Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,832
- 18,827
Anaandika Ezekiel Kamwaga:
Tuwe makini
Kuna fasheni imeanza ya watu kujionyesha wana msimamo mkali dhidi ya ushoga. Taratibu, jambo ambalo liko mbali sana kwenye matatizo yetu linaanza kukuzwa kwa sababu linagusa hisia za wengi. Hata hivyo, tutapoteza mwelekeo kama tutaanza kuwaona ‘mitume’ hawa wa Kupinga ushoga kama ndiyo watu wa muhimu zaidi. Nchi kubwa zimeanza kuyumba baada ya kuwafanya watu wanaojadili mambo madogo kuwa wa maana na kudharau wale wenye mawazo makubwa yenye kuondoa shida kubwa. Matatizo ya Tanzania yanajulikana. Kuna shida kubwa ya ajira kwa vijana wetu
Wapo viongozi wamesema hilo ni bomu. Vijana wenye nguvu, maarifa na ujuzi lakini wenye njaa na hasira ni tatizo kubwa kuliko ushoga. Tuna tatizo la mamilioni ya Watanzania kuwa nje ya mfumo wa Bima ya Afya na wanafilisika kwa kuugua au kuuguza. Kuna tatizo la ubora wa elimu yetu
Kwenye kukabiliana na changamoto za kisasa za duniani. Kuna tatizo la utayari wetu kujiandaa na majanga kwenye dunia hii ya mabadiliko ya TabiaNchi. Tutumie nguvu na maarifa zaidi kujadiliana mambo ambayo kweli ni shida kwetu. Tukienda na hii njia tuliyoanza, tutakuja kuchagua
Viongozi ambao sifa yao kubwa ni kupinga ushoga. Hiyo tu. Analysis ya siasa za siku hizi inaonyesha kwamba viongozi/wanasiasa wanaopoteza muda na vitu vya hisia ni wale ambao hawana majibu ya maswali magumu yanayokabili jamii zao wakati huo. Wanabaki kuwa watu wa vitu vidogo