Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,661
- 46,349
Kumekuwepo na matamanio ya watu wengi serikali kufanya udhibiti wa baadhi ya imani za kidini hasa za baadhi ya madhehebu ya Kikristo ambayo yamekuwa yakizuka kwa kasi miaka ya hivi karibuni.
Kwanza, lazima tufahamu uhuru wa kidini katika nchi hii upo katika katiba, kutaka kuuingiliwa uhuru huo kwa sababu ya kutozipenda baadhi ya imani au madhehebu ni kuhalalisha uvunjaji katiba.
Pili, Serikali haina uwezo wa kutambua dini ya kweli ni ipi, haina uwezo wa kujua nabii au mtume wa kweli ni yupi na pi aina uwezo wa kufahamu tafsiri sahihi ya maandiko yoyote. Kufanya uingiliaji wowote kwa manabii, mitume, walimu na imani zilizozuka kwa kasi itakuwa pasipo na vigezo vyovyote/"arbitrary".
Tatu, Serikali hapaswi kuingilia uhuru wa dini yoyote kwa namna yoyote ile, ni mfano/precedent/slippery slope mbaya sana kuelekea kukandamiza uhuru mwingine wa raia serikali inapokuwa na mkono mrefu katika masuala dini na imani.
Mwisho, Kinachotakiwa ni Serikali kuweka mazingira bora sana ya elimu kama Ulaya kuhakikisha raia wake wanapata elimu bora na wengi wanaweza kufanya tafakuri sahihi za logic kisha hao raia wataachana wenyewe tu na utapeli wa kidini au superstitions.