Hivi unaanzaje kuwaza kuoa au kuolewa wakati hujui maana halisi ya ndoa?

Kichwamoto

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
3,353
4,535
Hi,

WanaJF nimeboreka nimekutana na bonge la ufufu, mdada kaniletea kadi ya harusi nikampongeza, ila nikampa swali bwagizi, Best ndio utaolewa je unafahamu maana ya ndoa, naomba majibu nione kama unafuzu ndoa.

Katoa majibu mafufu matupu, nikapata fursa tena ya mtarajiwa mwenza nae kaleta kadi nikamuuliza kimasihara sharo unaoa je unafahamu maana ya ndoa? Majibu kabutua hovyo hata bench hakai.

Pumbavu mtaoa wenyewe mnachezea kanuni za Mungu pasipo ufahamu na marifa toshelezi.

Kila mtu aendelee na katiba na miongozo yake.

Nawasilisha
 
Bas hao wanaenda kufanya harusi na sio kufunga ndoa.
Siku hiz watu wengi wanataman kuvaa shela na kuongozana na mwanaume alievaa suti.
 
Wao hawajui maana unayoijua wewe, wanaoana kwa maana yao hiyo hiyo usiyoitaka wewe…. sema tu hutaki kuchangia au HUNA HELA.!
 
Wamekujibu nini na wewe unaelewa ndoa ni nini?

Isijekuwa wewe ndio kilaza halafu unaongeaongea tu hapa.

Weka majibu hapa tuone.
 
Back
Top Bottom