Ndo maana watu Wanachepuka, maana mtu mwishowe anachoka.
Hao watu wakichepuka hua wanachepuka na wanawake wa wapi? Si wanaenda kuchepuka na hao hao wanawake wa kibongo unao wasema wewe hapa?
Hata huyo Mwanamke wako wewe ukimuona hana mvuto,basi wapo watakao muona ana mvuto huko nje na watamtongozwa,
Kijana jifundishe kuijua saikolojia ya binadamu,
Binadamu hutamani kitu ambacho hana ila akisha kipata hukiona ni cha kawaida tu,na sio kwa wanawake tu,bali hata Magari,majumba au hela,ukisha zipata unaona ni kitu cha kawaida tu,
Trump ni tajiri ila akatamani kua kiongozi na akagombea urais wa US,ndio maana nakwambia kua binadamu hutamani kitu ambacho hana,
Ukienda Hotelini ukaagiza chakula kisha meza ya pili ya jirani yako,nae akiletewa chakula alicho agiza,utaona kama yeye kaagiza chakula kizuri zaidi yako,huyo ndio binadamu,hata uwe na Mwanamke mzuri wa aina gani,baada ya muda utamuona ni wa kawaida tu,
Hapo issue sio mwanamke wa kibongo bali ndio binadamu alivyo,
Hata wanawake nao hua wanachepuka pia,so hapo utasema wanaume pia wanaume wa kibongo nao hawana mvuto?