Habari za Asubuhi wakuu, natumaini mumeamka salama na wengine mshaanza kupambana tena kwa siku nyingine hii ya leo ambayo Mwenyezi Mungu ametubariki.
Sasa iko hivi tangu gharama za vifurushi za mitandao ya simu zipande, huu mtandao wa Vodacom naona bado mambo ni yale yale, yaani hakuna walichofanya kama vile hawajui kinachoendelea.
Yaani wameacha zile bei mpya za vifurushi mpaka wakati huu, ikiwa nasiki kuna baadhi ya mitandao wao wamesharudisha bei zile za mwanzo ambazo zilikuwa ni nafuu zaidi kuliko hizi za sasa hivi.
Sasa wakuu labda kama kuna mwenye kujua hizi mambo zitakaa sawa kwa wakati gani, au inabidi nizoee tu kama hawana mpango wa kurekebisha hivyo vifurushi.
Uzi tayari.