Kuna Mke au Mume ukimuacha umekula hasara ya Maisha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
Anaandika, Robert Heriel

Acheni kabisa, yaani kuna mtu kwenye mahusiano ukiachana naye hesabu umekula hasara ya Maisha. Achana na hawa wajingawajinga wanaowaza uchi wao, uchi kitu gani bhana! Uchi hata Malaya anao. Kwani ni Mwanamke gani asiye na uchi?

Kwa kweli uzoefu wangu Mwanamke Hana uwezo wa kuniringia uchi Kwa sababu uchi unapatikana muda wowote. Kwa upande wa wanaume ni wachache wenye mawazo ya kufikiri Mashine zao ndio silaha zao. Vyovyote iwavyo iwe ni Mwanamke au Mwanaume mwenye mawazo ya namna hiyo hata akikuacha huyo hujala hasara kubwa.

Ikiwa Mkeo anatabia hizi basi mng'ang'anie, kwani siku akikuacha basi utakuwa Umepata hasara kubwa ya Maisha;

1. Mcha Mungu na utamjua kwa sifa zifuatazo;
a) Ni mtiifu, na anakusikiliza.
b) Mama wa Maombi na ibada.

Jioni Mkeo huendesha ibada na watoto hata kama haupo, anaomba na kukuombea. Anakusisitiza ibada kulingana Imani yenu. Na hachoki.

Sio limwanamke halikumbuki mara ya mwisho limekuombea lini.
Familia yenye maombi lazima iwe na umoja na NI rahisi kutatua matatizo yenu.

Hakuna kitu kizuri kama umeenda kutafuta Pesa alafu unajua nyumbani kuna Mwanamke anakuombea, alafu unajua wazazi nao wanakuombea. Usipofanikiwa wewe niite Mimi Mbwa, lakini Mkeo hakuombea, wazazi nao hawakuombei lakini wao ndio wakwanza kukulalamikia na kukulaumu. Hapo hesabu hasara kubwa.

c) Mpenda Amani na utulivu na anayekuamini.
Mke mcha Mungu anapenda Amani na utulivu. Sio umeoa limwanamke muda wote linawaza kuwa unali-cheat yaani

2. Anayejua Bajeti na kuthamini Jasho Lako.
Mke anayejua Bajeti na kuthamini Jasho Lako huyo sio mbinafsi. Sio Yale mamianamke yanayokugeuza msukule wao. Yaani lenyewe ulilishe na lipendeze bila kukujali unapataje Pesa zako. Unakuta kimwanaume kimekonda na kufubaa kisa upumbavu.

Mke wa maana anathamini Pesa yako kama mumewe. Kila Pesa anaionea uchungu Kwa sababu ni Mali ya mumewe aliyoitolea jasho.

Mwanamke wa hivyo ukimpata alafu ukaachana naye hesabu umekula hasara kubwa Mno.

3. Mwenye Elimu ya Maadili ya Dini na Dunia.
Unarudi zako nyumbani unakuta Mkeo anawafunza Watoto maadili, anawafunza jinsi Dunia ilivyo na inavyoenda. Unaishia tuu kutabasamu. Unamkumbatia Mkeo na watoto kisha unaungana nao lakini unaacha Mama/Mkeo aendelee kuwa mwenyekiti.

MKE anafundisha Watoto maadili yaliyobora sio Maadili ya kitumwa au yakizamani. Moyoni unasema hapa MKE nimepata hata nisipokuwepo Watoto wangu wanamama Bora, watakua kwenye maadili.
Sio limwanamke halijui A wala B lipolipo tuu!

4. MKE Mfanyakazi au mfanyabiashara.
Mke anayejua kuwa kazi ni kipimo cha UTU. Kwamba kila Mwanadamu mwenye afya lazima afanye kazi na achangie mapato ya Familia. Mke ambaye anajisikia vibaya kuona anakaa tuu nyumbani pasipo kuzalisha Mali. Huyo ni MKE Bora.

MKE anayejisikia fahari kukusaidia na kuikuza familia yenu kimapato na kiheshima ndani ya jamii. Sio ,wanamke mpuuzimpuuzi anayeweza kugongwa tuu. Huyo hafai na hata mkiachana hutoona hasara yoyote Ile Kwa sababu Kikawaida uchi unazoeleka.

Ila kuachana na Mwanamke mchapakazi na mzalishaji hapo hesabu umekula HASARA kubwa, hasara ya Maisha. Kikawaida ukiwa na MKE mwenye Sifa hizo ni lazima uwe na watoto walionyooka, na uzee wako upo salama.

Lakini ukiwa na Mwanamke asiyeeleweka anayeweza kujipanua tuu ati ndio anachoweza hapo upo hatarini, sio wewe tuu Bali na kizazi chako kipo mashakani.

5. Mke anayekusaidia na mnayesaidiana
Kikawaida akishakuwa mchamungu, na Sifa nilizozitaja Huko juu, automatically atakuwa msaada mkubwa kwako. Yaani mtaishi zaidi ya Ndugu. Chochote mnachozalisha NI chenu, na hakuna ubinafsi. Ukiona mwanaume yeyote aliyefanikiwa na anaonekana anakuogopa Mkewe basi elewa huyo Mkewe anasifa nilizozitaja hapo.

Jamani MKE wa Aina hiyo anaogopesha hata kum-cheat inakuwa Kwa mbinde, wanaume wengi huhofia kuwa disappoint wake zao wenye sifa tajwa hapo juu.

Hivi utampata wapi Mwanamke mwenye Sifa kama hizo ikiwa uliyenaye utaachana naye? Hapo ndipo wanaume wengi wapo radhi waombe Msamaha na kupiga magoti lakini wasiachane na Wanawake zao WA maana. Kwani wanajua NI hasara kubwa kuachana na chuma kama hicho.

Bahati nzuri Wanawake WA Aina hiyo wengi hujijua jinsi walivyo. Na sio rahisi kufanya maamuzi magumu na wengi hutoa nafasi ya pili mpaka yatatu lakini siku wakiondoka wengi huondoka bila kurudi Nyuma.

Haya hivi unatuachaje wanaume wa aina yetu? Wanaume ambao kutupata ni mpaka chozi lako Mungu alione!
Wanaume wenye sifa hizi;

1. Wapole na waungwana
2. Wanaomjua Mungu na kumpenda
3. Wanaotafuta Pesa Kwa nguvu zote
4. Wasiopenda ku-cheat na Hawana mambo mengi kwani walishamaliza uchafu huo.
5. Familia kwetu ni Jambo la Kwanza, na wake zetu ni marafiki zetu.
6. Wanaodekeza Wake zao na kuwachukulia kama malkia.
7. Wanaofundisha Wake zao Njia njema ziwapasao.
8. Wanaowawezesha Wake zao kiuchumi ili wajitegemee ili hata siku tukiachana iwe Kwa kifo au Talaka Mwanamke awe anaweza kujisimamia wenyewe. Sisi hatuonei Wivu Wanawake zetu. Kwa sababu tunajiamini.
9. Wanaowapa Wanawake Uhuru WA kufanya mambo yanayowafurisha ilimradi wasivunje maadili na Sheria za nchi. Hakuna kumbana MTU. Kumuoa Mwanamke haimaanishi kuwa ni mtumwa wetu.

Ukiachana na wanaume kama Sisi Wanawake wengi huzihesabu kama hasara za Maisha Yao.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Anaandika, Robert Heriel

Acheni kabisa, yaani kuna mtu kwenye mahusiano ukiachana naye hesabu umekula hasara ya Maisha. Achana na hawa wajingawajinga wanaowaza uchi wao, uchi kitu gani bhana! Uchi hata Malaya anao. Kwani ni Mwanamke gani asiye na uchi?



Kwa sasa Dar es Salaam.
Labda kama ume muumba ww
 
Hizo tabia zote inatakiwa zipatikane ndani ya mtu mmoja? Au hata akiwa na sifa moja tu kafi ya hizo?
 
Kwa miaka hii ni vigumu mno kumpata mwanamke aliyetimia kiasi hiko
 
Hizi tabia tajwa kwa hazipatikani kwa wanawake au wanaume wazuri kwa mambo na sura, hapa ndio changamoto kubwa ilipo.,Vijana wengi huangalia mambo hayo sana kabla ya ndoa na kuacha vigezo muhimu kabisa.
 
Anaandika, Robert Heriel

Acheni kabisa, yaani kuna mtu kwenye mahusiano ukiachana naye hesabu umekula hasara ya Maisha. Achana na hawa wajingawajinga wanaowaza uchi wao, uchi kitu gani bhana! Uchi hata Malaya anao. Kwani ni Mwanamke gani asiye na
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Kama ex wang anavyojuta huko na bado
 
Anaandika, Robert Heriel

Acheni kabisa, yaani kuna mtu kwenye mahusiano ukiachana naye hesabu umekula hasara ya Maisha. Achana na hawa wajingawajinga wanaowaza uchi wao, uchi kitu gani bhana! Uchi hata Malaya anao. Kwani ni Mwanamke gani asiye na uchi?



Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Hakika!. Hivi tycoon ninaweza kufanya nini kuzivutia roho/miungu yenye nguvu inibariki?
 
Akiwa na hayo yote halafu mizagamuano hatoi ni kazi bure. Nilimuacha wa hivyo.
Akili ni zangu atazitumia kikubwa afuatishe maelezo yangu.
 
Back
Top Bottom