Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,159
Nimekuwa nikiwasikiliza wanasiasa wa Chama tawala cha CCM, katika majukwaa ya kisiasa na nilichokishuhudia ni viongozi hao kujigamba kuwa, vyama vya upinzani vya nchi hii vipo mahututi na vinasubiri kuzikwa tu, kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Rais ya kufanya maendeleo mbalimbali nchini, kama vile, ujenzi wa reli ya SGR, ujenzi wa Stiegler's Gorge na ununuzi wa nduge za dreamliners, ujenzi unaoendelea hapa nchimi wa barabara za lami na mengine mengi mazuri yanayofanywa na serikali hii ya awamu ya tano, na kuwa wapinzani hawana hoja za kuwaambia watanzania, kwa maana hiyo wanachosubiri ni vyama vyao kufa tu
Wamediriki baadhi yao kutamka kuwa wananchi watakaoendelea kuchagua wapinzani, akili zao siyo nzuri!
Hata hivyo maneno hayo ya majukwaani yana tofauti kubwa sana na vitendo vinavyofanywa na viongozi wa serikali kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Kama ni kweli serikali hii ingelikuwa inajiamini kiasi hicho cha kuwafanyia mazuri matupu wananchi wake, ni kwanini basi hawawaachi wananchi hao wakachambua mchele na pumba kwenye sanduku la kura??
Mbona figisu figisu zimekuwa nyingi mno katika zoezi zima la chaguzi za serikali ya mitaa zinazoendelea??
Hivi serikali hii ya awamu ya tano, imefikia kiwango hiki cha kufanya hila hizi ninazoweza kudiriki kuziita za kipuuzi kiasi hiki??
Tunashuhudia upendeleo wa wazi kabisa wa shughuli za kisiasa hapa nchini, ambapo Rais Magufuli alitangaza, kuvipiga marufuku vyama vya upinzani kutofanya shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020, wakati yeye na chama chake cha CCM, tukiwaona kila kukicha wakifanya kampeni nchi nzima!
Tumeshuhudia "uhuni" wa hali ya juu, ukifanywa na watendaji wa serikali wa kata, kuwanyima haki yao viongozi wa vyama ya upinzani kugombea kwenye serikali za mitaa, kwa sababu za kitoto kabisa, kama vile kuzikimbia ofisi zao, kwa nia tu ya "kuwakacha" viongozi wa uoinzani, wanaorejesha fomu zao walizozijaza za kuomba uongozi wa serikali ya mitaa
Tumeshuhudia pia wasimamizi hao wa uchaguzi wakiwa-disqualify viongozi wa upinzani kwa sababu za kitoto kabisa, kama vile kudai kuwa wamejaza kimakosa, fomu zao kwa kuandika vyama vyao wanavyotoka, kama vile kuandika unatoka chama cha ACT wazalendo au Chadema, kuwa umejaza kifupi, wakati wenzao wa kutoka chama tawala wakijaza kuwa wametoka chama cha CCM na kuambiwa kuwa wamejaza kwa usahihi wa asilimia 100!
Hebu niwakumbushe kidogo tu siku za nyuma wakati kampeni za kwanza kabisa kufanyika mwaka 1995, baada ya kurejesha mfumo wa vyama vingi, mashabiki wa mgombea urais wa chama cha NCCR Mageuzi, walizoea kumbeba mgombea wao wa urais, Augustine Mrema, kuonyesha kuwa wanampenda, ndipo Jeshi letu la Polisi likawa linawapiga wafuasi hao wa NCCR Mageuzi, ndipo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, akaingilia kati kuwa kama washabiki wao wameamua kumbeba mzoga mzoga kama maiti mgombea wao, nyinyi Polisi shida yenu ni ninii??
Waache wenyewe mashabiki wao waendelee kumbeba kama mzoga na wala msiwabugudhi mashabiki wao
Hivi hawa CCM wameshawahi kuusikia ule msemo maarufu wa kiswahili unaosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza?
Kama nyinyi CCM mnajiamini kiasi hicho, kwanini hamuachi uwanja wa ushindani ulio sawa, badala ya kufanya hizi hila za kitoto kabisa??