Hivi ni kweli sisi waafrika hatukuwa na chetu vyote ni vya kigeni kuanzia dini, ludha, chakula, elimu,siasa na imani?

Subiri somo la historia ya Tanzania lianze kufundishwa June,2021 ndipo utaelewa kwa upana.
 
Hivi ni kweli sisi waafrika hatukuwa na chetu vyote ni vya kigeni kuanzia dini, ludha, chakula, elimu,siasa, imani. Yaani vyote vilikuwa vya kishenzi.

Mtoto wa Mchungaji sielewi.
Mimi nadhani meeting of cultures kunaleta kitu kipya. Mfano, hata Uingereza, Ufaransa, Amerika, Canada etc sijui kama kuna kitu proper ambacho unaweza kusema 'hiki ni cha hawa' na 'kile ni cha hao'. Baba na mama wameoana makabila tofauti. Sisi watoto tuliozaliwa tumejikuta tuko katikati. Baba alikuwa haongei lugha yake, ila ya mama. Na familia nzima tunaongeza lugha ya mama, siyo kwa sababu tunadharau lugha ya baba, ila kwa sababu hakuna anayeongea lugha ya baba na sehemu tunakoishi lugha inayotumika ni pamoja na lugha ya mama. Pia kwa upande wa mila. Tumejikuta hatuna mila yoyote (matambiko). Siyo kwa sababu tunadharau mila ya baba au mama, ila kwa sababu tunaona hatufungwi na mila ya upande wa baba (ambayo hatuifahamu), wala ya upande wa mama ambayo tunaona siyo mila yetu. Kwa hiyo, watoto wetu wanakuwa na mila ya jumla - kuwa watu wema na kuwatendea wengine mema kama unavyopenda utendewe nao. Hii ndiyo imebaki mila yetu, ambayo naona fahari kuikiri. Hivi ndivyo naweza kusema hata kwa Waafrika. Hatuwezi kupata tena tulichokipata (kama hakipatikani tena). Katika mazingira hayo tuishi fully kile kilichobaki na kama hatuwezi, let's be good people na it's enough. Hata watu kutoka Ulaya na Amerika kama wakirudi kwao wanaonekana tofauti na wenzao (ambao hawajawahi kupata fursa ya kukutana na cultures nyingine). Nilichojifunza mimi darasani hasa kupitia anthropology (social and cultural) na kukutana na cultures za wengine kuna kitu kinachotokea kinachoitwa 'cross-fertilisation' - wewe unajifunza kitu kuhusu watu wengine na watu wengine wanajifunza kitu kuhusu wewe na hapo ndipo huzaliwa a new culture na ndipo tulipo leo Afrika. Ni useless usiku na mchana kulialia kwamba tuliuzwa watumwa, tukatawaliwa, tukaibiwa mali zetu na then tunaishia hapo tu. Cha kufanya ni kujifunza kwamba sisi tusiwe wakoloni in any form na ili tuwe mfano kwa wengine lazima maisha yetu yawavutie wengine - wakituona jinsi tunavyoishi, ongea, shirikiana, tenda etc. Hili ndilo jambo muhimu. Yaliyopita yatusaidie kuwa watu wapya na kusonga mbele (progression) na siyo kuchakaa na kurudi nyuma (retrogression).
 
Kwa asilimia kubwa hatuna chetu mpaka muda huu.

Wakoloni walikuja kwa nia mbaya sawa.
Ila bila shaka kama wasingekuja asilimia kubwa ya africa ingekuwa nyuma mara mbili ya sasa hivi.

Kama yale baadhi ya makabila yanayoishi maporini na kujenga vijumba vya nyansi na kuendeleza mila mbovu pia umasikini na ujinga uliopita viwango.
 
Endelea kuisoma historia ya utandawazi utaelewa mengi
 
Back
Top Bottom