Je, biashara yako Inatumia mfumo gani kati ya huu hapa?

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
Kabla Sijakwambia ni aina gani ya Mifumo naenda Kukuonesha hapa Chini.

Ngoja Kwanza...

Nikufumbue Macho na Nikutoe tongo tongo Juu ya Mifumo hii ya SIRI Inayotumiwa na...

Biashara kubwa Kutikisa biashara Ndogo ndogo kwenye Sokoni la sasa Lenye Miluzi mingi

Ukweli ni kwamba Wajasiliamali wengi Hutumia muda Mwingi.

"Kufanya kazi katika Biashara zao Lakini SIO Kwenye Biashara zao"

Najua Nitakuwa Nimekuacha...Ondoa shaka Naenda Kukuvunjia vunjia Hapa chini

Angalia...

Hivi ukiwa Unaanzisha Biashara yako huwa unataka Ionekanaje baada ya Kukamilisha kila Kitu?

Yaani...

Huwa unataka Mtu akija Kuiona au Mteja akija Kununua bidhaa au huduma toka kwako... Ungependa Ionekane Vipi?

Hata ukisema Utamuuzia mtu Unajua kabisa Biashara yako Inaanzia hapa Inaishia pale

Mfano Mzuri...

Ukienda kununua Kitu Used (Kilichotumika) Tuseme Gari... Si Ndio?

Muuzaji Huwa Anakwambia...

Hii Gari Inashida hizi hapa, ana Kwambia Labda...

Gia namba 3 Haifanyi kazi...

Pia TAA za Breki Haziwaki...

N.k

Kwa Ufupi Tu...

Anakupa kila Taarifa ya Muhimu unazotakiwa Kupata halafu Anakuonesha hadi Jinsi ya Kuliendesha hilo Gari... Si Ndio?

Yeah!

Sasa na wewe Biashara yako Unapoianzisha huwa Unataka iwe na Muonekano gani?..

Yaani...

Mtu akija kutaka Kuinunua au hata Kuwekeza... Una uwezo wa Kumwambia Inaanzia hapa Inaishia hapa

Kama bado Biashara yako haina Kitu kama Hicho basi Fahamu kwamba...

Biashara yako Inakosa kitu Kinachoitwa...

"Business System"

Usihangaike... Nimekuwekea Maelezo yake Hapa Chini

Angalia Inavyokuwa...

Bishara yako Inaweza kufanya KAZI Bila hata ya wewe Kuwepo?..

Biashara yako Inaweza Kutoa aina ile ile ya Bidhaa/Huduma kwa Miezi hata 6 mbele bila wewe Kuwepo?..

Mfano...
.
Unauza Mgahawa unaweza kuwa Unapika kila siku Chakula chenye Ladha ile ile kwa Miezi sita na zaidi Mfululizo?..
.
Biashara yako Inaweza kukupa UHURU wa kufanya shughuli Zingine wakati yenyewe Ikiendelea bila Changamoto?..
.
Biashara yako bado Inategemea Mtu mmoja ambaye Akiondoka tu Haiwezi Kuendelea?
.
Unaweza kuiuza Biashara yako kwa Mtu (Kama Ukitaka)?..
.
Unaweza kutaka Mwaka huu upate Faida ya 5M na Ukapata kupitia Biashara yako?..
.
Kama Biashara yako Inaweza kujibu Maswali yote hayo...Basi usiendelee Kusoma makala hii kwa sababu SIO kwa ajili yako
.
ILA...
.
Kama biashara yako Haiwezi kufanya hivo basi Makala hii ni Zaidi ya Pilau Kuku Kwako...
.
Kama wewe ni Huyu Hapo Mtu wa Pili... Basi ungana na Mimi hapa Chini
.
Ukweli ni Kwamba...
.
Biashara zote Zinazofanya Vizuri sokoni kwa muda Mrefu uwa zina kitu Kimoja cha Kufanana...
.
Ambacho ni..."Business System"
.
Na Tunaposema...
.
Business System Ina Maana ya...
.
Seti ya Kanuni, Taratibu na Desturi nzima za Biashara yako Zinazotumika ili Kuleta Matokeo flani
.
Kwa Ufupi ni...
.
Ni mfumo Mzima ambao Unaweza Kujiendesha wenye hata bila Mmiliki Kuwepo!
.
Na ukweli ni kwamba kwenye Biashara kuna aina Nyingi za Mifumo ya Uendeshaji
.
ILA...
.
Kwa Leo nitaenda Kukuonesha aina KUU Tatu (3) tu za Mifumo ambayo Unaweza kuanza Kuitumia hata leo
.
Mifumo ambayo hata Biashara ndogo kama yako Inaweza ku ADAPT na Kuanza kuifanyia kazi
.
Kwa sababu Biashara zote Unazoziona ni kubwa Zilianzia kwenye hii Mifumo Mitatu unayoenda Kuiona hapa Chini.
.
Nisikuchelewe...
.
Anza na Mfumo huu Hapa Chini
.
Mfumo wa Kwanza ni...
.
1). Hard System
.
Kama uko kwenye Biashara na Ukaanza kufanya vitu ambavyo vya Kuonekana
.
Mfano...
.
Kutengeneza Logo
.
Kuwa na Store yako
.
Kuwa na Sare (Uniform) za Kazi
.
Basi jua kabisa hapo Unatumia Mfumo huu... (Hard System)
.
Na ndio Mfumo unaotumiwa na Biashara nyingi kwa Sasa!
.
Yaani unakuta Mtu anaanza Kutengeneza Logo Kabla ya Kujua kina nani Watanunua anacho Uza
.
Na Sisemi kwamba huu Mfumo SIO Sahihi bali Hauwezi kukupa Matokeo makubwa Unayoyataka.
.
Vile Vile...
.
Sio kwamba huu Mfumo SIO Muhimu Kuutumia, Yaani kuwa na Vitu kama...

Logo, Tshirt, Business Cards n.k

Sio Muhimu...Hapana!
.
Ni muhimu Sana ILA kama Biashara ndo Inaanza unaweza Usione kama una Faida sana
.
Ndio maana Unakuja umuhimu wa Mfumo huu wa Pili
.
Yaani...
.
2). Soft System
.
Huu ni Mfumo ambao unaonesha Jinsi vitu Vinavyosikika au Kusemwa
.
Mfano...
.
Customer Care
.
Sales Scripts Zako
.
Customer Support
.
N.k...
.
Yaani...
.
Unaweza ukawa na Utaratibu kwenye Biashara wa kuongea na Wateja wako
.
Labda kila Mteja akifika huwa Lazima
.
1). Umsalimie
.
2). Umuulize Maswali flani ili kujua Pain Points zake
.
3). Kisha unampitisha Kujua kama ni Mteja Sahihi
.
Haya maswali Matatu yanaweza yakawa ni mfano wa...
.
Mfumo mzima wa Jinsi Biashara yako Inavyoongea na Wateja wako
.
Kwahiyo hata Kama wewe Hutakwepo bado una Uhakika wa Biashara yako Kufanya vizuri
.
Kwahiyo Soft System Inaweza ikawa ni...
.
Jinsi Unavyokabidili VIPINGAMIZI vya Wateja wakati wa Kuuza...(Customer Objections)
.
Jinsi Unavyo WASALIMIA Wateja wako...(Customer Care)
.
Jinsi Unavyouza Bidhaa/Huduma yako baada ya Kufika ofisini kwako
.
Jinsi Unavyo wasiliana na Walengwa wa Bidhaa/Huduma yako
.
Ndani ya hii "Soft System"...Unaweza kukadiria Mauzo yako ya Mwaka Mzima
.
Kwasababu...Factor zake Ziko Measured!
.
And...
.
"Anything that Can be Measured Can be Done"
.
3). Information System
.
Huu ni mfumo Mzima wa taarifa... Kuanzia kwenye
.
Mission ya Biashara yako
.
Culture (Utamaduni) wa Biashara yako
.
Core–Values za Biashara yako
.
Sijui Unanipata Vizuri?..
.
Anyway...
.
Ngoja nikupe Mfano ili Unielewe Jinsi unavyofanya Kazi huu Mfumo
.
Tuseme umebahatika Kupata Mgahawa wako na...
.
Mungu kakujalia Mpaka Umeweza kutoa Ajira kwa Vijana wadogo kama wewe Watano
.
Ikitokea moja ya Kijana wako Mmoja unayemuamini akaamua Kupumzika kazi kutokana na...
.
Changamoto mbali mbali Zilizopo njee ya Uwezo wake na Wewe kama...
.
Boss pale Ukaamua kumpa Ajira Kijana Mpya...
.
Sasa kama Unataka kijana aliyekuja awe Kama kijana aliyeondoka... Unafanyaje?
.
Kama una Mfumo wa aina hii Basi Haitakuwa na Tatizo kwako.
.
Kwasababu...
.
Utampitisha Kijana Mpya kwenye Mafunzo ya wiki au Mwezi mmoja...
.
Ambayo...Yatamuongoza kufanya Kazi kama yule aliyeondoka na Bila changamoto yoyote ile
.
Hayo Mafunzo yote kwa Ujumla ndio tunaita..."INFORMATION SYSTEM"
.
Na hiyo Ndio maana Halisi ya kuwa na Mfumo wa Biashara.
.
Yaani...
.
"Mfumo unaendesha Biashara yako, Na watu (Wafanyakazi Wako) Wanaendesha Mfumo"
.
Wafanyakazi hawana Uhusiano wa moja kwa moja na Biashara yako.
.
Na hivyo ndivyo unavyojenga MFUMO Ambao unajiendesha Bila wewe Kuwepo.
.
I Hope Umejifunza Kitu Japo kwa Uchache.
.
Uwe na IJUMAH Kareem!
.
Gracias
.
Seif Mselem
 
Back
Top Bottom