Hivi tutawapoteza watu wetu wa karibu mpaka lini kisa Pesa.!?

Shida iko wapi? Si utafute zako...

Mimi mtu akianza tu habar za mizinga urafiki au undugu lazima upungue kama sio kuisha, hivi hatuwezi kuwasiliana tu pasipo kuhusisha pesa?
Sasa kama una rafiki na hawezi kukusaidia wakati wa shida zako, huyo rafiki ni wanini? Rafiki wa story ama? Urafiki ni kwenye shida na raha. Kama huwezi mkopesha mpe. Kama huwezi mpa mwambie sina. Basi. Mimi rafiki yangu nampa hela yoyote na siwazi, ilimradi nijiridhishe kuwa na mimi nikiwa na shida nitapata
 
Hi guys,

Kiukweli hili suala limenifika shingoni, kadri muda unavyozidi kwenda naona khali inazidi kuwa mbaya, na hii tabia inazidi kuota mizizi mno, yaani sahii ukitaka uwe na uadui na mtu wako yeyote yule wa karibu wala hata usitumie nguvu kubwa, wewe ihusishe tu PESA,

Unazungumza na mtu kabisa vizuri na unamuamini vizuri mno, kila kitu kinakuwa sawa kabisa mwanzoni lakini ikija kuhusika pesa tu, unashangaa kuona vile ghafla anakuwa ni mtu mwingine kabisa usiyemfahamu, kuanzia simu hazipokelewi, text hazijibiwi, yaani mtu anaanza kuku-avoid kwa nguvu, unaweza shangaa hata unakuwa blocked kabisa..!!

Tunakosea wapi mpaka jamii yetu imepotoka kiasi hiki..!? Kwanini pesa imefikia hatua ya kututoa uaminifu kwa kiwango kikuu namna hii, kwanini watu wa karibu kabisa itugombanishe na kutufarakanikisha kufikia hatua ya kuwa maadui, mbona we were just cool kabla 'paisa' ihusike..??! Sahii ni kawaida kabisa kutukuta ni watu wa karibu mno, ila tunaogopana kama nini linapokuja suala la shilingi..!!

Doh'...! Mungu atunusuru tu, am afraid tunakoelekea ndiko kubaya zaidi...!!

👍👍👊
 
Ukitaka kuweka amani na kila mtu basi usiweke matarajio makubwa sana kwa watu.
Ukikopeaha kopesha kiroho moja kwamba fanya kama umetoa tu sadaka asiporudisha basi. Vinginevyo utavunjika moyo bure uje ugombane na kila mtu na ni ww ndiye utaonekana mkorofi.
Hii kanuni huwa inanisaidia sana. Nikitoa basi natoa tu. Isiporudi poa tu.
wacha tuanze kutembea na hii kanuni walaqhi', tupunguze haya maumivu ya moyo.!!
 
Nimejifunza roho mbaya kwasababu ya watu wasio waaminifu kwenye kulipa madeni mtu anakuja mikono nyuma na shida ilhali anajua kabisa na wewe upo juu ya mawe unajitolea kumdhamini kwa mtu akipewa hela kurudisha majanga anakuachia msala. Nitasaidia ndugu yangu wa damu ambaye najua hata nikifulia hanitupi au mpita njia najua nakua nimetoa sadaka ila rafiki sisaidii asilani bora urafiki uishe. E, S, N mlichonifanya kunibebesha madeni ya mamilioni ya shilingi na kuniacha nilipe nimewasamehe ila sitakuja kuwasahau na mmenifundisha kitu.

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
Pole sana sana mamylove, ila usijivike roho mbaya ambayo hukuwa nayo sababu ya binadamu wachache.! that's not you.!!
 
Mimi n mradi wangu mkoani,kijana naemuamini kusimamia n kununua kanipiga 4.7...cnc dec 2020 na kusepa....namtafutia nafasi lazima familia yake iuze ngombe za kutosha wanilipe sitaki riba,mwezi ujao lazima nimdake mana simu zake zote ziko hewani
Jamani,
Sasa niambie utamuamini nani maisha haya..!?
 
Asante sana Carleen na nimejifunza sana..na hapa naungana na mamylove ila natofautiana nae sehemu ndogo sana..Watu pekee ambao sitaacha kuwakopesha kamwe ni ndugu zangu...hata wasiponilipa sitaumia maana it has always been my desire kufanikiwa na kuwasaidia ndugu zangu kimaisha...I have my young bro yuko chuga..Desemba mwaka jana alibanana nikamkopesha ila hadi leo hajanilipa na siumii na wala huwa sipigi mahesabu kama kuna hela ipo kwake coz that is my responsibility as a big bro to my juniors....

Kuhusu Marafiki ni HAPANA..kuna rafiki angu mwingine nilisoma nae advance, tulivoenda chuo akaja nmkopeshe ada na kweli asingefanyiwa registration...nakumbuka ilikuwa 100k na akasema atanilipa na riba, mimi nikakataa riba ila nikamwambia akipata tu hiyo hela anilipe..na aliahidi within one month maana atapata toka hom...

Sikuona ile hela, badae anakuja ananipa namba ya mama ake niwe namdai..kwani mimi nilimkopesha mama yake?....sawa nikawa naongea na yule mama ananipa ahadi kila siku...Baadae rafk yangu akaja kunambia kuwa eti katika kumdai yule mama yake nilimtukana kwenye msg na ndio maana hataki kunilipa....Nilijisikia vibaya sana, nikamwambia nimemtukana kwa msg, basi nipo tayari twendeni polisi akashitaki..kati ya kitu siwezi kufanya ni kumtukana mama mtu mzima tena mzazi wa rafiki yangu maana hata mm sitapenda kutukaniwa mama yangu...Mwisho wa siku nilipoteza hela na urafiki....

Baada ya mwaka mmoja yule rafiki yangu akaanza kunitafuta tena..kipindi hicho tumemaliza chuo..Mambo yake yakibanan ananicheki nimsaidie hata nauli au hela ya vocha..mwanzoni nikawa na mpa ila mara ya mwisho nilimtumia ilikuwa 2000 tu ya vocha na hapo hapo nikamuuliza, hivi mshikaji, pamoja na kunidhulumu laki moja yangu na kunisingizia nimemtukana mama yako, unapata wapi ujasiri wa kunitafuta na kuniomba tena hela?.....Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kaniomba msaada yule jamaa...



NB: 'unakuta unaemwamini ndiye anakuwekea sumu, hawana alama binadamu wanaokuja kukuhukumu' - DARASA
Kitu maisha yamenifunza ni kuwa siyo lazima yakutreat vizuri hata kama wewe ni mtu mzuri.! Ila pia usiache kuwa mwema sababu ya tabia mbovu za wengine..!! Be good always Fohadi..!!
 
Mtu anapokuja kwangu na kutaka kuniazima pesa huwa nampa nusu ya kiasi anachotaka,hii uwa nafuata principle moja ya pesa inayoniambia usimpe mtu pesa ambayo huwezi kuipoteza.ukija kwangu unataka kukopa elfu 50 basi nitakwambia dah hali ngumu mwanangu Mimi Nina 20000 hapa,ukichukua ata usipolipa hainiumi kama 50000
Haha...!
Nimependa hii idea yako pia Sinanjema..!
 
Back
Top Bottom