Hivi mtu unaanzaje kumchukulia rafiki yako mchumba wake?

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
2,017
2,384
Hivi huwa mnaanzaje? Hata hamuwaonei huruma rafiki zenu?

Waachie watu wa mbali wamchukulie mchumba wake lakini sio wewe unaemfahamu vizuri tu rafiki yako. Unawajua vizuri na umeshuhudia mapenzi yao mara nyingi tu halafu leo bila aibu unaenda kuwatenganisha kwa kitu ambacho hata hujui kama utadumu na huyo kaka.

Unavunja urafiki wa miaka kwa hisia tu za kupita ambazo ungeweza hata kuzicontol? Kuna dada mmoja amemchukulia rafiki yake kipenzi mchumba yake.

Urafiki wao ulianzia tokea wako secondary school mpaka hivi sasa urafiki wao ulivyokufa kama miezi minne iliyopita. Hao wachumba wamedumu kwenye relationship miaka tisa.

Hawakuwahi hata kuwa engaged. Sasa wameachana mkaka ameanza kuwa na rafiki wa ex wake ndani ya wiki 2 tu baada ya kuachana kwao. Sasa hivi wana miezi kama minne na wame engaged last night.

Eti wanatarajia kuoana mwezi wa tisa au wa kumi 😏 Alishindwa kuwa engaged na mwanamke aliedumu nae miaka 9 alafu amekuja ku engaged na mwanamke aliekuwa nae kwenye uhusiano miezi kadhaa :( ila kuna wanawake wengine hawana akili hata kidogo hivi unakubali vipi kuishi na mtu hujaoana nae miaka yote hiyo 9?

Miaka 9 kama mkopo wa nyumba vile 😂 yaani hiyo miaka 9 kama ungekuwa umekopa mkopo wa nyumba ungekuwa unamalizia kulipa deni lako mwaka huu 😂 Sasa wee miaka 9 yote mwisho wake umekuja kuporwa mchumba wako na best friend ako😔

Mimi siku ikija kunitokea kitu kama hiki simuachi mtu. Hata kama sijawahi kuroga, naenda kuroga wote wajinga hao 😏 Na wanaume huwa mnakosa kabisa watu wa kuwa nao mpaka unatoka na best friend wa mchumba wako? Halafu bila aibu mnavishana pete mnashare ati "she said yes"

Nimemsikitikia sana huyu dada alieibiwa mchumba ake. Hakuna mtu yoyote ana deserve kitu kama hiki. Jifunzeni kutowamini sana watu hasa wale wanaojifanya kuwa ni marafiki kwako. Kuwa na urafiki nao ila usiwape nafasi wakajua mambo yako na usiwaweke sanaa karibu yko. ✍️
 
Hao walikuwa wanakulana toka zamani tu.
Halafu huwa mtu akikaa muda mrefu na mwanamke bila kumuoa akimuacha akapenda mwingne anatangaza ndoa mwaka huo huo
 
mbona hizo ni mambo za kawaida sana tuu, hivi mwanamke unaendaje kwa mpenzi wako au mchumba wako na rafiki yako wa kike?, angali wajua amekuzidi mvuto?

Nina evidence kibao tuu, za kuhusu wanawake kunyang'anyana wachumba, unashangaa mwenye mchumba anatemwa, anaolewa rafiki yake. Hizo ni ishu za kawaida sana.

ONYO; Wanawake unapokwenda kwa mchumba wako usipende kuongozana na mwanamke mwenzako, hata kama ni dada ako au mdogo wako wa kike, vinginevyo utakuja shangaa umeachwa wewe, anaolewa yeye.

Pia mwanamke unapokuwa ukiongea na mchumba wako usipende kumuongelea rafiki yako wa kike au ke yeyote, utajashangaa ushapigwa kibuti anachukuliwa yeye.

Na pia mwanamke unapopata mchumba usitake ke wenzako wajue kisa upate sifa, haohao unaowaambia ndo watakaokuchukulia huyo mchumba.
 
kweli kabsaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom