ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 20,732
- 48,466
Ukiachana na msemo kwamba tumbo halina shukrani; hata lipewe chakula kizuri na kitamu kiasi gani, ni lazima baadaye litahitaji tena,
Ni kitu gani kingine unadhani hakina shukrani?
Umewahi kukutana na mtu asiye na shukrani?
Umetenda wema kwa uwezo wako wote, ukajitolea kadiri ulivyoweza Lakini siku ukiteleza na kufanya kosa moja tu, mtu akalibeba hilo kosa kana kwamba hujawahi hata siku moja kumfanyia jambo jema
Na pengine hata wewe amewahi kukukosea na kukupa maumivu?
Nini humfanya mtu kusahau wema wote aliotendewa baada ya kuona au kuhisi umefanya kosa?
Kwa nini mara nyingi huonekana kana kwamba kosa moja linafuta mema yote yaliyowahi kufanywa?
Wewe umewahi kumhukumu mtu kwa kosa moja na kubeba kinyongo kwa muda mrefu kiasi cha kusahau wema wote aliowahi kukutendea?
Je, kati ya mbeba kinyongo na yule anayesamehe kirahisi, nani huishi kwa amani zaidi?
Nikianza na mimi mwenyewe, wanasema mtu haoni madhaifu yake🤔
Lakini ukweli ni kwamba mara nyingi mtu hujijua zaidi kuliko watu wengine wanavyomjua
Mimi huwa nina hasira nikikosewa, lakini hasira yangu haidumu sana
Kununa kwa muda mrefu siwezi Hasa kama mtu huyo aliwahi kunifanyia wema, huwa nakumbuka yale mema na kumpa nafasi nyingine kwa sababu naamini binadamu si mkamilifu
Je, wewe upo vipi? Ukikosewa na mtu aliyewahi kukutendea mema, huwa unakumbuka wema wake au kosa lake?
Saturday 🫴🥰
ShesRise_1 🖐