Hivi Serikali hii ya Awamu ya 5 imeshindwa kweli kumshika na kumshtaki mtu anayeitwa Kigogo2014?

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
1,214
2,000
Wakuu Salaam;

Wapo watu wengi wameshikwa na kupelekwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ya kimtandao.

Juzi kadakwa Idriss na hakieleweki hadi saivi, shauri lake linasoma ni makosa ya mtandaoni.

Waandishi wa Habari, Viongozi wa vyama vya upinzani imekua ni rahisi sana kuwaita kituoni na kuwapeleka mahakamani ikibidi pale ambapo wanaandika maudhui ya aina fulani mtandaoni. Hali hii imefanya pia wengine kupata kesi zilizobadilisha taswira ya siasa kutokana na hukumu zilizotolewa kwa wahusika.

Hali ni tofauti kwa mtu anayejiita Kigogo2014 anayetumia mtandao wa Twitter sana kuposti mambo mbalimbali, mengine yana kejeli kwa Mkuu wa nchi na sekta mbalimbali na hata viongozi husika.

Juzi kadakwa Mdude, na pia alishawahi shikwa na kuteseka kisa ishu ileile ya maudhui mtandaoni na hili kila mtu anakumbuka.

Mifano iko mingi kwa viongozi wa siasa hasa wa vyama vya upinzani waliopata kesi hizo.

Kwanini hii awamu ya 5 ya JPM isiojaribiwa kama anavyosema iliyopitisha sheria kuhusu matumizi ya mtandao imeshindwa kumshika mtu anayeitwa Kigogo2014 ilihali inaweza shika wengine kirahis tu?
 

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,814
2,000
Kama mange kimambi walikua wanamjua sura, wanafahamu anapoishi wnawajua watoto wake na ndugu zake na aliwasumbua for years kila siku akizusha kitu kipya na kuzua taharuki kila siku. Hadi siku moja akawafanya polisi kama watoto wadogo kwa kuwapigisha kwata nchi zima huku wakizunguka na silaha za kivita mitaani lakini walimshindwa.

Sasa watamuweza mtu ambaye hawamjui jina wala sura?
 

mwamwala iyunga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
923
1,000
Huyo hana lolote, ametumia corona kuleta uchonganishi kati ya serikali na wanannchi /mataifa ya nje, ameshindwa, sasa amehamia kwenye kudai kua anatafutwa , mara sijui fulani ns fulani wamekaa vikao vya kumkamata, ndicho anachoweza huyo fara kufanya hasaidii chochote na wala hawasaidii Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona povu hivyo mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
1,214
2,000
Uliza serikali mwaka wa 5 huu haijapabdisha mishahara kwa watumishi wake..hayo ndio mambo ya kuhoji
Unafikiri kila mtu ana njaa na kutegemea mshahara kama wewe. Mi siwezi tetea mshahara kwasababu sili huko.
Wewe anzisha mada yenye kilio cha mshahara ndiyo mlie wote humo pamoja.

Eagles never flock but pigeons do.

You are a pigeon.
 

Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,527
2,000
Kama mange kimambi walikua wanamjua sura , wanafahamu anapoishi wnawajua watoto wake na ndugu zake na aliwasumbua for years kila siku akizusha kitu kipya na kuzua taharuki kila siku. Hadi siku moja akawafanya polisi kama watoto wadogo kwa kuwapigisha kwata nchi zima huku wakizunguka na silaha za kivita mitaani.. lakini walimshindwa.

Sasa watamuweza mtu ambaye hawamjui jina wala sura
Vipi unaweza kutuambia yuko wapi huyo mambi wenu?

God save us
 

X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
584
1,000
Huyo mpuuzi tu hana lolote, ametumia corona kuleta uchonganishi kati ya serikali na wanannchi /mataifa ya nje, ameshindwa, sasa amehamia kwenye kudai kua anatafutwa , mara sijui fulani ns fulani wamekaa vikao vya kumkamata, ndicho anachoweza huyo fara kufanya hasaidii chochote na wala hawasaidii watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu swali kwanini hajakamatwa hadi sasa?
 
Top Bottom