Hivi ulishawahi kuujiuliza hili Jambo kweli

Mkuu Pilipili zina faida sana aisee. licha ya kuwa apetizer, inakata mafuta, inapasha mwili joto, inasaidia wenye sukari na Kwa wanaume ni nzuri zaidi etc etc
Sasa hapo natafuta kupiga chafya tuu na mimi ni adui wa pilipili wala siwezi kujiwekea lengo za kuzitumia na kwa hali halisi ni ngumu sana kukaribisha ukorofi na ukali
 
Mkuu Pilipili zina faida sana aisee. licha ya kuwa apetizer, inakata mafuta, inapasha mwili joto, inasaidia wenye sukari na Kwa wanaume ni nzuri zaidi etc etc

Mkuu Tized hakuna kitu nachukia kama pilipili na wala hizo faida zake haziwezi kunifanya niwe mpenzi wa pilipili hata uzitangaze vipi
Niliwahi kung'oa mti wake nyumbani maana walikuwa wakipika msosi wao wanaweka pilipili nikaona ahhh ya nini shida nikautolea mbali
 
Last edited by a moderator:
1. huwa mkimya sana mwanzoni lakini nikishakuzoea basi huo ukimya hupotea kabisa.
2. huwa na kinyongo kwa muda mrefu kwa mtu aliyeniudhi sana.
3. kununua vitu ambavyo sikuwa nimepanga kununua nikiwa natoka nyumbani ila tu kwa sababu nimeviona kwa wakati huo na vimenivutia
 
Hii ya kuwa mpole sana imenigharimu kwa upande mwingne,nmedhurumiwa sana
 
Hahahahaaaa... Aisee hadi ukang'oa mti kabisa!!! hahahahaaaaa... kweli we kiboko.

Sisi tulikuaga na mashindano ya kuoneshana ugumu... unabugia yale mapilipili mareefu membamba mekundu kama nini halafu makali balaaaa... ukiweza kutafuna ukakaa nazo mdomoni halafu usitoe machozi unakuwa ndo bingwa (hakuna kumeza wala kunywa maji baadae).... nlikua nashindaje bingo ya kujipoozea na chochote!! hahahahaaaa ndio apo nilipopataga uguru wa hizi mambo utafikiri nilizaliwa India

Unatafuna unakuwa mwekundu kila mahali, mashavu na ulimi unawaka moto lakinio kidume unakomaatu... Du zamani tulikua na raha zetu bwana. Siku hizi umpe mtoto pilipili kama enzi zetu lazima akalazwe na dripu juu za kutosha.

Mkuu Tized hakuna kitu nachukia kama pilipili na wala hizo faida zake haziwezi kunifanya niwe mpenzi wa pilipili hata uzitangaze vipi
Niliwahi kung'oa mti wake nyumbani maana walikuwa wakipika msosi wao wanaweka pilipili nikaona ahhh ya nini shida nikautolea mbali
 
hapa kuna shida na sijui ntafanyaje.....
nakuwa na kinyongo na mtu nilokosana nae tena napenda kulipiza kisasi japokuwa hata nikilipiza kisasi bado nakuwa na hasira na huyo mtu..... na hata aniudhi sitoi chozi hata kidogo la! ila nahakikisha nimelipiza ingawa hainizuii kumfanyia kitu kibaya
 
Mi napenda sana kukaa peke yangu nyumbani, nahisi isingekuwa kwenda kazini na mihangaiko ya kila siku ningekuwa sitoki kabisa! Lakini pia huwa nasamehe hata bila kuombwa msamaha na sipendi kuombwa msamaha! Daaaaah sijui huwa nipoje Mimi jamani!
 
Hapo hujasema udhaifu wowote bali mazuri yako. Kupenda kukaa nyumbani ni haiba tu labda kama unatamani kutoka lakini unaogopa.
 
jaman wewe kama mimi vile mpaka naitwa boya lakin kukaa peke yangu nyumbani ndio starehe yangu kumbe tupo wengi hongera.
 
Ukisikia neno udhaifu unalitafsirije? Huo mi naona ni udhaifu wangu kusamehe bila kuombwa msamaha nalo ni tatizo! Tena sipendi kabisa mtu aniombe msamaha, nimezungumzia kupenda kukaa nyumbani tena pekeangu! Au unisaidie udhaifu ninini maana yake, pengine mi sielewi halafu unawezaje kuupima udhaifu wa mtu? Don't u know ure weakness can be my strength and vice versa!
 
Hahaaaah kumbe tupo wengi eeeeh! Kati ya marafiki zangu wote mimi tu ndo nipo hivi! Najickia vizuri zaidi kukaa peke yangu nyumbani.
 
Ukisikia neno udhaifu unalitafsirije? Huo mi naona ni udhaifu wangu kusamehe bila kuombwa msamaha nalo ni tatizo! Tena sipendi kabisa mtu aniombe msamaha, nimezungumzia kupenda kukaa nyumbani tena pekeangu! Au unisaidie udhaifu ninini maana yake, pengine mi sielewi halafu unawezaje kuupima udhaifu wa mtu? Don't u know ure weakness can be my strength and vice versa!

sina kamusi hapa labda ningenukuu maana ya udhaifu lakini maana rahisi ya haraka ni ile ya kinyume chake, yaani, kutokuwa na nguvu/mashiko/ujasiri/kiwango.

Ninawezaje kuupima udhaifu wa mtu? = kwa kuulinganisha na ambacho si udhaifu, mfano, utajua mtu ana udhaifu wa ukatili kwa kuulinganisha ukatili wake na huruma.

Mimi napima udhaifu kwa vipimo vyangu vya jema na baya. Mtu kupenda kukaa ndani kwangu mimi si udhaifu maana wanadamu hatuwezi kuwa na haiba moja, yaani wote hatuwezi kuwa "outgoing". Ndo maana nikakwambia kukaa ndani si udhaifu ila kama huwa unatamani kutoka nje ila unaogopa au unaona aibu basi ni udhaifu.

Kwangu mimi kusamehe si udhaifu bali ni ujasiri kwani si tabia ya asili ya mwanadamu, na ndo maana (mimi mkristo) kunakuwa na amri na hamasa kuwa tusamehe. Wakristo tunaita msamaha mojawapo ya tunda la roho. Ili ulipate unahitaji nguvu ya ziada ya makusudi. Huko juu kuna mtu kasema udhaifu wake ni kutosamehe-kuweka kinyongo muda mrefu na kulipa kisasi. Huyu anajua kusamehe ni "jema" alilolikosa. Uwezo wa kusamehe ni jambo jema, tena kusamehe bila kuombwa msamaha ni jema zaidi. Inaweza kuwa udhaifu endapo una tabia nyingine ambayo unaifananisha na msamaha kwani mtu akisamehe hujiskia mwenye amani na furaha. Msamaha ukikufanya ujihisi tofauti basi si msamaha ni kitu kingine. Mtu mwenye uwezo wa kusamehe hata wabaya humsifia.

Endapo utaamua kusema wewe ni dhaifu kwa kuwa hauko kama fulani basi huo ndo udhaifu, yaani, kutojiamini au kujikubali. Kwa mfano mtu mtaratibu/mpole kujiona dhaifu kwa sababu yeye si mchangamfu, au mchangamfu kujiona dhaifu kwa kuwa si mpole. Upole na uchamngamfu ni sifa nzuri. Nikisema udhaifu wangu ni weusi kwa sababu kuna weupe udhaifu wangu utakuwa si rangi yangu bali kutojikubali ndo udhaifu, ila nikisema udhaifu wangu ni kuropoka nitakuwa sijakosea kwa sababu kuropoka haijawahi kuwa ujasiri mahali popote kwa hiyo msemo wa "udhaifu wako ni ujasiri wa mtu mwingine" unakosa mashiko hapa. Kama upole wako au uchangamfu wako hausababishi makwazo kwa wengine huo si udhaifu ni ujasiri. Lakini kuna wengine ni wazubaifu, wana viburi au dharau au kujiona wanyonge halafu wanajiita wapole. Wengine wako arrogant wanajiita wachangamfu.

Mtu kutambua udhaifu wake ni jambo zuri sana, ila kuyaona mazuri yake kama udhaifu ni jambo la hatari.
 
umenifanya ni login......big up bro...
 
Muda mwingi naonekana ni mwenye hasira kumbe sivyo pia sizoeleki kiurahisi hasa mtaani kwangu, nina rafiki mmoja tu naye kanizidi umri na hayupo nilipo, waliokaribu yangu yaani ndugu na jamaa hunipenda sijisifu kwa vile ni msikivu kwao mwepesi wa kukubali kukosolewa mtoaji msaada mzuri mgumu kusamehe pia si rahisi kujua kama umeniudhi ila huhesabu visa (nikiwa na maana siku nikiamua kukwambia umeniudhi nitakueleza yote tangu mwanzo hata kama umeniudhi mara alfu nitakuambia yote kwa siku moja na hapo natoa uamuzi), mgumu sana kulia, nikikasirika hadi nikalia hata miaka kumi ipite mtu akikumbushia hicho kitu palepale nakasirika na kulia tena kwa kwikwi, nacheza sana na keyboard kutatua matatizo yangu kuliko kumweleza mtu. Kuna gazeti linaitwa Cosmo kutoka kwa madiba hilo huwa ni mtatuzi wangu wa yaliyoko moyoni kwa kweli limenisaidia sana maana ukimwambia mtu mambo yako kesho yanatoka hakuna nisichokipenda kama mtu kujua siri zangu wakati sikupenda ajue. nikikuzoa muongeaji sana pia nikiongea na wewe leo uitegemee kesho tena hapana, ila nitakusalimia naendelea na yangu.
 
Back
Top Bottom