Hivi ni kweli ukikopa benki ukashindwa kurudisha pesa zao hakuna Benki Tanzania itakayokukopesha tena?

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,539
Habari JF?

Naomba tufahamishane kuhusu hili suala?

Mfano nimekopa Sh laki 5 pale NMB branch Ya Igoma, baadae nikashindwa kurejesha mkopo wao wakaja wakabeba dhamana.

Je, Taarifa zangu za kushindwa kurejesha mkopo zitapelekwa kwenye system za benki nyingine za Biashara Tanzania ili nikienda kukopa huko waone kwamba niliwahi kopa kwingine na nikashindwa kulipa?

Je, sitakopesheka tena maisha yote hata kama nina Dhamana nyingine?
 
Hakuna hicho kitu.
Kila benki humkopesha mtu baada ya kuridhika na Amana zako au udhamini wako. Ikiwa umeshindwa kuliko taratibu zinafuata ili kurecover ili wasipate hasara.
 
Weeee kopa tu..... kisha sepa zako
Jana niliongea kidogo na Financial Analyst wa NMB kwa uchache sana akanieleza kuhusu Mfumo wao unaoitwa Credit Reference Bureau (CRB)

Akaniambia wale loan failures wote huwa wanajazwa humo hata kama umechelewesha kwa siku 1.

Sasa nataka kusikia kwa waliowahi kukopa kwenye hizi taasisi kubwa kifedha, Je washawahi kukutana na hii kitu?
 
Habari Jf?

naomba tufahamishane kuhusu hili suala?

mfano nimekopa Sh laki 5 pale NMB branch Ya Igoma, baadae nikashindwa kurejesha mkopo wao wakaja wakabeba dhamana.

Je, Taarifa zangu za kushindwa kurejesha mkopo zitapelekwa kwenye system za benki nyingine za Biashara Tanzania ili nikienda kukopa huko waone kwamba niliwahi kopa kwingine na nikashindwa kulipa?

Je, sitakopesheka tena maisha yote hata kama nina Dhamana nyingine?
Embu jaribu tuone itakuwaje
 
Kila bank inajitegemea. Itategemea makato yatafanyikia wapi, kama kwenye mshahara ambao utakatwa moja kwa moja hakuna shida; au dhamana utakayowapatia na wao kujiridhisha pale ambapo utashindwa kulipa wanaweza kuitaifisha.
 
Shukran sana. Umeeleweka sana mkuu
 
Habari Jf?

naomba tufahamishane kuhusu hili suala?

mfano nimekopa Sh laki 5 pale NMB branch Ya Igoma, baadae nikashindwa kurejesha mkopo wao wakaja wakabeba dhamana.

Je, Taarifa zangu za kushindwa kurejesha mkopo zitapelekwa kwenye system za benki nyingine za Biashara Tanzania ili nikienda kukopa huko waone kwamba niliwahi kopa kwingine na nikashindwa kulipa?

Je, sitakopesheka tena maisha yote hata kama nina Dhamana nyingine?
Siyo kweli.
 
Kuna kitu kinaitwa CRB(Credit reference bureau)hapo ukichelewa kulipa mkopo wako wanakueka hapo hata kama ukimaliza kulipa utakua bado upo CRB kwa hio utatakiwa kuomba bank yako kukutoa kwenye CRB,Na kipindi chote ukiwa CRB Huwezi kupoke mkopo wowote kutoka kwenye taasisi yoyote.

Huku kwetu Rwanda ndio hivyo sijui huko TZ Lakini najua na nyinyi mnaelekea huko.

Asante
 
CRB(credit reference Bureau) wadau miaka ya nyuma waliipigia kelele ikanzishwa...hapa Kati kumekuwa na ukimya kuhusu utendaji wake...it's work or not? Na Kama iko active inafanya kazi..?...ukomo wa mtu kuhesabika ni defaulter anadumu muda gani kwenye system Yao? Wenye majibu please

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru kwa maswali yako na mimi nina maswali kama haya haya
 
Back
Top Bottom