduma na madawa katika hospitali za umma kifisadi tu. Watu hawa wanyonge ambao elimu ya watoto wao imewekwa rehani kwa utajiri wa mafisadi hawa wachache HAKIKA watu hawa ni watu wampingao Mungu wa mbinguni.