Wana JF Wenzangu,
Nimetafakari sana juu ya tutokapo,tulipo na tuendapo na kufikia hitimisho kuwa unahitaji kuwa na akili za mwendawazimu kuishabikia CCM na kuwa mwanachama wa CCM. Nimefikia hitimisho hilo kwa kuwa CCM imekuwa ikihubiri kuleta maendeleo mengi lakini kiuhalisia kinachohubiriwa nao hakilingammi kabisa na rasilimali za nchi hii zilizotumika. Mbaya zaidi, mimi kama mzazi nitasikitika siku zote na sitapenda kuona kuwa familia yangu inakosa mkate wa kila siku kwa mimi kushindwa kutimiza jukumu langu hilo.
Kwa sasa hivi, chini ya utawala huu wa CCM imekuwa kawaida kwa wafanyakazi wa serikali hasa wale wanaolipwa kima cha chini kushinda njaa mchana wakati wakiwa kazini kwa sababu malipo ya ujira wanayopewa hayatoshelezi kwa wao kukidhi haja ya kula mchana na wakati huohuo kuhudumia familia. Ninajiuliza, ni mafanikio gani utakwenda mbele ya jukwaa uanze kutamba nayo wakati nyumbani kwako watu hawapati milo mitatu kama ilivyo kawaida?
Ushahidi na utafiti nilioufanya ni kwamba katika maofisi mengi ya umma hasa hapa Dar es Salaam wafanyakazi wengi ambao hulipwa kima cha chini mchana kwao wanapitisha bila kutia kitu chochote tumbo, si kama wanapenda, la hasha ni kutokana na kiasi kidogo cha ujira wanachopata,ninajiuliza, kweli ndani ya miaka 50+ ya uhuru mfanyakazi wako anashinda njaa kwa sababu ya ujira mdogo, halafu bado unajitokeza mbele ya jukwaa na kujigamba kwamba umethubutu, umeweza na sasa unasonga mbele? Ni mwendawazimu tu ndiye atayakubali maneno haya na kejeli hizi,ndiyo maana mimi huwaona siku zote wanaoishabikia na wanachama wa CCM wote kwamba ni wendawazimu