Ningeshauri punguzo la kodi ili vitu vishuke bei, kuliko kuongeza mshahara

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
NINGESHAURI PUNGUZO LA KODI ILI VITU VISHUKE BEI,KULIKO KUONGEZA MSHAHARA.

Leo 13:15hrs 15/05/2023

Je ni kweli gharama za maisha za leo hii ili mtumishi amudu maisha inabidi kima cha chini kiwe millioni moja!!? Mimi nadhani ingekuwa vyema kama tungeongeza tija katika uzalishaji ili pesa ipande thamani na mshahara ule ule hata ukiwa 80,000 uweze kutosha,vinginevyo tunaweza kusababisha mfumuko wa bei mkubwa zaidi kama ule wa mwaka 1994,ni kweli gharama za maisha hazipungui kwa kupunguza uwezo wa raia wako kufanya manunuzi lakini thamani ya hela inaongezeka pale demand ya pesa inapokuwa kubwa,

Naomba ifahamike ya kwamba thamani ya pesa ni purchasing power yaani uwezo wa pesa hiyo kununua bidhaa na huduma,huwezi kubeba hela kwenye torori ukanunue mkate halafu useme pesa hiyo ina thamani,kwa hili la mfumuko wa bei ulivyo hivi sasa hili ongezeko kubwa lisipoambatana na kutunza thamani ya pesa kwa kudhibiti mfumuko wa bei basi hzi jitihadi yaweza kuwa kama kumwaga mchele kwenye kuku wengi,matokeo kidogo kwenye uchumi wa mfanyakazi Mmoja mmoja,maendeleo hayana chama,naomba kuwasilisha,

Wapo wafanyabiashara wahuni watatumia kupanda kwa bei kupandisha bidhaa zao,sio mafuta tu,kila kitu kitapanda bei,maji,soda na bia vilikuwa vinashuka bei sasa vimeanza kupanda,Bia tegemeo la wengi kujifariji nazo zitapanda,baadhi ya bidhaa hazijawahi kupanda kwa muda mrefu mfano Michele,Unga, Mafuta ya kupikia na bidhaa zote za mahitaji ya kawaida vyote vimepanda bei,huku kuupiga mwingi kielekea golini kwetu kunawasaidia nini watanzania wa kawaida zaidi ya kuwaminya na kuwafanya watamani kuenda Rwanda kwenye maendeleo ya watu wa kawaida!

-Chumi mbili tofauti katika awamu ya chama kimoja!

-Awamu ya tano Serikali kuwa na pesa na kufanya maendeleo "Contractionary economic policy" kuna faida na hasara zake.

-Awamu ya sita,Wananchi kuwa na pesa "Expansionary economic policy" kuna faida na hasara zake,ikiwemo watu kuwa na pesa kuliko Serikali,mtu anaweza kuikopesha Serikali.

Ni jambo la kuamua,tofauti ya Awamu ya tano na Awamu ya sita,Mama ameamua kuwapa pesa wananchi na JPM yeye aliamua Serikali ndio iwe na pesa,sasa hapo kila chumi ina faida na hasara,lakini mwisho wa siku Wananchi wote kwa ujumla wananufaika vipi!? Wananchi wanapaswa kunufaika na Serikali pia kufanya mambo ya maendeleo hilo lazima liwe balanced.

Sioni sababu ya kitaalamu ya kuonheza mishahara kwa wafanyakazi wa umma,Serikali unatakiwa kujikita kupandisha thamani ya shilingi ya Tanzania ili pesa inayo patikana kwa wananchi kwa ujumla wao iweze kukidhi mahitaji yao ya kila siku,kupambana na mufumko wa bei ya bidhaa na huduma mbalimbali,upo ushahidi kila mshahara unapo panda bidhaa hupanda bei,hivyo inawaumiza wale wasio na mshahara wa mwezi Bali ni wahangaikaji wa vibarua visivyo rasmi,

Ongezeko lilipaswa liendane na kushusha inflation maana mwisho wa siku unaweza kuongezeka elfu 80,000/= kwenye mshahara wako ambayo haitaleta impact yeyote kama maisha yataendelea kupanda! lakini kupunguza kodi kungeweza kuleta ahueni kwa kila mtu maana bei ya vitu ingeshuka sababu bidhaa imepunguziwa kodi,Waajiriwa 1,000,000 v/s watanzania 59mil waliopo katika mfumo usio rasmi,na ambao kilio chao hawafahamu pa kukipeleka,Hayati Rais Magufuli aliangalia sana hapa!

Hata hivyo serikali bado kuna kazi kubwa ya kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa jumuishi kwani serikali imeajiri wafanyakazi ambao hawazidi laki 8;
Sekta binafsi (rasmiimeajiri zaidi ya mara 4,sekta isiyo rasmi ina nyomi ila mchango wake kwenye kukuza uchumi wa nchi iko very fragile na uncordinated na sekta ya fedha ili kukuza uzalishaji wenye tija.

Kilimo/Ufugaji/Uvuvi iko haja ikawa highly organized ili iwe na access na sekta ya fedha ili kinachozalishwa kiwe na uhakika wa soko na kuwafanya wakulima wa-benkike, wachangia NSSF na wamudu kulipia bima ya afya;
Kinachozalishwa kwenye kilimo kikiweza kuchakatwa na viwandani vya ndani kutaongeza ajira na ku-cut down imports ya consumables,ni aibu tuna import 90% ya ngano.
Ni aibu tuna import surgical cotton, bandage, gauze, mashuka ya hospitali na tunalima pamba na tunashindwa kuzalisha products za pamba
Ni aibu tuna import 80% ya mafuta ya kula...the list goes on

Mguso huu utaipa serikali tax base kubwa based on purchasing power ya watu na makampuni ya ndani na hawa walio sekta isiyo rasmi na kilimo hasa cha kibiashara wataipa serikali chanzo kingine cha uhakika kukusanya kuhudumia Watanzania ikiwamo mishahara na maslahi mengine ya watumishi wa umma.

Sekta binafsi ili uongezewe mshahara inabidi uongezewe kazi kwa maana ya kupanda cheo ila serikalini mtu anaongezewa mshahara bila kuongezewa kazi siku ya mei mosi,Sekta binafsi output yako itafanya uongezewe mshahara au ubaki kama ulivyo, huko serikalini wao wanaongezwa tu, vigezo nadhani ni "kupanda kwa gharama za maisha". No wonder watu wengi wanapigania ajira za serikali ili "wakapumzike".

-Kwa nini tulipaswa kupunguza PAYE kuliko kuongeza mshahara kama alivyofanya Hayati Rais Magufuli.

Baada ya kuongeza mishahara kuna kazi endelevu ya inapaswa kufanya ya kudhibiti mifumuko ya bei itokanayo na kupandisha mshahara na athari za vita vya Urusi na Ukraine,Awamu ya tano ya CCM chini ya Rais John Pombe Magufuli haikupandisha mishahara bali ilishusha kodi kwa wafanyakazi PAYE hii ikasababisha uimara katika kudhibiti mifumko ya bei,hivyo basi wafanyakazi hawakuwa na hali mbaya sana mfano nauli ya daladala ilikuwa ni 400,bajaji 500 kwa muda wote nauli za mabasi zilkuwa zile zile lakini leo nauli ya daladala ni sh 550 na bajaji ni sh 700,hivyo Serikali yetu ya awamu ya sita ina kazi ya kuwasaidia Wafanyakazi kwa kudhibiti mifumko ya bei,itakuwa hakuna faida ya ongezeko la mishahara iwapo kutakuwa ongezeko maradufu la bei kwa bidhaa mbalimbali badala ya ongezeko la mishahara kuwa neema linakuwa kichocheo cha mfumuko zaidi ya bei ya bidhaa mbalimbali,

Rais wa Zanzibar kaongeza 15 % wakati Udhibiti bei za bidhaa ni mzuri na upo chini kwa kuanzia kuwasaidia wazanzibari,Rais wa SMZ amefanya juhudi kubwa sana za kupambana kudhibiti na kupunguza makali ya mifumko ya bei ya bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari 1900 petrol 2650 nk nk nk pia nauli za usafiri wa umma hazijapanda kwa ufupi Serikali ya Zanzibar imejielekeza kupambana kudhibiti na kupunguza makali ya mfumko wa bei kisha wanapandisha mishahara huku Tanzania bara (Tanganyika) mbali mfumko wa bei iliyopo kwa kila bidhaa bila Jitihada za Makusudi zaidi ya kupunguza sh 29 kwenye mafuta ongezeko la 23.3 % linaenda kuwa kichocheo kipya cha ongezeko la mfumuko wa bei ya bidhaa mbalimbali nchi nzima ya Tanzania bara,sasa Serikali yetu inapaswa kujielekeza kwenda kukidhibiti hili kwa manufaa ya CCM na Serikali yake.

Nimalizie kwa kusema Serikali ya CCM ya Awamu ya tano haikupandisha mishahara kwa miaka 6 Ila ilipunguza kodi za Wafanyakazi wote wa Umma na sekta binafsi,hivyo kuonekana ahueni kwenye maisha ya Wananchi hao,Serikali ya CCM ya Awamu ya sita imepandisha mishahara baada ya mwaka mmoja tu,hongera kwa Serikali yetu ila naomba irejee awamu ya tano ilipunguza PAYE kwa kiwango kikubwa ambapo faida ilikuwa kwa watumishi wote wa umma na binafsi awamu ya tano ilihakikisha kuna umeme wa kutosha muda wote hivyo gharama za uendeshaji wa shughuli za kibiashara,kiuchumi na uzalishaji wa viwanda zilikuwa chini awamu ya tano ilidhibiti mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali kwa ufupi adui namba moja wa Mshahara na Kipato,ni mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali,hiyo ndio side effect ya kupandisha mshahara kote duniani,

Nimalizie kwa tafakuri jadidi,Ukiongeza mishahara unavutia ongezeko la gharama za maisha,hapa tulipo tayari gharama za maisha zipo juu sababu ya athari za vita ya Ukraine na Urusi bado tunaongeza mishahara mambo yanazidi kuwa magumu ilitupasa tuongeze marupurupu tu na sio mshahara na njia sahihi zaidi ilipaswa kuwa kupunguza kodi,Unapoongeza ni kwamba kuna faida katika biashara yako au mapato yako,sasa tumeongeza mishahara,Je kuna pato la ziada,hilo pato la ziada lipoo?? Au tunafanya siasa tu wakati hali hairuhusu,tusije kuanza kukopa kulipa mishahara,nionavyo shillingi yetu ipo vile vile kama kushake ni kidogo sana,kuna vitu viwili hapa tuvielewe balabala,

1.Cost-Push Inflation inasababishwa na kupanda kwa gharama za uzalishaji na hii inasababisha na athari ya kupanda kwa mafuta,

2.Demand-Pull Inflation inayosababishwa na kuongezeka kwa demand ya bidhaa,hii inasababishwa na athari za kuongezeka mshahara,maana mshahara ukiongezeka,mifuko inawasha utataka kila siku unywe bia na nyama choma,ununue crown uongeze na Mke wa pili,

-Lipo tatizo kwenye kununua bidhaa toka nje ya nchi "Much Imports" kuliko kuuza bidhaa nje ya nchi "Exports".

Ni muda mrefu umepita hatujawa tegemeo kuu la bidhaa fulani Specific Duniani (Parachichi,Zabibu,Mchele,Soya,Arizeti,Viazi) jambo ambalo lingefanya currency yetu kuwa na thamani na kwa kuwa tunategemea dola tukipandisha thamani shilingi kwa ku-Export basi dola ingeweza kubadilishwa kwa kiwango cha kawaida kwa kuwa Demand ya Shillingi yetu kama foreign Currency kwenye Trade ingekuwa kubwa kwa uhitaji wa vitu tunavyolima mfano Parachichi.

Niwaambie ukweli Watanganyika, Wazanzibari kwa neno moja Watanzania wenzangu! Taifa linalozalisha vyema halina Inflation kubwa ya kustusha mpaka katika very special circumstances mfano uwepo wa vita vya sisi wenyewe kwa wenyewe,tuchukulie mfano Urusi inazalisha gesi na mafuta dunia inawategemea,inaendesha vita kuipiga Ukraine na maisha yao yanakwenda kama kawaida.

Nifunge mjadala kwa kusema ningefurahishwa kwa kutoongezewa mshahara wafanyakazi zaidi ya kupunguziwa kodi, nikirejea ushauri nilioutoa hapo juu,lakini watu wameongezewa mshahara,ila tujiulize swali lifuatalo;- Je, ni kweli uzalishaji wa bidhaa unakwenda sawa na uhitaji wa bidhaa uliopo? Maana mshahara ukiongezeka mahitaji ya mtu nayo yanaongezeka,asiyekunywa bia nae atataka anywe bia na asiye na gari na atanunua gari, Tukumbuke ya kwamba increase in income lead to increase in demand and it may lead to increase in price if suppy remain constant,kama tutaongeza mshahara basi bei itaoongezeka na tutaukaribisha mfumuko wa bei zaidi na zaidi,ninachoshauri marupurupu yaongezeke kwa Wafanyakazi ila sisemi kwamba watu wajilipe safari za kwenda Semina Uingereza,kabla ya kwenda Uingereza wanaenda kufanya shoping Ufaransa (outfit) baada ya shopping wanaenda kucheki afya Ujerumani wakitoka Ujerumani wanaenda Ontario Canada kufanya small gathering "assembly" kisha wote wanapanda ndege moja kuelekea Uingereza,tusifanye hivyo,tutakuwa tumerudi enzi zile za kupishana angani kama kumbikumbi.

Mwisho kabisa niipongeze Serikali kwa kupandisha kima cha chini ambapo sasa watakwenda kuchangia kodi kwa Taifa letu la Tanzania bara,tunatafuta kodi ili kuendesha Serikali,sasa kuna mishahara ya kima cha chini haitozwi kodi,salary ambazo zipo chini ya tax band flani hazitozwi kodi,mishahara hiyo haitozwi kodi,sasa increment ikifanyika tu zikavuka hiyo band zinalimwa kodi na hasa hilo ndio lengo kubwa la government,kwa hiyo tunapoongeza mshahara kima cha chini tunawasogeza katika eneo la kuanza kukatwa kodi,Mwananchi mmoja ananiambia bora kupunguzwa kodi kwenye mishahara kama tuna nia ya dhati kwa mfanyakazi na kama tuna nia ya dhayi ya kupunguza mfumuko wa bei Tanzania bara,Tukumbuke tu kiasi taslimu kichoongezeka ni Tril 1.5 tu katika bajeti ya mwaka huu na ndicho kitaenda kuaffect hayo maongezeko yooooote kwa mwaka mzima.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Ungejua mishahara ya Tanzania bado IPO chini sana usingeandika haya.

Serikali iongeze mishahara, kima cha chini kiwe 1010000 (milioni moja na elfu kumi), Pia idhibiti mfumuko wa bei kama Mkapa alivyokuwa anafanya.
 
Naunga mkono hoja. Shida ya Wafanyakazi sio ongezeko la mshahara Bali Ni purchasing power.
 
Upumbavu huu.hujui mishahara isipopanda na pensheni inakua ndogo??ulitaka mishahara isipande milele??hivi vi uchumi Vya definition msituletee huku,pelekeni kwa wake zenu
 
Yeye kuongeza mishahara hakuzuii kulitazama ombi lako. Acheni roho mbaya, mishahara bado ni midogo lakini bado mnaikingia kifua ili wote muwin muendelee kuwakopesha wafanyakazi na kuwasema sana mitaani.
 
Uchumiwa vyeti ni mnaya sana . Unaweza kukuta mleta mada ana digree kutoka jalalani kabisa. Anashindwa kuleta facts anakuja na assumptions. Sasa huko ulaya kwenye mishahara ya juu na uchumi wao umekua walifanyaje. Module gani aliyosoma huko chuo inasema moja ya njia ya kuondoa umaskini ni kumlipa mtumishi pesa kiduchu.

Mleta mada kajaribu kuwasoma wachumi wenzako kama kina Beno Ndulu wamesajest njia za nchiza Afrika kujiondoa katika umasikini ni kama kufanya yafuatayo
1 Kuwa na nishati ya uhakika na kwa bei nafuu
2 Ujenzi wa miundombinu kama barabara na reli
3 ujenzi wa viwanda nk
Hayo unayosema wewe ni mapya ndio kwanza tunaskia kwako. Petrol iliuzwa 1500 kipindi cha korona mbona nchi haikutajirika au kustawi kiuchumi kama tatizo pekee ni mfumuko wa bei
 
Watu wanaojisikia vibaya watumishi wakiongezwa mshahara siyo kwamba wanakosea tu ila wanakosea sana kwani malipo bora yataimarisha kiwango cha utendaji kazi cha hao watumishi wa umma hata circulation ya hiyo hela itamfikia mtu yeyote labda tu yule ambaye hajishughulishi kwani purchasing power ya watumishi itaongezeka kila kitakachozalishwa na mtu wa kawaida au kuuzwa hakitakosa soko.Muacheni mama atekeleze hiyo sera ya kupeleka fedha kwa watu tofauti na ile ya kubana matumizi ambayo ilisababisha watumishi kuishi maisha ya ovyo
 
Back
Top Bottom