Hivi udini wa Samia Suluhu uko wapi? Tuzungumze ukweli

Hivi udini wa Samia Suluhu uko wapi? Tuzungumze ukweli

Kusini kuchele

Senior Member
Joined
May 21, 2023
Posts
121
Reaction score
687
Humu jukwaa kuna tuhuma ambazo Samia Suluhu anatupiwa ya kwamba ni mdini na amejaza waislamu katika wateule wake sasa najiuliza udini wa Samia uko wapi? Au udini wa Samia anaufanyia wapi?

Mbona nikiangalia kati wateule wake kati ya wakristo na Waislamu naona wakristo ni wengi sana kwa maana kuna idadi kubwa ya wakristo Kati wateule wake kuliko waislamu?

Je, udini wa Samia uko wapi? Na mbona kiongozi akiwa muislamu hizi kelele za udini ni nyingi sana kuliko akiwa wa dini nyingine?

Mimi nauliza tu wala sina maana mbaya uzi uachwe.
 
Humu jukwaa kuna tuhuma ambazo samia suluhu anatupiwa ya kwamba ni mdini na amejaza waislamu katika wateule wake sasa najiuliza udini wa samia uko wapi? Au udini wa samia anaufanyia wapi? Mbona nikiangalia kati wateule wake kati ya wakristo na Waislamu naona wakristo ni wengi sana kwa maana kuna idadi kubwa ya wakristo Kati wateule wake kuliko waislamu?

Je udini wa Samia uko wapi? Na mbona kiongozi akiwa muislamu hizi kelele za udini ni nyingi sana kuliko akiwa wa dini nyingine?

Moderator mimi nauliza tu wala sina maana mbaya uzi uachwe.
Hata ajaze wote wao wake au waislam wote sawa tu lakini tuone matokeo, siyo longolongo.
Hata aweke watoto wake wote na mume na wake wenza. Merits.
 
Udini wake upo pale anapojaribu kujitetea tuhuma dhidi ya uongozi wake kuwa anachukiwa sababu ya dini yake.
Watu wanahoji matendo ya ukandamizwaji haki, utekaji na kuuwa watu hovyo 29/10 yeye hajibu hizo hoja analeta hoja ya dini yake.
Namheshimu Sana, na nimemtetea mwanawe kufanya biashara, nimekemea wanaomkosoa kwa kumtukana. Ila sitaacha kumkosoa kwa kutowadhibiti wabadhirifu wa mali za umma na wauwaji na watekaji. Pia nitamkosoa kwa uteuzi wake kwa baadhi ya watu inaonesha upendeleo(nepotism) kwa kujuana au undugu kuliko kuangalia sifa.
 
Back
Top Bottom