Watumiaji wa usafiri wa ndege tunajuta kwanini Serikali imenunua ndege zake

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Kabla ya Mwaka 2015. Tanzania ilikuwa na mashirika ya ndege za ndani Makubwa manne.
1. Air Tanzania
2. Community air line
3. precision air.
4. Fast jet.

Community air line ilirudi kwa kishindo mwaka 2008. Ililet ushindani mkubwa katika soko la ndege. Mpaka sisi Manyonge ( makapuku) tukaweza kupanda ndege.

Nakumbuka kunakipindi Nauli ya Dar to Kilimanjaro ilifika 49,000Tsh. Huku nauli kutoka mwanza kwenda dar iliwa ni 69,000 pamoja na Tax. Na report zilionesha haya mashirika yalikuwa yakipata faida.

Kabla ya hapo, mashirika mengine yalikuwa yakicharge kati ya 200,000 hadi 350,000 mwanza to dar.

2011 kukawa na ujio wa shirika lingine jipya lijulikanalo kam FarstJet Tanzania. Hawa nao walikuja kwa kishindo kwa kushindana na Community air line.

Ushindani ukawa mkubwa mpaka mashirika mengine kama Air Tanzania na Precission air yakapunguza gharama za usafiri ili kucompete na Fastjet pamoja na community airline.

Haya mashirika yalifanyaa ATCL na precision air kupumulia mashine.

2016 Rais magufuli akaja na mkakati wa kufufua ATCL kwa kuanza kwa kuzinunulia Ndege. Baada ya hizi ndege kuja ATCL ikafufuka.

Mara pa tukasikia Fastjet na Community air line wamepotea kwa kasumba ambazo mpaka leo ni siri ya serikali na ayo mashirika.

Kibinafsi sisi wa hali ya chini Tuliokuwa tumezoea kupanda ndege za bei za fungulia dogi tunaumia sana awamu hii. Makampuni yaliyobaki sasa yamekuwa monopoly. Hakuna ushindani Tena. Ni kama bei zinapangwa na super monopoly ATCL.

Mfano, leo hii Ukitaka kufanya booking Mza to Dsm kwa kesho, cheapest flight ni USD 109 ambayo ni Air Tanzania. Huku Precission wakicharge USD 118. Na hii ni kwenda tu.

Screenshot_20200609-095111_Chrome.jpg

Hivi hizi ndege zilizonunuliwa Awamu hii ni kweli zimekuja kumsaidia Mtanzania myonge au ndyo zimekuja kumyonga zaidi?

Pia, hizi bei kubwa za Nauli za ndege ni mwiba katika secta ya utalii nchini.

Serikali itueleze Manufaa/ faida ya Manunuzi ya ndege mpya za ATCL kwa watanzania Wanyonge.
 
naunga mkono hoja..., tangu elfu 2017 nimepanda ndege mara tatu tu mpaka leo tena pale nilipokuwa na ulazima wa kufanya hivo, Bei zimepanda sana zamani ilikuwa chini na ushindani wa mashirika ulileta unafuu kwa bei.

sasa acha nikomae na basi, labda nikatiwe tiketi ya ndege na ofisi ndio nitapanda
 
Siku zote biashara ikiwa haina ushindani hua inakua maumivu tu kwa watumiaji , hapa naona Kama serekali yetu inafeli.

Mfano mwingine ni Tanesco hakuna ushindani mambo hovyo hovyo umeme bei juu .

Pia kukiwa hakuna ushindani na huduma hua zinaelekea kua Mbovu Mbovu tu.
 
Hakuna mantiki yoyote ya serikali kufanya biashara itengeneze sera rafiki za kuanzia kodi na Mazingira ili Private investors ndo wafanye Business ama sivo watoe monopoly na waruhusu competition.

Tungekuwa na ttcl tu huenda hata humu jamvini tusingekuwepo muda huu mana data zingekuwa juu
 
Acha kuzungumzia siasa. Usafiri wa ndege baada ya kuja ATC umesaidia sana kwenye ushindani na kupunguza nauli.

Mfano huko nyuma Dar-Bukoba[one way] nauli ilikuwa Tshs 485,000 hivi sasa nauli ni Tshs 283,000. Hata hivyo siyo lazima wote tupande hizo ndege kwani hata usafiri wa barabara umeboreka na kuna mabasi mazuri ambayo yanahudumia nchi nzima.
" Kupanga ni kuchagua"
 
Wewe inawezekana hata ndege hujawai kupanda.
 
Acha kuzungumzia siasa. Usafiri wa ndege baada ya kuja ATC umesaidia sana kwenye ushindani na kupunguza nauli.
Mfano huko nyuma Dar-Bukoba[one way] nauli ilikuwa Tshs 485,000 hivi sasa nauli ni Tshs 283,000. Hata hivyo siyo lazima wote tupande hizo ndege kwani hata usafiri wa barabara umeboreka na kuna mabasi mazuri ambayo yanahudumia nchi nzima.
" Kupanga ni kuchagua"
Fikiria jinsi gani wanao watakavyokudharau wakijua aliyeandika huu utoporo ni baba/mama yao.
 
Siku zote biashara ikiwa haina ushindani hua inakua maumivu tu kwa watumiaji , hapa naona Kama serekali yetu inafeli.
Mfano mwingine ni Tanesco hakuna ushindani mambo hovyo hovyo umeme bei juu .
Pia kukiwa hakuna ushindani na huduma hua zinaelekea kua Mbovu Mbovu tu.
Unajua gharama ya kuzalisha unit moja ya umeme?. Bei juu ikilinganishwa na bei ya wapi Tunaomba majibu tafadhali
 
Unajua mwaka 2011 unit ya umeme ilikua chini tsh 100 , sasa hivi ni 240+ , kipi kimebadilika mpaka unit iongeze bei namna hiyo , nijuze
Kwanza kabisa kimebadilika thamani ya dola...wanaowauzia Umeme Tanesco e.g Symbion,Songas na wenzao wanawauzia unit kwa dola...now go and do the math 2011 dola ilikua ngapi na ss ipo ngapi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kuzungumzia siasa. Usafiri wa ndege baada ya kuja ATC umesaidia sana kwenye ushindani na kupunguza nauli.
Mfano huko nyuma Dar-Bukoba[one way] nauli ilikuwa Tshs 485,000 hivi sasa nauli ni Tshs 283,000. Hata hivyo siyo lazima wote tupande hizo ndege kwani hata usafiri wa barabara umeboreka na kuna mabasi mazuri ambayo yanahudumia nchi nzima.
" Kupanga ni kuchagua"
Izo bei unazosema wewe hata ATCL ilikuwa ikilipisha ivyo. Lakini sio kati ya 2008 had 2014 julipokuwa na ushindani mkubwa hapa nchini.
 
Back
Top Bottom