Hii issue ya Daladala na Bajaji Arusha serikali ya mkoa imeshindwa

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,157
Tulishuhudia mgomo wa daladala za kutoka Morombo kwenda mjini Arusha, wakaahidiwa kulishughulikia. Wakiwa ktk mchakato wa kulishughulikia bajaji wakaandamana, serikali ikawagwaya, imewaogopa maana waliitishia serikali kuwa watarudia kazi yao ya kuvunja na kuiba. Nafikiri Rais angewaondoa hao viongozi wote wa mkoa wa Arusha John Mongela ameshashindwa kuliongoza jiji la Arusha. Bajaji nyingi hazijasajiliwa na zimetoka maeneo mengine ya nchi. Nchi ni km haina uongozi. Serikali isimamie sheria km viongozi walivyoapa.

Ndio maana sazingine watu wanasema serikali hii imeshindwa kuongoza, viongozi wanaogopa kutoa maamuzi. Vyombo vingi vya usafiri ni vya viongozi, nani atoe uamuzi labda rais au waziri mkuu pekee. Arusha imeoza, viongozi ndio wenye daladala na bajaji, ndio utamkumbuka baba wa Taifa alivyopiga marufuku viongozi kufanya biashara, matokeo yake ndio haya. Kiongozi analipwa mshahara na marupurupu mengine kwa kodi ya mwananchi, kiongozi huyo huyo ndio amewekeza kwenye biashara, kwanza ana access ya kupata hela kwa kujichukulia mkopo mkubwa benki, pili ndio wakwepaji wakubwa wa kodi. Polisi wengi ndio wenye vyeo vikubwa ndio wamiliki wa hivyo vyombo.

Azimio la Arusha bado ni muhimu sana, kiongozi achague kimoja kufanya biashara au utumishi wa umma. Ndio maana wananchi wanashindwa kumsahau Magufuli, rais wangu ukicheka sana na hawa watu utashindwa kuongoza nchi. Kwa kuanzia waziri mkuu aingilie jambo hili, viongozi wote wakubwa wahamishwe Arusha kuanzia mkuu wa Mkoa. Bajaji zifuate sheria, zibaki kuwa vyombo vya kukodishwa km taxi, angalia walivyokuwa na kiburi nauli badala ya 500, leo wanachaji 1000 bila kujali habari ya mwanafunzi maana hata mwanafunzi wanamchaji 1000 badala ya 200. Hii nchi ina uongozi kweli? Au jiji la Arusha ni nchi inayojitegemea km Somali land? Maana ni vurugu tu hakuna order yoyote inayofuatwa, si polisi, si mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa yuko busy kupokea wageni, amekuwa km receptionist.

Tunasubiri kauli thabiti ya viongozi wakubwa iliyojikita ktk kutii sheria na taratibu za mipango miji. Watu wasijitetee eti watafanya shughuli gani ili kufanya uhalifu, kazi halali ziko nyingi, kuna kilimo, kuna ufugaji, kuna kazi kem kem zilizo halali. Tatizo lingine ni mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo, huyu ana bajaji nyingi, anazitumia kujipatia kipato ila hasa lengo kuu ni kuzitumia ktk uchaguzi ujao kwa kuwatumia wale vijana waendesha bajaji km mtaji wake wa kisiasa. Anausumbua sana uongozi wa mkoa wa Arusha, wamewagawa wananchi. Serikali iweke msimamo uliojikita ktk sheria bila kumtazama mtu usoni wala kujali madhara ya muda mfupi.
 
Duh poleni sana. Hivi vimigomo vya vyombo vya usafiri visikie tu.
Wayback viligoma hapa Dar hafu nakaa Komgowe ya kule Mbagala. Mbona niliimba.
 
We ona akili za CCM ingekuwa ni mkutano wa Chadema kuhusu masuala ya bandari wangekodi hata polisi wa Mkoa jirani. Ila mgogoro wa daladala unawashinda
 
Back
Top Bottom