Hivi ni Bodi gani inaweza kumpangia mtumishi wa umma mshahara mkubwa kuliko wa Rais?

Usitupe lawama kwa Rais aliyepo haya mambo yalikuwepo hata kabla yake.
Watu wanasahau kwamba maovu mengi yanaonekana sasa hivi lakini yalianza kipindi cha Mkapa na Kikwete. Watu walijimilikisha taasisi na idara za serikali wakawa wanajiamulia chochote wanachojisikia kinawafaa.
 
Kwa mujibu wa Rais Magufuli ni kwamba kuna watumishi wengi tu wamemzidi mshahara.

Sasa nauliza tu.

Je, ni bodi ipi ina ujasiri na mamlaka ya kuipima kazi ya mkurugenzi fulani ni kubwa, ya thamani na ni ngumu kuliko ya Rais?

Je, mshahara wa Rais Tanzania hupangwa na Rais mwenyewe aliye madarakani?

Mtangulizi wa Rais Magufuli (Kikwete) aliwahi kuanika mshahara wake?

Je, mshahara wa Rais haupitii hazina?.
Kama Magufuli aliona hana haja ya kulipwa pesa nyingi kwa manufaa ya taifa, je, kwanini hajaamuru mishahara ya watumishi wote iwe chini ya milioni 10?

Au amekubali kuwa kuna watumishi ni muhimu zaidi yake.
Raisi kuzidiwa mshahara na watumishi wengine siyo jambo jipya. Hiyo ni kawaida dunia nzima. Kwa mfano USA mshahara wa raisi ni $400,000 kwa mwaka. Lakini kuna maelfu ya wafanya kazi wanaopata mamilioni ya dollar kwa mwaka. Utakuta huo mshahara wa mwaka wa raisi ni mshahara wa mwezi kwa watumishi. Huko private sector ndiyo usiseme, mishahara ni kufuru.

Pia kuna jambo lingine za kuzingatiwa kwa tofauti hiyo ya mshahara ambayo mwishoni inaweza kumfanya raisi awe na mshahara mkubwa kuliko hao wenye mishahara mikubwa. Kumbuka raisi ana ruzuku ambayo inagharimia maisha yake na familia yake. Yeye mshahara wake huo wa millioni tisa unaenda strait benki. Lakini wenye mishahara mikubwa wengine hulipia gharama zote za maisha na huo mshahara. Kwa nmana hiyo ingawaje mshahara wa Magufuli ni mdogo kuliko wa mkuu wa TRA lakini baada ya makato na matumizi yule Bw. wa TRA anabaki na salio dogo kuliko Raisi Magufuli.
 
Nchi inaongozwa na washamba na malimbukeni hapa ndiyo msingi wa matatizo yote
Nani mshamba kati yako unayetumia avatar ya Vladimir Putin mzungu badala ya kuweka ya kwake au ya Kiafrika
 
Pia ukiacha mshahara posho zaweza kuwa kubwa kwa prezidaa na hivyo mpunga wake ukawa mrefu uspime
 
Raisi naye tumpangie nchi ikipaa kiuchumi aongezewe mshahara ikiporomoka kiuchumi Kama Sasa naye apunguziwe mshahara
 
Twende kidigital mapato ya nchi yakiongezek automatically mishahara nayo inaongezeka, ulienda bank ukakuta mshahara umepungua ujue ufanisi umeshuka
 
Ni Bora watu wawe na mishahara mikubwa ili purchasing power iongezeke..na wafanya biashara wapate wateja.. Kuna watu humu wanaumia kuona mtu analipwa mshahara mkubwa hajui kwamba hiyo mishahara unarudi kwenye mizunguko na kumnufaisha ata yeye mwenyewe. Watu wote tukiwa masikini hakuna biashara itafanyika
 
Sidhani Kama Kweli Rais Anachukua mshahara wa chini ya Milioni 20. Na Kama ni Kwel basi haoni hasara Kwakuwa Anapga Pesa Nyingi kiujanja
tatizo letu wabongo ...kuwaza kupiga every time. wengine wapo kutumikia wananchi. furaha yake ni kuona maisha ya wananchi yanae.kuwa mazuri,miundombinu mizuri watu wanasafiri.sio kila wakat kuwaza kupiga tu ndio maana hatuendelei kimiundombinu na kisekta kwa kuwaza kujaza matumbo tu ..
Usiwe na mawazo mgando kwamba fulan anapokea kias fulan eti hakitoshi atakua anapiga. sio kweli
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom