Hivi kwa nini unaogopa kuoa au kuolewa?Unajua nini maana ya Ndoa?Biblia inasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwa nini unaogopa kuoa au kuolewa?Unajua nini maana ya Ndoa?Biblia inasemaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, Jan 10, 2011.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 2,550
  Trophy Points: 280

  [​IMG]

  Hawa nao ni Adamu na EvaNDOA, TALAKA NA KUOLEWA TENA

  UTANGULIZI

  Ndoa ilianzishwa (instituted) na Mungu. Mungu aliumba mke kwa ajili ya Adamu kwa kuwa Mungu aliona "Haikuwa vema" kwa Adamu kuwa peke yake.

  Mungu alimuumba mke (Eva) kuwa msaidizi (suitable helper) wa Adamu kutawala dunia, kulea familia na kumuabudu Mungu.
  (Mwanzo 2:18, 42)

  Ndoa ni mke mmoja na mume mmoja (monogamous).
  Mungu alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu na si Eva na Jane, Ingawa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba wanawake wengi kadri anavyoweza ila alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu. Agano la kale kulikuwa na polygamist na matokeo yake hakukuwa na amani.
  (Mwanzo 2:22)

  Ndoa ni mke na mume. Biblia haizungumzii kuumbwa kwa Adamu na James au Eva na Linda na kufanya ndoa bali Adamu na Eva.
  (Mwanzo 2:22, 1:28)

  Ndoa inahusisha Mume kuondoka kwa wazazi ili kuanza familia yake kama mke na mume na pia kuna kuwa na taarifa kwa jamii (public recognition) kwamba fulani na fulani ni mke na mume hata kama formalities au tamaduni hutofautiana.

  Ndoa inawafunga mke na mume hadi kifo.
  Marko 10:9
  1Wakorintho 7:39
  Warumi 7:2-3

  Ndoa inahusisha wajibu wa kila mmoja katika mahusiano kwa mke kutii (submissive) na Mume kumpenda mke wa kujitoa sadaka (sacrificial love)
  Efeso 5:22-24, 25-28)

  Ndoa huhusisha mume kuwa kichwa cha nyumba au mke kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa
  Efeso 5:23
  1Wakorintho 11:3

  Ndoa ni suala zito ni uamuzi wa pili kwa uzito duniani (kwanza ni wokovu na pili ni ndoa) hivyo si kuingia tu kwa kadri unavyijisikia kwani barabara unayoingia ni dead end hakuna kutoka hadi kifo.

  Dunia imejaa udanganyifu wa kila aina kuhusiana na suala la ndoa jambo la msingi ni kujua kweli na kweli itakuweka huru.

  Unapoingia kwenye ndoa unahitaji kuwa makini, mbele ya safari kujitetea eti nilikuwa bado nina akili ya kitoto, au nilidhani atabadilika au sikuwa na akili timamu au sikujua kama itakuwa hivi haitakusaidia kwani ukiingia ni hadi kifo kitakapowatenganisha hivyo kama hujaoa au kuolewa please be extra carefull siyo unabeba bora liende then kesho unasema "I made a terrible mistake" naweza kuachana naye! hakuna kitu kama hicho.

  Ubarikiwe!
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Nzuri ila ndefu muno
   
 3. MAENE

  MAENE Senior Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ubarikiwe sana,vijana tunahitaji kupeana maarifa kama haya ya KUTUJENGA.
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Naogopa kuolewa kwa kuwa nimeshuhudiwa maisha yangu yote kuwa ndoa ni ngumu na ina mateso. Asante kwa kutuelimisha zaidi jinsi neno la Mungu linavyosema kuhusu ndoa.Tutaendelea kuwa makini ili tusije jutia kama wanaojutia na kutushuhudia sis ndoa ni ngumu na yenye shida.

  Neno la Mungu pia linaruhusu watu kutoolewa: 1Wakorintho 7:8,imeandikwa Kwa wale wasiooa na kwa wajane,ingekuwa vizuri wakabaki kama mimi nilivyo.Lakini kama hawawezi kujizuia,basi waoe na kuolewa,kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa. Kwa msingi huu kama mtu ana uwezo wa kuishi bila ya kuoa au kuolewa na akampendeza Mungu basi na iwe hivyo.
   
 5. J

  J Lee Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu nashukuru sana umetoa somo zuri sana naamini utasaidia wengi sana, hakika ubarikiwe.
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Naogopa kuolewa kwasababu sijawahi kuona ndoa iliyodumu muda mrefu bila migogoro.
  Ahsante kwa somo lako ingawa halijaniingia akilini.
   
 7. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mi siogopi na siku ikifika nitakubali kuolewa tena kwa ujasiri mwingi. people want to fall into marriage and enjoy but instead they fall out of it soon after their great wedding ceremonies and suffer greatly in their hearts. we need to grow in marriages, preserve and sustain it with all purity while be willing to accept all associated risks and rewards under the Lord's care.

  inashangaza watu hawataki kuolewa/kuoa lakini kuzini wako tayari 24/7. it seems that we are totally thinking out of our senses, away from Gods plan. ndoa ni mpango wa Mungu na si wa mwanadamu. kama Mungu alipotosha design ya ndoa, hakika mwanadamu hawezi kuinyoosha kwa akili zake. kumbukeni imeandikwa kuwa "kwa maana hekima ni ulinzi kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo. tafakari vyema kazi yake Mungu kwa sababu ni nani awezaye kukinyoosha kitu kile alichokipotosha yeye?" (mhubiri 7:12-13).
   
 8. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 2,550
  Trophy Points: 280
  Asante Miss Judith!! You deserve thanks na mungu atakubariki maisha yako yoote na kukunyooshea yale yaliyo mema kwako!!
   
 9. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 2,550
  Trophy Points: 280
  Pole kwa kuwa shetwani ndio kiongozi wako!!ulishawahi jiuliza kwani nini hao wanaolewa wamekuwa na migogoro?Unahisi ndizo sababu zitakazokufanya na wewe uwe kwenye migogoro ya ndoa?unafikiri migogoro ya Ndoa ni mikubwa kuliko uliyonayo kwa hao unaowaita sweet,darling,dear,honey au red carpet?
  Ukinijibu nitakushukuru.Asante
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  lol!
  Umenikosea nidhamu. Mimi kiongozi wangu ni mungu.

  Unajua mara nyingi tunajifunza kutoka kwa watu. Na hata tunapotaka kufanya kitu tunaangalia ni wangapi walifanikiwa katika hilo.
  Ndoa za sikuhizi ni utata mtupu AU.
  Ila Simaanishi kwamba sitoolewa. Itakapofikia muda wa kuolewa nitafanya hivyo maana ni agizo la mungu.
   
 11. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,724
  Trophy Points: 280

  Ugonvi au mfarakano kwenye ndoa ni kitu cha kawaida sana Husninyo. Isikukatishe tamaa. What matters is LOVE. Ukimpenda mtu hakuna kosa ambalo litakufanya ujutie kuolewa. Hata kama anatoka nje ya ndoa, kitendo cha wewe kugundua mara nyingi kinafanya penzi lenu lichanue upya. It is sometimes boring if you just live without conflicts.

  Kwa mfano mimi mume wangu niligundua anatoka na mdada tena to my assessment could be "good looking" (think this is right word) than me na nikamwambia ahamie kwa kimada wake akagoma na kunipigia magoti nikajua kweli mume wangu kanizimia. From there I could measure how much my hubby loves me and I am still his number one wengine ni mapoozeo tu.

  Niliweka private investigators kuona kama ana-muattend huyo dada na nafurahi kuwa amesitisha huduma.
   
 12. s

  shosti JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  naolewa ili iwe nini sasa,kama watoto ntapata bila hata kuolewa,kama furaha nkishaolewa ndio itaisha,kama pesa najua kuzitafuta,kama maziwa nnakunywa bila kufuga ngombe,na la zaidi nnaishi kwa amani bila matatizo,poleni wapenda kubanana vitandani.
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye bold,je umeweza kujizuia?
   
 14. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 15. Ishmael

  Ishmael JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2014
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mungu akubariki ndugu.

  Hakika Adam alikuwa na mmke mmoja Eve na hivyo ndivyo Mungu alitaka tokea mwanzo.
   
 16. l

  lady in action JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2014
  Joined: Feb 1, 2014
  Messages: 612
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 60
  ndoa za siku hzi????? bora niwe msimbe tu
   
 17. sokwe

  sokwe JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2014
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 2,010
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Ila usiwe mzinzi Kama hutaki kuolewa baaaasi.
   
 18. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2014
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,685
  Likes Received: 30,843
  Trophy Points: 280
  Real we unaweza?
   
 19. Mtoto halali na hela

  Mtoto halali na hela JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2014
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 19,190
  Likes Received: 2,885
  Trophy Points: 280
  hadi leo waogopa?
   
 20. sokwe

  sokwe JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2014
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 2,010
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Yes...
   
Loading...