Zaidi ya asilimia 80 ya wananchi hasa mijini wanaishi nyumba za kupanga. Kwa mji kama DSM ambapo bado kuna uhitaji mkubwa wa makazi bora, watu hutumia zaidi ya robo ya vipato vyao kulipia kodi za nyumba kila mwezi, lakini cha kushangaza, serikali haioni unyeti wa kuingilia na kusimammia sehemu hii. Hapa nina hakika serikali ingeweza kukusanya kodi ya kutosha kabisa kutoka kwa wenye nyumba iwapo wangeweka utaratibu mzuri wa usimamizi.
Tunaelekea kumaliza miaka 5 ya awamu ya kwanza ya JPM, lakini waziri Lukuvi na wizara yake wamekuwa wakiimba tu mapambio juu ya kanuni za upangishaji nyumba. Ugumu uko wapi kuleta sheria na kanuni zake ili kuwaondolea kero wananchi wanaopanga nyumba? Watu wanalazimishwa kulipa kodi mpaka ya mwaka mzima kisa tu hakuna kanuni husika.
Tutengeneze sheria, kama mtu akiamua kupangisha nyumba yake basi akubali kufuata kanuni za serikali, moja wapo ni kutolazimisha mtu kulipa kodi ya miezi 6/mwaka.
Kuna issue ya madalali wa nyumba, ambao kwanza wengi wao huku uswahilini hawajasajiliwa, maana yake wanafanya kazi bila utaratibu maalum. Matokeo yake wamejitengenezea utaratibu usio haki wala halali wa kudai kodi ya mwezi mmoja kama mtu ataamua kupanga nyumba husika. Wizara ya Ardhi kama wangekuwa wanatimiza wajibu wao, leo hii tungekuwa na muongozo wa kuwasajili na kutengeneza viwango vya malipo halali kwao pamoja na kukusanya kodi kutoka kwenye vipato vyao.
Haiwezekani mtu apewe kodi ya mwezi mmoja ambayo hata haikatwi kodi mahali popote na serikali kisa tu alisimama katikati ya mwenye nyumba na mpangaji.
Waziri Lukuvi, hizi ni petty issues kwako, ambazo ukiamua tu ndani ya muda mchache solution inapatikana na impact inakuwa kubwa.