Hivi ni Bodi gani inaweza kumpangia mtumishi wa umma mshahara mkubwa kuliko wa Rais?

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
2,933
2,000
Kwa mujibu wa Rais Magufuli ni kwamba kuna watumishi wengi tu wamemzidi mshahara.

Sasa nauliza tu.

Je, ni bodi ipi ina ujasiri na mamlaka ya kuipima kazi ya mkurugenzi fulani ni kubwa, ya thamani na ni ngumu kuliko ya Rais?

Je, mshahara wa Rais Tanzania hupangwa na Rais mwenyewe aliye madarakani?

Mtangulizi wa Rais Magufuli (Kikwete) aliwahi kuanika mshahara wake?

Je, mshahara wa Rais haupitii hazina?

Kama Magufuli aliona hana haja ya kulipwa pesa nyingi kwa manufaa ya taifa, je, kwanini hajaamuru mishahara ya watumishi wote iwe chini ya milioni 10?

Au amekubali kuwa kuna watumishi ni muhimu zaidi yake.
 

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,738
2,000
Tunatakiwa watumishi wote wa umma wawe na mfumo mmoja kwenye kupanga mishahara. Kusiwepo na ubaguzi. Unapopanga mishahara minono kwa watumishi fulani na wengine inawapangia mishahara kondefu una maanisha nini? Kuna watumishi muhimu na wasio muhimu au? Vivyo hivyo iwe kwa watumishi wa sekta binafsi.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,087
2,000
Umeandika pumba tupu!:

Unaelewa kuwa hakuna sheria inayokataza mtu kulipwa mshahara mkubwa kuliko Rais?Unaelewa kuwa Rais siyo chombo cha kupangia watu kiasi cha mshahara hata aagize kuwa hakuna mfanyakazi kulipwa zaidi ya million 10?
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,127
2,000
Tunatakiwa watumishi wote wa umma wawe na mfumo mmoja kwenye kupanga mishahara. Kusiwepo na ubaguzi. Unapopanga mishahara minono kwa watumishi fulani na wengine inawapangia mishahara kondefu una maanisha nini?Kuna watumishi muhimu na wasio muhimu au?Vivyo hivyo iwe kwa watumishi wa sekta binafsi.
Unakosea sana Mzee mishahara haiwezi kulingana kamwe kama unataka kuwalinganisha Watu wa halimashauri au Wizarani na kwenye Taasisi kubwa ambazo ndio zina generate mapato utazingua na uta create rushwa katika izo taasisi huwezi mlipa sawa degree holder wa TRA au Tanesco au Tanapa na Degree holder wa halmashauri lazima Gap ziwepo tu
 

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
1,723
2,000
Ni Bora mtumishi wa TRA alipwe milioni 20 kuliko raisi alipwe milioni 20.

Reason.
Ela ya mtumishi wa TRA itarudi kwenye cycles atajenga nyumba.atapanga, atanunua Gari, atapeleka watoto kusoma, atakupa Bata.Raisi yeye sijui mshahara wake huwa anafanyia nn maana kila kitu amekua covered.
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
2,933
2,000
Umeandika pumba tupu!:

Unaelewa kuwa hakuna sheria inayokataza mtu kulipwa mshahara mkubwa kuliko Rais?Unaelewa kuwa Rais siyo chombo cha kupangia watu kiasi cha mshahara hata aagize kuwa hakuna mfanyakazi kulipwa zaidi ya million 10?
Rais hana mamlaka ya kumpangia mtumishi mshahara ila ana mamlaka ya kuzuia nyongeza ya mtumishi kwa miaka zaidi ya 5!!!!
Kweli wewe pimbi.

Rais ni chief treasure, ana mamlaka yote juu ya fedha za umma. Ndio maana alitumia authority hiyo kuminya haki zetu watumishi.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,087
2,000
Rais hana mamlaka ya kumpangia mtumishi mshahara ila ana mamlaka ya kuzuia nyongeza ya mtumishi kwa miaka zaidi ya 5!!!!
Kweli wewe pimbi.
Rais ni chief treasure, ana mamlaka yote juu ya fedha za umma. Ndio maana alitumia authority hiyo kuminya haki zetu watumishi.
Rais kuwa chief treasure haimfanyi awe juu ya sheria,kanuni na taratibu zilizopo zinazotawala mambo ya fedha ikiwemo ulipaji wa mishahara.Rais siyo chombo kinachopanga wala kusimamia mishahara ya wafanyakazi.Na Rais alipozuia nyongeza ya mishahara kwa watumishi kwa miaka mitano hakufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.Alivunja sheria na hilo siyo suala la kujivunia hapa!
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,319
2,000
Hiyo haikuwa point ya Magufuli, kwamba mishahara yote ishushwe iwe chini ya anacholipwa yeye,

Point yake ni kuwa hao waliohamishwa walipwe kulingana na mishahara ya huko walikopelekwa, hiyo ina make sense kisheria.

Kwa mfano Twiga Bank na Tanzania Postal Bank zilipomerge, watumishi wa Twiga Bank waliopelekwa TPB walipewa mikataba mipya kulingana na mishahara ya TPB na sio Twiga Bank, wapo ambao hawakuridhika wakaacha, maana unakuta anapokea kidogo kulinganisha na huko alikotoka.

Mleta mada unataka tuanze kusema kwamba kwakua Trump aliamua kupokea dola moja hivyo wamarekani wote walipwe below 1$, haiko hivyo, mshahara wa rais upo kisheria ila ni kwa Utashi tu ambao tunamshukuru Sana MH. Rais Magufuli akaamua kupokea hicho alichokitaja.
 

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,738
2,000
JK aliundaga tume ya mishahara walati anaingia madarakani.Kila ili itoe ushauri wa kuboresha maslahi ya wsfanyakazi lkn taarifa ya hiyo tume haikuwahi kuwekwa hadharani hadi leo
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,553
2,000
Rais hana mamlaka ya kumpangia mtumishi mshahara ila ana mamlaka ya kuzuia nyongeza ya mtumishi kwa miaka zaidi ya 5!!!!
Kweli wewe pimbi.
Rais ni chief treasure, ana mamlaka yote juu ya fedha za umma. Ndio maana alitumia authority hiyo kuminya haki zetu watumishi.
Ndio udikteta unaoongelewa juu ya huyu rais!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom