Hivi Precision Air mna akili kweli?

Hivi Precision Air mna akili kweli?

Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
14,084
Reaction score
8,400
Hivi inakuaje mtu amekata tiketi na kulipia kwa wakati, halafu kufika Airport mnasema hakuna ndege mpaka kesho yake? Huu ni ubabaishaji uliotukuka kabisa, inakera na kuudhi na kushusha hadhi ya usafiri wa anga. Inakuaje kuwe na over booking??

Mnafanya usafiri wa ndege sio wa kutumainia tena, mathalan mtu anaenda kwenye usaili ama anaunganisha ndege kesho yake- ni kiasi gani atapoteza dira ya safari nzima? Inakera sana na ndio maana watu weupe wanatudharau kwa kutokua makini na mipango yetu.

Haya, mtu kacheleweshwa sawa, mnampeleka hotel ya kichochoroni huko, mkitamba 'eat and drink' whatever you like, all bills will be shout out by us! Very low standard accomodation, aibu sana na bahati mbaya Tanzania hakuna Consumer Bureau, watu kwenda kulalamika.

Huo ni ujuha, upuuzi na mnajitakia laana kwa kupotezea watu kazi, biashara na mipango yao. Ninashauri hii kampuni ichunguzwe na hata boss wao ajipange upya. Hivi Precission Air mna akili? Dunia ya leo kuwe na over booking na kuacha abiria kweli??

Mnaudhi sana
 
Pole sn ndugu hata mimi mke wangu ilimkuta. Tena yeye walimwambia baada ya wiki mbili ndiyo ndege itakuwepo au atarudishiwa pesa yake. Sasa kilichotokea hiyo pesa tuliipata baada ya miezi miwili...
 
umeanza na hakuna ndege....umemaliza na over booking?

Safari hatua....punguza munkari...
 
Hayo mambo yapo kila mahali mkuu,, sasa Kama ndege imepata tatizo unataka upelekwe na nini?? Unatakiwa kuelewa tu. Na uzuri unapewa option ya ndege inayofuata ya safari yako.
 
umeanza na hakuna ndege....umemaliza na over booking?

Safari hatua....punguza munkari...

Mkuu ishu ni kusafiri kwa schedule yako na sio yao, haijalishi sababu lakini mwisho wa siku ni HAKUNA ndege ya kufanikisha safari yako.

Badilikeni acheni ukanjanja wa kipuuzi mnashusha hadhi usafiri wa ndege
 
me cjawahi kusafir kwa ndg lakn ndug zangu wamekuwa wakillalamik hebu tubalike p/Air
 
Jerrymsigwa

Mkuu pole, nadhani sijakuelewa vizuri,umesema ndege wame ghairisha ukimanisha siku hiyo ndege haikuondoka kama nimekuelewa vizuri... kama tatizo ni hilo na umefika airport ontime unatakiwa upewe hotel gari yakukupeleka chakula na gari ya kukurejesha tena airport na airport au waku fanyie booking na ndege nyengine hayo yote ni juu yao ndio ilivyo.

Overbooked flight sijui kwa shiriki hilo lakini inavyotakiwa wakupe offer kama hiyo apo juu na tkt nyengine ya Bure as long as unayo booking ya siku iyo na umefika airport ontime,mambo ya ku overbook flight ni normal kwa airline lakini wajue njia yakuwaridhisha Passenger wao kwa kauli nzuri na service kama hizo.... pole sana.
 
Last edited by a moderator:
Wanachosema wao ni kua sio kila anaefanya booking basi atasafiri sababu mara nyingi kunakuaga na "No Show" hivyo kujikuta wakienda pungufu.

Sasa basi overbooking hua inakuwepo kwa ajili ya ku-cover hizi "No Show". Labda tatizo ni kua issue nzima ya No Show in uncertain tu, hivyo inaweza iwepo au isiwepo. Ikitokea wote mmekuja ndio matatizo kama haya hutokea.
 
mimi hao jamaa sina hamu nao kabisa wajaalaaana wakubwa waliniweka KIA siku mbili nakwenda nakurudi yaani nilishaachana nao kabisa juzi nilijaribu tena wakanifix tena,ndege ya kuondoka saa 1 usiku kwenda KIA tuliondoka saa sita usiku..Hapo ndio nimekoma kabisa sirudi hata kwa dawa bora nisafiri na gutta
 
Umenisikitisha sana.
Kwa hiyo unakubaliana na hizi overbookings kama za ngorika na unatuaminisha it is a standard procedure?
Wanachosema wao ni kua sio kila anaefanya booking basi atasafiri sababu mara nyingi kunakuaga na "No Show" hivyo kujikuta wakienda pungufu.

Sasa basi overbooking hua inakuwepo kwa ajili ya ku-cover hizi "No Show". Labda tatizo ni kua issue nzima ya No Show in uncertain tu, hivyo inaweza iwepo au isiwepo. Ikitokea wote mmekuja ndio matatizo kama haya hutokea.
 
Hayo mambo hapo kila mahali mkuu,, sasa Kama ndege imepata tatizo unataka upelekwe na nini?? Unatakiwa kuelewa tu. Na uzuri unapewa option ya ndege inayofuata ya safari yako

Hawa siyo kwamba ndege ina matatizo,kama safari yako ni saa nne mchana ndege uliyopangiwa unakuja halafu inapiga rout zingine ambazo hazipo kwenye ratiba,ndo ije sasa kwa safari husika
 
Umenisikitisha sana.
Kwa hiyo unakubaliana na hizi overbookings kama za ngorika na unatuaminisha it is a standard procedure? Kaombe kazi air zimbabwe aisee, wayakupa ukurugenzi.

Wenzetu wametuacha mbali sana,panda kitu kama Emirates,qatar airways,Egypt,Turkish airways.

Ukichelewa unaachwa,mda wa kuingia ni ule ule,na kuondoka na kufika ni ule ule.
 
Hata kama kuna wasafiri wa akiba huwa wanakuja airport at their own risk. Mtu asipo-check in kwa wakati ndio anachukuliwa. Hii ya over booking ni uhuni wa kiswahili. Mtu akishaconfirm booking yake ana haki ya kusafiri
Wenzetu wametuacha mbali sana,panda kitu kama Emirates,qatar airways,Egypt,Turkish airways.

Ukichelewa unaachwa,mda wa kuingia ni ule ule,na kuondoka na kufika ni ule ule.
 
Hata kama kuna wasafiri wa akiba huwa wanakuja airport at their own risk. Mtu asipo-check in kwa wakati ndio anachukuliwa. Hii ya over booking ni uhuni wa kiswahili. Mtu akishaconfirm booking yake ana haki ya kusafiri

Ni tamaa za hela na uswahili,wangejenga uaminifu mbona wateja wangekwepo,kuna ndege za kimataifa unakata hata ticket miezi sita mbele,sometimes hazijai ni mwendo wa hivo hivo wachache,Imagine mtu anaumwa au tatizo kubwa unaona heri ugharamikie ndege kuliko bus halafu unakaa airport siku mbili,yaani bus inawahi kufika,ubaya hamna wa kumlalamikia na wa kujali wateja
 
Back
Top Bottom