Hivi Rais Samia anawezaje haya yote?

Hivi Rais Samia anawezaje haya yote?

Chini ya Rais Samia amana zimefikia TZS 42Trilioni,

Tuulizane mama amewezaje yote haya?

Wakati Rais Samia anaingia madarakani Tanzania ilikuwa na kiasi cha amana(deposits) kwa fedha za ndani (TZS) na amana kwa fedha za kigeni ($) jumla ya TZS23Trilioni mwaka 2020, Kiasi hiki pamoja na amana za Seiikali kilifikia jumla ya TZS 24Trilioni kwa mwaka 2020.

Mwaka 2024 kiasi hicho cha amana kiliongezeka na kufikia TZS40Trilioni kwa fedha za ndani na fedha za kigeni,Wakati pamoja na amana za serikali kiasi hiki kilifikia TZS42Trilioni, Hivyo chini ya Rais Samia amana ziliongezeka kwa TZS18Trilioni sawa na 75%.Hiki ni kiashiria kuwa Watanzania wana pesa za kula na kusaza na kuweka kwenye akaunti zao za amana

Mambo 20 Chini ya Rais Samia​


  1. Diplomasia ya Uchumi – Amefungua Tanzania kwa dunia, kurejesha mahusiano mazuri ya kimataifa na kuvutia wawekezaji.
  2. Miradi ya Maji – Utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji vijijini na mijini, kuhakikisha wananchi wanapata huduma safi na salama.
  3. Sekta ya Afya – Ujenzi na ukarabati wa hospitali, vituo vya afya na zahanati nchi nzima; kuongeza vifaa tiba na dawa.
  4. Sekta ya Elimu – Kuondoa ada kwa shule za sekondari hadi kidato cha sita na ujenzi wa shule mpya pamoja na mabweni.
  5. Barabara na Miundombinu – Ujenzi na ukarabati wa barabara kuu na za vijijini, madaraja na barabara za mchepuo mijini.
  6. Mradi wa Umeme Vijijini – Upanuzi mkubwa wa REA unaowafikia wananchi wengi zaidi vijijini.
  7. Umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) – Kuendeleza mradi wa umeme wa megawati 2,115 kwa maendeleo ya taifa.
  8. Uboreshaji wa Shirika la Ndege (ATCL) – Kununua ndege mpya na kuongeza safari za kimataifa.
  9. Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) – Kuendeleza mradi wa reli ya umeme kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
  10. Uwekezaji katika Bandari – Kuboresha bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ili kuongeza biashara na mapato.
  11. Ajira kwa Vijana – Kupitia miradi ya kilimo (Building a Better Tomorrow – BBT) na sekta nyingine.
  12. Kilimo na Chakula – Kutoa ruzuku ya mbolea na pembejeo, kuanzisha Programu ya Kilimo cha Kibiashara.
  13. Mikopo ya Halmashauri 10% – Kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu.
  14. Mapambano dhidi ya Ufisadi na Rushwa – Kuimarisha uwajibikaji na uwazi katika taasisi za umma.
  15. Sekta ya Madini – Kuboresha mikataba ya madini ili Tanzania inufaike zaidi.
  16. Michezo na Sanaa – Kuwezesha vijana kushiriki kimataifa na kuanzisha mfuko wa kuendeleza sanaa.
  17. Afya ya Mama na Mtoto – Kujenga vituo vya kisasa vya huduma ya dharura na kuongeza watoa huduma.
  18. Mfumo wa Kidigitali Serikalini – Kuongeza matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma.
  19. Utalii na Hifadhi za Taifa – Kutangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu, promosheni na uwekezaji.
  20. Amani na Umoja wa Kitaifa – Kuimarisha mshikamano wa kijamii, kisiasa na kuendeleza majukwaa ya mazungumzo ya kitaifa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom