Sikupenda kuchangia uzi hu kwasababu za kidini na pia kwasababu humu ndani hua unaweza kuhisi hisi tu kwamba huyu ni dini fulani au dhehebu fulani, nimeonelea nidandie kwako kwasababu kwanza huna conflict of interest ya dini kupitia uzi hu and hence you may be free (though bado naamini this is too theoretical kwamba huamini chochote kuhusu dini hizi 2 ) and hence naweza kuandika chochote na usikasirike.
Mwandishi kasema Uislam una 1000 years hapa kwetu? I think hi sio sahihi, Uislam umeingia miaka ya 1800 so how ifike hiyo 1000 years? Labda alimaananisha duniani but not Tanzania or even east Africa.
Kidogo nisaidie kaka, kwamba Uislam ndio umeleta mwamko wa kusoma na kuandika? Hili sidhani kama ni kweli, nimeishi kwenye Uislam hadi nikiwa na miaka 23 ndipo niliamua mwenyewe kuingia kwenye Ukristo, hadi mwaka 1987 nikiwa nasoma madrasa, sikuwahi kumwona mwalimu akitufundisha kuandika, alikua anatufundisha kusoma Kuruani, miaka hiyo hiyo ya 80 nadhani ndipo zilipoanza kuja juzuu zenye tafsiri ya Kiswahili so tukaanza kujua hasa tafsiri ya nini ya kile tunacho jifunza. Unless unishawishi kuliamini hili la kujifunza kuandika. Kwangu mimi naona historia ya kusoma na kuandika ipo upande wa Ukristo zaidi kuliko Uislam cause hata majengo ya ilimu yanaibeba zaidi historia hiyo kwao kuliko Uislam. Kuna mmoja hapo juu kazungumzia lugha ya Kiswahili kwamba imeletwa na Uislamu? 😆 seriously 😐? Sijui vitabu tulivo soma, nikiwa form 1 or form 2, mwalimu wa Kiswahili alitufundisha kwamba, Waarabu walivo fika pwani ya Africa mashariki, wakiwakuta wenyeji nao wakaanza kuwaita Sahel yaani Waswahili, na lugha yao kua ni Kisahel, from sahel (according to Arabs ) ndio ikaja Kiswahili na Waswahili so kusema eti Uislam ulileta lugha ya Kiswahili to my opinion sidhani kama ni sahihi, lugha ilikutwa but labda kuna maneno yaliongezwa kama zilivyo lugha zingine zote duniani except Kiyunani. Maneno kama Laa meaning HAPANA, ni ya kiarabu but maneno kama SHULE ni ya Kijeruman but tunayatumia kwenye Kiswahili chetu.