Hivi wachezaji wetu wanagundu au wana tatizo na mfumo?

6 Pack

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
1,826
4,074
Za asubuhi wakuu wote wa hapa JF.
Kuna maswali nimekuwa nikijiuliza kuhusiana na wachezaji wetu wa timu ya taifa na hata wale wa club ambao ni watanzania. Mbona sijawahi kuwaona wakigombea au kuchaguliwa kuwa wabunge kama wenzao wasanii?

Mbona sijawahi kuwaona wakichaguliwa au kuteuliwa kuwa mawaziri au manaibu waziri kama wenzao wasanii?

Sijawahi kuwaona wakichaguliwa au kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya nk kama wenzao wasanii?

Je tatizo ni nini kutokujiweka karibu na siasa au kutokukubaliwa na mfumo ambao mara nyingi ndo hupanga nani awe nani na nani awe nani?

Mwenye kujua au kuwa na majibu ya haya maswali naomba anisaidie kunijibu. Nitamshukuru kwa majibu yake. Lakini pia hata asiekuwa na majibu pia anaruhusiwa kusoma na kuchangia.
Haya twende kazi!
 
Attachments

  • Screenshot_20230503-121156.jpg
    Screenshot_20230503-121156.jpg
    57 KB · Views: 4
  • Screenshot_20230503-121320.jpg
    Screenshot_20230503-121320.jpg
    53.2 KB · Views: 3
Wacheza mpira kinachowakwamisha sana ni elimu. Wengi wao wanavuta bangi na walianzia kazi yao katika mazingira ya kihuni sana huko mtaani kwahiyo hata background zao zinawasaliti. Kutokana na uduni wa elimu hata uwezo wao wa kuongea mbele za watu ni mdogo mno. Wachezaji waliomaliza kidato cha nne salama ni wachache tofauti na wanamuziki ambao hadi wenye Masters wapo kama kina MwanaFA. Pamoja na elimu duni pia kifedha hawako vizuri. Hela za kwenye mpira ni chache zinazopatikana mwa miaka michache sana.
 
Punguani mmoja wewe. Chizi kabisa huyo Ronaldo ni mtanzania ? Embu acha ujinga bhana
Iwe kitaifa au kimataifa bado naona msanii anakimbiza aisee. Check hapo
 
Attachments

  • Screenshot_20230503-121156.jpg
    Screenshot_20230503-121156.jpg
    57 KB · Views: 2
  • Screenshot_20230503-121320.jpg
    Screenshot_20230503-121320.jpg
    53.2 KB · Views: 1
Amekuwa mchezaji na Mfungaji bora kabisa wa ligi kuu

Na amekuwa mbunge wa Kilolo kwa miaka 10
Ok mkuu huyu sikuwahi kumfahamu. Ila ni wa kutafuta na tochi ukilinganisha na wasanii ambao hata mtoto wa miaka 7 ukimwambia akutajie msanii ambae ana wadhifa serikalini na bungeni atamwambia fulani fasta bila kupapasa.
 
Wacheza mpira kinachowakwamisha sana ni elimu. Wengi wao wanavuta bangi na walianzia kazi yao katika mazingira ya kihuni sana huko mtaani kwahiyo hata background zao zinawasaliti. Kutokana na uduni wa elimu hata uwezo wao wa kuongea mbele za watu ni mdogo mno. Wachezaji waliomaliza kidato cha nne salama ni wachache tofauti na wanamuziki ambao hadi wenye Masters wapo kama kina MwanaFA. Pamoja na elimu duni pia kifedha hawako vizuri. Hela za kwenye mpira ni chache zinazopatikana mwa miaka michache sana.
Yani wewe ndio umefafanua vizuri sana, i mean umepita mlemle kiasi kwamba ni vigumu mtu kusoma bila kukuelewa.
 
Ok mkuu huyu sikuwahi kumfahamu. Ila ni wa kutafuta na tochi ukilinganisha na wasanii ambao hata mtoto wa miaka 7 ukimwambia akutajie msanii ambae ana wadhifa serikalini na bungeni atamwambia fulani fasta bila kupapasa.
Inategemea na kiwango alichofikia cha Uchezaji mpira, kwa Ngazi ya Timu ya Taifa huyo Tenga na Ally Mayai, Lakini Hata Dr Ramadhan DAU aliwahi kucheza yanga kids kadhalika Prof Mshindo Msola
 
Back
Top Bottom