Waandishi wajengewa ujasiri kupambana na changamoto katika majukumu yao

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
1694283478510.png

Waandishi wa habari licha ya kuwa watu muhimu katika jamii lakini wamekuwa katika mazingira ambayo siyo mazuri wanapokuwa.wakitekeleza majukumu yao ya kuhabarisha Umma kwani miongoni mwao kupata vitisho wengine kutekwa na wengine kufikishwa katika vyombo vya sheria wakiwa wanadai haki zao hivyo serikali na wadau mbalimbali hawana budi kuangalia watu hao kwa jicho la tatu.

Yamebainisha hayo jijini Dar es Salaam katika mafunzo ya kujenga Ustahimilivu na Uwajibikaji wa Kidigitali kwa waandishi wa habari katika mafunzo hayo changatomo mbalimbali zilitolewa ikiwemo suala la mikataba ,bima za afya wanaomiliki vyombo vya habari wao wamekuwa wakiangalia maslahi yao hivyo waandishi wameshauriwa kuangalia fursa zilizopo mtandaoni kwa maudhui wanayotengeneza wakifanya kwa weledi wataondokona na dhana ya kuajiriwa badala yake kujilipa kupitia intaneti.

Akifafanua katika mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums , Maxence Mello amesema matukio mengi wamekuwa wakikabiliana nayo kutokana na kuandika ukweli kuhusu masuala mbalimbali yanayotendwa na baadhi ya viongozi wa serikali hivyo kupelekea kupewa vitisho vya kuomba radhi wengine kutekwa na kutishiwa maisha hivyo pamoja na hayo yote wanakosa watetezi wengine kuwekwa gerezani na kubambikwa makosa ambayo hawayakutenda hivyo amewasihi wawe wajasiri Mungu atawapigania.

” Mmeshuhudia kwa masikio na macho yenu mimi kilichonikuta miaka ya nyuma na nilikaa gerezani kwa kesi mbalimbali na haku na kule nikapata wanasheria wa kujitegemea wakanisimamia kesi zilizokuwa zikinikabili huku gazeti fulani la kimkakati likiandika vibaya kunishafua nikakamatwa na kuwekwa ndani kesi isiyokuwa na dhamana kutishia kumuua rais aliyeko madarakani lakini niko mbele yenu namshukuru Mungu amenisimamia na sasa bado nasonga mbele kutetea haki hivyo niwasihi changamoto zipo msikate tamaa”amesema Maxence.

Sambamba na hayo amewashauri waandishi kutokuwa na itikadi ya chama chochote kuzingatia miiko na sheria za uanndishi wa habari ziliziwekwa kuachana na uchawa kwani ili maudhui wanayaoandika wasiwe wanapendelea kwani kesho ni fumbo pia amesisitiza kuwa na usiri wa taarifa za watu simu au vifaa wanavyotumia wawe navyo makini kuepukana kutumia bando la bure kwani ni hatari kutokana na kazi zao.

Sanjari na hayo kunafursa iliyopo kupitia mtandao lakini wawe wabunifu wa maudhui kulingana na mitandao pasipo kwa kuzingatia miiko na taratibu za kisheria zilizowekwa kwani Tanzania sheria zimekuwa zikitungwa na kutolewa maoni na ikiwa na matatizo hurekebishwa wakati mwingine hufutwa hivyo yeye kwa kuwa amepitia changamoto nyingi kutokana na Maudhui ya kimtandao ametoa elimu ya ujasiri wa kusimama bila kuwa na itikadi ya chama chochote

Naye mwakilishi kutoka kituo cha Sheria na Binadamu Wakili Fulgence Massawe amesema nchi nyingi za Afrika katika suala la digital vyombo vya habari hakuna uhuru wa kujieleza sheria ipo lakini maadhui yakandikwa huambiwa wafute kilichoandikwa au kuandika makala tatu mfululizo za kilichoandikwa au kuomba radhi wakati mwingine vyombo hivyo kupigwa faini au kufungiwa na mamlaka husika.

1694283591171.jpeg

‘Sisi wanasheria tumekuwa na kesi nyingi za Waandishi wa habari tuliokuwa tunaenda mahakamani kusaidia kesi zao na Wakashinda ikiwemo Eric Kabendera, Maxence Mello wote hao lakini hakuna kesi hata Moja tuliyomwona muajiri akija kutoa ushirikiano walikuwa wanajivua na kuendelea. na. shughuli zao lakini kesi hizo tulishinda” amesema. Wakili Masawe

Naye Wakili kutoka. Watetezi wa Haki za binadamu THRDC Nuzulack Dausen amesema sheria zipo lakini nao hawana budi kukaa meza Moja na waajiri wao kuangalia namna ya mikataba yao bima za. afya kwani hivyo ni vitu muhimu lakini walio wengi waajiri hawajali.

Aidha licha ya Jitihada na juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha miundombinu inaboreshwa lakini bado baadhi ya maeneo suala mawasiliano limekuwa changamoto hivyo ile dhana ya Dunia kuwa kijiji kupitia digitali imekuwa historia inahitaji jitihada za makusudi zifanyike kusaidia hilo.

Pia ni jukumu la Serikali kuhakikisha watu wote wanapata mawasiliano popote walipo internet inapatikana masaa 24 huku umeme nao ukiwa wa uhakika kwani vitu hivyo viwili vinategemeana na sasa kupitia teknolojia iliyopo Vijana walio wengi wamekuwa wakijiajiri kipitia Mitandao kufanya biashara , wengine kutuma maudhui mbalimbali na wengine ambapo wameachana dhana kutegemea kuajiriwa wamejiajiri kupiti blog ,YouTube,Instagram,Twitter.

1694283553909.jpeg


Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Chanzo: Jamhurimedia
 
Back
Top Bottom