Hivi tunajua maana ya kusalimiana au tunafanya mazoea?

shizukan

JF-Expert Member
Jan 16, 2011
1,158
563
Moja kati ya tabia zetu (Watanzania) zinazonishangaza ni namna yetu ya kusalimiana. (Na pengine salamu zenyewe)

Mfn:

A na B wameongozana pamoja, wanamkuta C kakaa nje ya nyumba yake. A anamsalimia C : Habari za saa hizi? Anajibiwa: Nzuri wkt huo huo B anamsalimia C : Habari za leo? Naye anajibiwa : Nzuri.

Kinachonishangaza: Kulikuwa na umuhimu gani kwa B kuuliza swali ambalo A ameshauliza? Nia ya B ni kutaka kujua hali ya C au anakamilisha tu mazoea?

Turudi kwenye salamu zetu: SHIKAMOO
Katika kulifuatilia hili neno kwa waliokistudy kiswahili kama fani majibu yao kwangu yalikuwa: shikamoo = nipo chini ya miguu yako. Matumizi ya neno shikamoo yalianzia ktk zama zile ambazo Waarabu walikalia maeneo ya Pwani ya A.Mashariki. Na cha kushangaza ni kwamba hawakuambiana shikamoo wao kwa wao(kwa umri) , bali wa hadhi ya chini ndio alimwambia shikamoo aliyemzidi hadhi.

Rudi ktk jamii yetu ya sasa: Shikamoo imekuwa muhimu kuliko maudhui ya salamu. Ni imani yangu kuwa lengo la kusalimiana ni kujuliana hali. Lkn cha kushangaza, ukimsalimia mzee namna hii: U hali gani mzee? utaonekana una dharau na huna adabu.Tunafarijika sana kuambiwa shikamoo bila kupata nafasi ya kuwaeleza walio mbele yetu juu ya hali zetu.

Kingine na cha mwisho (kwangu, naamini wengine mtakuwa na mengi) ni haya mazoea ya kuitikia: NZURI!
Haya mazoea nayo yananiacha hoi. Unakwenda kwa mtu na umuulizapo hali yake atakwambia nzuri. Mbele huko katika mazungumzo si ajabu akakwambia, "usinione naongea hapa, nina homa kali ndugu yangu...na jana usiku kucha nimekohoa kama mbwa aliyemeza mjusi". Sasa hebu jiulize, ile 'nzuri' ilimaanisha nini? Je, msingepata wasaa wa kuendelea na stori ungeyajua yote haya ya mtu kukohoa kama mbwa aliyepaliwa na mate akibweka umbea (R.I.P Mr.Ebbo)?

Twende kazi wana JF...
 
huwa sipendi 'shikamoo'. Unawambia mtu nipo chini ya miguu yako,chini ya miguu ya huyo mtu unafanya nini? Kama hajavaa underwear je?
Ila napenda kutumia salamu ya kilugha chetu
 
Hii ya kusema nzuri wakati hali ni mbaya huwa inatumika ili kutokumshtua mtu, isitoshe siyo kila unayekutana naye unapaswa kumweleza matatizo yako ndo mana unajibu nzuri ili mambo mengine yaendelee...
 
Watanzania wa Pwani hasa wilaya ya Rufiji kijiji cha Nyaminywili wanalijua hili tatizo hasa la neno "Shikamoo" katika salamu linakuwa la mwisho. Shikamoo halipewi uzito sana. Ndiyo maana utamkuta mtoto wa miaka 10 ana msalimia mtu mzima wa miaka hamsini hivi:

Mtoto: Habari za leo Baba/Mama Zai,
Mtu mzima: Nzuri
Mtoto: Zai hajambo?
Mtu mzima: Hajambo.
Mtoto: Shikamoo.
Mtu mzima: Marahaba mwanangu.
 
Labda bara huko....huku pwani sie tunasema 'salam aleikum'? Unaitikia '(w)aleikum salam'....simple!
 
Mimi binafsi si ipendi kabisa shikamoo. Unakuta mtu kakuzidi sana anakupa shikamoo eti kisa una pesa..Kama sio utumwa wa fikra ni nini?
 
Mwanamke: taspota
Mwanaume: maspoteige
hizo salamu za mchana hadi usiku na asb ni hivi
mwanamke: tatuleilota
mwanaume: matuleilotaige
 
Yani mnataka kucomplicate mpaka salamu sasa?
Kwani mtu akijibu safi huku kichwa kinamuuma kwenye tatizo gani?Unataka kila wanaekutana nae wajue ye mgonjwa?
 
Yani mnataka kucomplicate mpaka salamu sasa?
Kwani mtu akijibu safi huku kichwa kinamuuma kwenye tatizo gani?Unataka kila wanaekutana nae wajue ye mgonjwa?

Si lazima wawe woote, lkn je walio karibu huwa unawaambia kwanza au unasema safi na baadaye ndio unasema kama unaumwa?
 
Labda bara huko....huku pwani sie tunasema 'salam aleikum'? Unaitikia '(w)aleikum salam'....simple!

Sisi huku kwe2 2nasalimiana ki kwe2 "good morning,good afternoon,good evining" .....simple
 
mmmh, kwa kiswahili na inglish naishi kwa mazoea
ila kilugha naelewa nilitendalo
 
moja kati ya tabia zetu (watanzania) zinazonishangaza ni namna yetu ya kusalimiana. (na pengine salamu zenyewe)

mfn:

a na b wameongozana pamoja, wanamkuta c kakaa nje ya nyumba yake. a anamsalimia c : habari za saa hizi? anajibiwa: nzuri wkt huo huo b anamsalimia c : habari za leo? naye anajibiwa : nzuri.

Kinachonishangaza: kulikuwa na umuhimu gani kwa b kuuliza swali ambalo a ameshauliza? Nia ya b ni kutaka kujua hali ya c au anakamilisha tu mazoea?

turudi kwenye salamu zetu: shikamoo
katika kulifuatilia hili neno kwa waliokistudy kiswahili kama fani majibu yao kwangu yalikuwa: shikamoo = nipo chini ya miguu yako. matumizi ya neno shikamoo yalianzia ktk zama zile ambazo waarabu walikalia maeneo ya pwani ya a.mashariki. Na cha kushangaza ni kwamba hawakuambiana shikamoo wao kwa wao(kwa umri) , bali wa hadhi ya chini ndio alimwambia shikamoo aliyemzidi hadhi.

Rudi ktk jamii yetu ya sasa: Shikamoo imekuwa muhimu kuliko maudhui ya salamu. ni imani yangu kuwa lengo la kusalimiana ni kujuliana hali. Lkn cha kushangaza, ukimsalimia mzee namna hii: u hali gani mzee? utaonekana una dharau na huna adabu.tunafarijika sana kuambiwa shikamoo bila kupata nafasi ya kuwaeleza walio mbele yetu juu ya hali zetu.

Kingine na cha mwisho (kwangu, naamini wengine mtakuwa na mengi) ni haya mazoea ya kuitikia: nzuri!
haya mazoea nayo yananiacha hoi. Unakwenda kwa mtu na umuulizapo hali yake atakwambia nzuri. Mbele huko katika mazungumzo si ajabu akakwambia, "usinione naongea hapa, nina homa kali ndugu yangu...na jana usiku kucha nimekohoa kama mbwa aliyemeza mjusi". sasa hebu jiulize, ile 'nzuri' ilimaanisha nini? Je, msingepata wasaa wa kuendelea na stori ungeyajua yote haya ya mtu kukohoa kama mbwa aliyepaliwa na mate akibweka umbea (r.i.p mr.ebbo)?

Twende kazi wana jf...

kwa kweli nimeipenda hii
 
Ndo maana huwa tunaishia kusema 'mhola' na gawiza kisha kila mmoja anaendelea na mambo yake
 
Back
Top Bottom