Hivi tutawapoteza watu wetu wa karibu mpaka lini kisa Pesa.!?

Kwani wewe binafsi unaichukuliaje pesa? Tuanzie kwako mwenyewe, Je, uko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekutia hasara pesa zako? Awe ndugu au rafiki au mtu baki, akikutia hasara utachukulia poa tu??
Hebu tumbie madam Carleen
 
Pole sana Carleen....

Uzi wako umenifanya nimkumbuke rafiki yangu mmoja..kipindi fulani cha maisha yetu tuliwahi kuishi pamoja na kuwa karibu sana..Tulikuwa ni kama ndugu wa tumbo moja ingawa tulikutana ukubwani katika harakati za maisha..nikiugua ananitibia, akiugua namtibia pia, hayo ndio yalikuwa maisha yetu ya upendo ..Kwa zaidi ya miaka 2 tuliyoishi pamoja, HAKUWAHI KUNIFANYIA KITU KIBAYA/ROHO MBAYA na wala sikuwahi kumfanyia ubaya...Hatukuwahi hata kugombana ile seriously ukiacha some quarrels which are normal in life....

Kipindi fulani alipata shida moja kubwa sana ambayo ilikuwa inaweka hatarini future yake..Hakuwa na tegemeo jingine zaidi ya mimi ndugu yake..Hata wazazi wake wasingekubali kumsaidia ndio maana hakutaka kuwashirikisha..Namimi isingekuwa rahisi kumkimbia ndugu yangu niliyeishi nae vizuri sana kisa changamoto aliyoipata..nikapiga moyo konde, nikasema wewe ni ndugu yangu tunasolve hii inshu..Inshu yenyewe ilihusisha pesa, alikuwa na inshu moja kubwa sana na ya muhimu ambayo alitakiwa kuisolve kwa pesa...Akanifata akanambia, FOHADI naomba unikopeshe kiasi XXXXXXX haitapita miezi miwili nitakupa....Sikuwa na hofu, wala sikuwaza kama nitaipoteza ile pesa kwa jinsi tulivyokuwa...Nilizama mfukoni nikamkopesha ndugu yangu nikiamini kuwa nailinda future yake...Nikweli, alisolve inshu yake na mambo yake yakawa byeee kabisa...nilikuwa na furaha kumuona ndugu yangu amekuwa na amani...Baada ya muda akapata kazi Musoma, ikabidi aniage akaondoka huku akiniahidi kuwa ndani ya miezi 2 pesa yangu itakuwa imerudi...

Kilichofata baada ya hapo ni maumivu kwangu..Niliumia sana kupoteza kiasi kikubwa tena kwa mtu ambae sikumtarajia na mbaya zaidi mtu aliyekuwa na uwezo wa kunilipa ile hela...Simu zangu zilikuwa hazipokelewi, msg hazijibiwi na sikuambulia kitu..Ni miaka mingi imepita, hadi leo sijaambulia kitu chochote, Nimesamehe, nishasahau...Ila urafiki mimi nayeye tena ni FUTURE IMPOSSIBLE TENSE...

Pole sana carleen..I know the feeling.
Pole sana Fohadi maisha yana namna nyingi sana sana za kutufunza, naamini utachukua hilo kama funzo, sindiyo.?
 
Watu kwao Uaminifu ni jambo gumu sana.

Hatuna kabisa utamaduni wa kuheshimu makubaliano au mikataba.

Sometimes, tunalalamika hatuna mitaji lakini ukiangalia tatizo kubwa linaanza kukosa uaminifu.
Katika matatizo sugu tuko nayo kwa jamii yetu kubwa zaidi ni kukosa uaminifu, na hili halichagui mkubwa ama mdogo, dini wala kabila.!!
 
Mimi kuna rafiki yangu ameniomba nimkopeshe pesa lkn kwa kutambua atasumbua kunilipa niliamua ni muahid ntampa. Ilipofika siku nikakataa kumpa aisee huwezi amini amenichukia adi sasa ivi. Imekua km ni ma adui ss. Wakati alikua rafiki yangu wa karib kbs.
Au nlikosea ndugu zangu?
Ulikosea. Ungemueleza mapema km huna hiyo ela kuliko kumpotezea muda. Ndio maana alichukia
 
Mimi kuna rafiki yangu ameniomba nimkopeshe pesa lkn kwa kutambua atasumbua kunilipa niliamua ni muahid ntampa. Ilipofika siku nikakataa kumpa aisee huwezi amini amenichukia adi sasa ivi. Imekua km ni ma adui ss. Wakati alikua rafiki yangu wa karib kbs.
Au nlikosea ndugu zangu?

Kuna best yangu friend in did nilietoka nae mbali nilimuomba aniazime elfu 30 nichangie harusi moja hivi baada ya mwezi mmoja ningemrudishia, alikuwa ni muajiriwa mahari fulani ,alinipa ahadi Kama ww jamaa kesho nakupa ,
ilikuwa mwezi wa 9 ,2019,😂😂😂 mpaka mwaka unaisha jamaa hakuwahi kupokea simu wala kujibu SMS ,alikuwa rafiki yangu mnoo changu chake chake changu, ila aliniacha stage moja kuelekea mafanikio ktk maisha akatupa mti na jongoo wake😁😁😁 , namshukuru Mwenyezi Mungu mwaka huu mwezi wa 4 na mm kanifungulia milango jamaa. Sikuhizi ni mwendo wa ku like post tu Facebook na Instagram nikipost ana like na yeye akipost na like , Juzi kanunua gari ni ka like , All in All pesa imevunja urafiki wetu na kilicho baki ni kutambiana kwa kulike post ktk mitandao ya kijamii.
 
Nimejifunza roho mbaya kwasababu ya watu wasio waaminifu kwenye kulipa madeni mtu anakuja mikono nyuma na shida ilhali anajua kabisa na wewe upo juu ya mawe unajitolea kumdhamini kwa mtu akipewa hela kurudisha majanga anakuachia msala. Nitasaidia ndugu yangu wa damu ambaye najua hata nikifulia hanitupi au mpita njia najua nakua nimetoa sadaka ila rafiki sisaidii asilani bora urafiki uishe. E, S, N mlichonifanya kunibebesha madeni ya mamilioni ya shilingi na kuniacha nilipe nimewasamehe ila sitakuja kuwasahau na mmenifundisha kitu.

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
 
Dah ngoja nifanye nimrudishie mjomba angu laki 3 yake maana tangu anikopeshe ni muda na hajanishtua hata siku moja, sijui ananilia timing


Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Fanya urudishe aisee, siku nyingine utapata shida utashindwa kumkimbilia maana deni lako kwake linakufunga,hata ww mwenyewe utaona aibu...labda kama ndio wale watu wakujichetuau anajifanya kasahau deni,
 
Nimejifunza roho mbaya kwasababu ya watu wasio waaminifu kwenye kulipa madeni mtu anakuja mikono nyuma na shida ilhali anajua kabisa na wewe upo juu ya mawe unajitolea kumdhamini kwa mtu akipewa hela kurudisha majanga anakuachia msala. Nitasaidia ndugu yangu wa damu ambaye najua hata nikifulia hanitupi au mpita njia najua nakua nimetoa sadaka ila rafiki sisaidii asilani bora urafiki uishe. E, S, N mlichonifanya kunibebesha madeni ya mamilioni ya shilingi na kuniacha nilipe nimewasamehe ila sitakuja kuwasahau na mmenifundisha kitu.

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
Asante sana Carleen na nimejifunza sana..na hapa naungana na mamylove ila natofautiana nae sehemu ndogo sana..Watu pekee ambao sitaacha kuwakopesha kamwe ni ndugu zangu...hata wasiponilipa sitaumia maana it has always been my desire kufanikiwa na kuwasaidia ndugu zangu kimaisha...I have my young bro yuko chuga..Desemba mwaka jana alibanana nikamkopesha ila hadi leo hajanilipa na siumii na wala huwa sipigi mahesabu kama kuna hela ipo kwake coz that is my responsibility as a big bro to my juniors....

Kuhusu Marafiki ni HAPANA..kuna rafiki angu mwingine nilisoma nae advance, tulivoenda chuo akaja nmkopeshe ada na kweli asingefanyiwa registration...nakumbuka ilikuwa 100k na akasema atanilipa na riba, mimi nikakataa riba ila nikamwambia akipata tu hiyo hela anilipe..na aliahidi within one month maana atapata toka hom...

Sikuona ile hela, badae anakuja ananipa namba ya mama ake niwe namdai..kwani mimi nilimkopesha mama yake?....sawa nikawa naongea na yule mama ananipa ahadi kila siku...Baadae rafk yangu akaja kunambia kuwa eti katika kumdai yule mama yake nilimtukana kwenye msg na ndio maana hataki kunilipa....Nilijisikia vibaya sana, nikamwambia nimemtukana kwa msg, basi nipo tayari twendeni polisi akashitaki..kati ya kitu siwezi kufanya ni kumtukana mama mtu mzima tena mzazi wa rafiki yangu maana hata mm sitapenda kutukaniwa mama yangu...Mwisho wa siku nilipoteza hela na urafiki....

Baada ya mwaka mmoja yule rafiki yangu akaanza kunitafuta tena..kipindi hicho tumemaliza chuo..Mambo yake yakibanan ananicheki nimsaidie hata nauli au hela ya vocha..mwanzoni nikawa na mpa ila mara ya mwisho nilimtumia ilikuwa 2000 tu ya vocha na hapo hapo nikamuuliza, hivi mshikaji, pamoja na kunidhulumu laki moja yangu na kunisingizia nimemtukana mama yako, unapata wapi ujasiri wa kunitafuta na kuniomba tena hela?.....Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kaniomba msaada yule jamaa...



NB: 'unakuta unaemwamini ndiye anakuwekea sumu, hawana alama binadamu wanaokuja kukuhukumu' - DARASA
 
Bora umuambie uwezo wa kumpa huna na uishie hapo, hujafanya vyema kumpa ahadi hewa, japo naamini ungempa pia ungezungushwa mpaka ujute.!
Mimi n mradi wangu mkoani,kijana naemuamini kusimamia n kununua kanipiga 4.7...cnc dec 2020 na kusepa....namtafutia nafasi lazima familia yake iuze ngombe za kutosha wanilipe sitaki riba,mwezi ujao lazima nimdake mana simu zake zote ziko hewani
 
Mtu anapokuja kwangu na kutaka kuniazima pesa huwa nampa nusu ya kiasi anachotaka,hii uwa nafuata principle moja ya pesa inayoniambia usimpe mtu pesa ambayo huwezi kuipoteza.ukija kwangu unataka kukopa elfu 50 basi nitakwambia dah hali ngumu mwanangu Mimi Nina 20000 hapa,ukichukua ata usipolipa hainiumi kama 50000
 
Back
Top Bottom