Hivi ongezeko la mshahara linalofanywa kisiasa kwa kupunguzwa kodi kwa asimilia 01 lina matokeo gani?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Hii imeshindwa kueleweka kwa wengi.

Je, ina maana kuwa ile kodi aliyokuwa analipa mfanyakazi lets say ni shilingi laki moja (100,000) kwa sasa inapungua kwa kiasi cha asilimia 1 ina maana analipa shilingi elfu tisini (90,000)? - Kwa maana hiyo kwenye mshahara wake anaongezewa shilingi elfu kumi (10,000) hiyo iliyopunguzwa kwenye kodi?

Hebu wanaojua mahesabu ya kodi mtufundishe hapa ili tujue kama ni siasa tu au kuna uhalisia wa punguzo hilo?
 
Hii nchi tangu Magufuli aingie madarakani imekuwa yenye nuksi na mikosi.

Kipi Bora?

Kuongeza maslahi ya watumishi ili productivity iongezeke au kumwambia mtumishi aongeze uzalishaji ili aongezewe maslahi?
 
Hata hiyo haikufafanuliwa vema!

Ufafanuzi upo ni vile tuu watanzania hatusomagi

Halafu tunaishiaga kulalamika

Screenshot_20210503-132959.jpg
 
M
Ufafanuzi upo ni vile tuu watanzania hatusomagi

Halafu tunaishiaga kulalamika

View attachment 1772020
Mama D safi sana. Unachotakiwa kufanya sasa ni kufafanua hicho ulicholeta. Kwanza hapo kuna lugha ya Kiingereza mabayo hata mimi ninaona nyota nyota tu. Mie nikuombe ufafanue mf. hiyo Tsh 22,500/- au 70,500/- na 202,500/- je ndiyo nyongeza au?
 
Mshahara wa kuanzia 270,000 hadi Tsh. 520,000/= 9% - 1% = 8%
Mshahara wa 520,001 hadi Tsh. 760,000/= 20%
Mshahara wa 760,001 hadi Tsh. 1,000,000/= 25%
Mshahara wa 1,000,001 Tsh. / na zaidi = 30%
 
Mshahara wa kuanzia 270,000 hadi Tsh. 520,000/= 9%
Mshahara wa 520,001 hadi Tsh. 760,000/= 20%
Mshahara wa 760,001 hadi Tsh. 1,000,000/= 25%
Mshahara wa 1,000,001 Tsh. / na zaidi = 30%
Ndo nini mama maana bado sijaelewa nisaidie kufafanua zaidi
 
Hii imeshindwa kueleweka kwa wengi.

Je, ina maana kuwa ile kodi aliyokuwa analipa mfanyakazi lets say ni shilingi laki moja (100,000) kwa sasa inapungua kwa kiasi cha asilimia 1 ina maana analipa shilingi elfu tisini (90,000)? - Kwa maana hiyo kwenye mshahara wake anaongezewa shilingi elfu kumi (10,000) hiyo iliyopunguzwa kwenye kodi?

Hebu wanaojua mahesabu ya kodi mtufundishe hapa ili tujue kama ni siasa tu au kuna uhalisia wa punguzo hilo?
Haizidi elfu 3 mkuu
 
hesabu ulipata ngapi?

Mkuu

Wanakuondoshea hapo kwenye sahani ya kupeleka nyumbani ili ukenue meno ila punguzo hilo linaenda kufichwa mahala pengine ambapo unchungu wake ni mara ishirini zaidi bila kujua.

Usicheze na wanasiasa wanachezea sana maisha ya watu bila kujali chochote na ndio chanzo cha uharifu wa aina zote ambazo unazifahamu.
 
Nilipata F Mkuu! A level lakini!
Ndugu iko hivi, kwanza lazima ujue hilo punguzo la asilimia moja, Linawahusu wale tu wenye vipato vya chini yaani utahusika hapo kama unapokea mshahara wa 270,000-520,000.
Sasa twende vizuri hilo kundi hapo juu walikuwa wanakatwa kodi asilimia 9 ya mshahara wanaopokea.
Jana mama samia kasema atawapunguzia asilimia moja, kwenye hiyo asilimia 9 ili ibaki asilimia 8.

Sasa tuchukulie mfano mtu aliekuwa analipwa mshahara wa 300,000 kabla mama hajawapunguzia hiyo asilimia moja
300,000×9%=27,000 huyu mtu alikuwa analipa elfu ishirini na Saba.
Baada ya punguzo la asilimia 1 ikabaki asilimia 8
300,000×8%=24000.
Sasa huyu mtu mwisho wa mwezi badala ya kukatwa 27,000 atakuwa akikatwa 24000 ..so 27000-24000=3000 atapata unafuu wa 3000 kwa mwezi ya kunywa maziwa
 
Mimi nikienda Atm!! Nitachek salio lipo kias gan....Mshahala ukitoka....

Siumiz kichwa ...nitajua tu mzigo ulioongezeka:
 
Ndugu iko hivi, kwanza lazima ujue hilo punguzo la asilimia moja, Linawahusu wale tu wenye vipato vya chini yaani utahusika hapo kama unapokea mshahara wa 270,000-520,000.
Sasa twende vizuri hilo kundi hapo juu walikuwa wanakatwa kodi asilimia 9 ya mshahara wanaopokea.
Jana mama samia kasema atawapunguzia asilimia moja, kwenye hiyo asilimia 9 ili ibaki asilimia 8.

Sasa tuchukulie mfano mtu aliekuwa analipwa mshahara wa 300,000 kabla mama hajawapunguzia hiyo asilimia moja
300,000×9%=27,000 huyu mtu alikuwa analipa elfu ishirini na Saba.
Baada ya punguzo la asilimia 1 ikabaki asilimia 8
300,000×8%=24000.
Sasa huyu mtu mwisho wa mwezi badala ya kukatwa 27,000 atakuwa akikatwa 24000 ..so 27000-24000=3000 atapata unafuu wa 3000 kwa mwezi ya kunywa maziwa
🤣🤣🤣🤣🤣 HiiIiii,siamini..hakuna mwenye utaalamu humu jf!hesabu inatuzingua,vip jamani Annual increments itakuepo?!mama hakuzungumzia hilo!
 
Hakuna faida yoyote kwa mfanyakaz coz basic inabaki vilevile na hakuna nchi kukua kiuchumi kama Samia ataogopa kutake risk kama mtangulizi wake.
 
Back
Top Bottom