Hivi NMB Jumatatu itakuwa lini

Hivi NMB Jumatatu itakuwa lini

Rutechula

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2024
Posts
822
Reaction score
1,067
Wana JF nani anajua Jumatatu ya hawa jamaa wa NMB itakuwa lini?
Kwenye calender ya Gregoly, waliyotwambia ndiyo leo kakini mambo ndiyo bado magumu kabisa hata hizo sijui POS nazo hakuna kitu asubuhi hata ATM zao zililinuna kabisa duuuhhh.
 
bank inakazana na kuleta techonology mpya huku wao bado hawajafanyia kazi techonlody za zamani, huwezi ukaikalisha huduma ya fedha bila utatuzi kwa masaa mengi hivi tena huduma ya kifedha na mapesa ya watu yapo kwenye bank yako,wanahitaji kubadilika maana ina cost wateja
 
Nimetizama salio langu naona kuna pungufu la pesa, hili nazaa nao.
 
Online banking bado haifanyi kazi. Kwa walioko nje ya Tanzania tuendelee kulia tu.
 
Wamerud hewani
Bado maana app nayo inasuasua sana muda huu imenigomea bila sababu kabisa na ile nyingine ya kupitia simu ndiyo hamna kitu kabisa.
NMB kwa sasa hivi hawana tofauti na wababaishaji wengine wa mtaani.
 
Kuna kitu kinakuwa implemeted, kulikuwa na malalamiko kuwa pesa za wateja zinapotea baada ya kufanya hiyo upgrade. Nadhani mchezo hii inaenda kuendelea huko NMB.
 
Kuna kitu kinakuwa implemeted, kulikuwa na malalamiko kuwa pesa za wateja zinapotea baada ya kufanya hiyo upgrade. Nadhani mchezo hii inaenda kuendelea huko NMB.
Duuuhhh uwenda tunaweza pigwa kimya kimya? duuuhhh
 
Poleni sana, mlicheka sasa ni zamu yenu afadhali benki ya maendeleo vijijini walikuwa wanaweza kutoa pesa kidigitali
 
Walitangaza Mapema kabisa, Hamkujifunza CRDB?

Ukishasikia benk kuna mabadiriko ya mfumo au maboresho, toa kiasi cha pesa cha matumizi kisha print Bank statement
 
Tumieni Binance benki za kibongo si salama tena
 
Back
Top Bottom