WINGER_TEREZA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 242
- 450
Leo katika zoezi la kuthibitishwa kwa jina la Makamu wa Raisi Bungeni Jijini Dodoma Spika wa Bunge, Job Ndugai, alipata wakati mgumu wa kati amruhusu kwanza aliyekuwa Mbunge wa Buhigwe, Dkt. Mpango (VP now), ahutubie kwanza kabla ya matokea ya kura za kuthibitishwa kuwa makamu wa Rais hayajatangazwa au baada ya kutangazwa. Spika Ndugai alionekana anatafuta na kunukuu vifungu kadhaa vya katiba ili asitende hiko anachoita uvujifu wa katiba kwa kutaka kung'amuwa ni namna gani ataepuka hilo.
Ila cha ajabu kunamatukio mengi ambayo yamebalikiwa chini ya Spika Ndugai yanayohusishwa na uvunjifu wa katiba wa moja kwa moja lakini Spika hajachukua hatua yoyoye ya kuyazuia zaidi yake amebaliki kwa kuyakingia kifua kwa nguvu zote.
Mfano Spika amewakingia kifua wale Wabunge 19 wanaoitwa wabunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CHADEMa ili hali chama kilishawavuta uanachama na kila mtu anajua hilo. Hii ni kinyume na katiba ambayo leo ameonekana kuangalia namna ya kutafsiri ili "asiivunje". Pia alinukuliwa akisema yeye ndiye Spika wasiogope kwani hakuna mtu wa kuwatisha!
Mfano mwingine wa uvunjifu wa katiba "uliosimamiwa" na Spika Ndugai, rejea saga la CUF enzi zile za CUF ya Maalim (RIP) na CUF ya Lipumba kuna Wabunge wa upande fulani walivuliwa uanachama hivyo kukosa sifa za kuwa Wabunge kwa mujibu wa Ibara (nimeisahau hiyo ibara) ya katiba inayosema Mbunge atakoma kuwa Mbunge tu pale atakapo koma kuwa mwanachama wa chama chake cha siasa "kilicho mzamini".
Kwa mukutadha huo ninapata wakati mgumu kumuelewa Spika ni Katiba gani aliyotaka asiivunje leo ili hali kasaivunja hiyo katiba mara kadhaa huo nyuma tena kwa wazi wazi?.
Leo sijamuelewa kabisa Mh. Spika.