Fahamu kuhusu mgomo uliopo katika mtandao wa 'Reddit'

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
Habari wapenzi wasomaji! Leo nataka kuongea nanyi kuhusu mgomo unaoendelea kwenye Reddit na API yake.

Kama mnajua, Reddit ni moja ya mitandao maarufu zaidi ya kijamii ambapo watu wanaweza kushiriki maoni, habari, picha na video za kuvutia. Lakini hivi karibuni imeingia katika ugomvi mkubwa na moderators na apps nyingine kama vile Apollo ambayo ni app inayotumia contents za Reddit kwa kutumia API yake.

API ni kifupisho cha Application Programming Interface, ambayo ni njia ya kuwasiliana na programu nyingine. Kwa mfano, kama unataka kutumia programu ya simu ya Reddit, unahitaji API ya Reddit ili uweze kupata maudhui yote yanayopatikana kwenye tovuti yake. API inaruhusu programu mbili au zaidi kubadilishana data na kuagiza vitendo.

reddit-usage-and-growth-statistics.webp

Kwa kawaida Reddit imekuwa ikiweka API iwe inapatikana bure na kila mtu ana uhuru wa kuitumia na kutengeneza platform ambayo inatumia contents na mfumo wa Reddit. Mfano app ya Apollo ni app ambayo inatumia platfom ya Reddit kwa kutumia API yake. Pia moderators wengi wanatumia app ya Bot ambayo inawasaidia ku-post kwenye Reddit na kusimamia majukumu mbalimbali. Watu wengi hawapendi kuitumia platform ya Reddit original kwa sababu haina mwonekano mzuri lakini katika Third Party kuna mwonekano mzuri na kuna features nyingi ambazo hazipatikani kwenye Reddit ya kawaida.

April 18 mwaka huu; Reddit ilitangaza kuwa API itaanza kuwa ya kulipia. Na bei yake ambayo Reddit imesema ni kubwa sana na haina uhalisia kwa Third Party ambao wanatumia API ya Reddit kuitumia. Mfano app ya Apollo inalazimika kulipia dola Milioni 20 kwa mwaka, kitendo ambacho kimeonyesha kuwa Reddit imeamua kuzuia API yake isitumike makusudi.

image-5.png

Apollo ni app ambayo inakwenda kupata hasara na tayari imesema kuwa itafunga app yake mwisho wa mwezi huu. Reddit imegoma kushusha gharama za API na moderators wake wameanza kugoma na kuamua kuweka mgomo wa kufunga subreddit zao.

PNG-image-copy.png

Reddit haikujibu vizuri ni kwanini imeamua kuweka gharama kubwa. Umekwepo mvutano mkubwa kati ya mwanzilishi wa Apollo na CEO wa Reddit; kwa sababu Apollo ni moja kati ya app ambayo imelalamika itaumia kwa sababu ya mabadiliko hayo ya API.

Mwanzo CEO wa Reddit - Steve Huffman; alionekana amemjibu vibaya Christian na alisema kuwa mwanzilishi wa app ya Apollo ametishia kuifungulia kesi Reddit. Lakini mwanzilishi wa app ya Apollo ambaye ni Christian Selig alisema taarifa hizo sio za kweli na alitoa ushahidi wake wa calls zote alizokuwa anawasiliana na CEO wa Reddit. Na kupelekea CEO wa Reddit kuomba msamaha kwa kumsingizia Christian kuwa ameitishia Reddit.

Kwanini watu wengi hawapendi kutumia Reddit lakini wanatumia apps kama vile Apollo ambayo inatumia API ya Reddit?​

  1. Ni kwa sababu Reddit ina mwonekano mbaya, na ina features nyingi ambazo zinakosekana. Mfano hauwezi kufungua video vizuri na hauwezi ku-save HD Pictures.
  2. Reddit haina sehemu nzuri ya Accessibility. Watu ambao wana mahitaji maalum wanatumia app kama vile Apollo.
  3. Moderators wanatumia API ya Bot kwa sababu ina tools nyingi za kusimamia posts na contents.
  4. API ya Reddit itakuwa haikubali contents za “Not Safe for Work”.
BlogHeader_PortalSnoo_002.png

Kwanini Reddit imeamua kuweka API iwe ya kulipia, na kuweka gharama kubwa?​

  1. Kwa sababu uchumi ni mgumu na hali za kibiashara katika kampuni za tech ni changamoto. Na Reddit haipati faida sana kupitia matangazo hivyo inajaribu kuweka vyanzo vya mapato kupitia API yake.
  2. Reddit ina mpango wa kuingia katika soko la Hisa, hivyo inalazimika kuweka mfumo wa kupata thamani kubwa endapo kama itaingia kwenye soko la hisa
  3. Ongezeko la AI duniani: Hizi Generative AI ambazo tunaziona duniani mfano ChatGPT na Bard ya Google zinatumia texts na taarifa nyingi za texts katika kutengeneza mfumo wa Akili Bandia na kujibu maswali. Data zake zinazotumika ni data za Twitter, Reddit, Quora na platform nyingine nyingi. Akili Bandia hizo zinatumia API za mitandao ya kijamii ili kusoma na kuona texts na contents. Zinachukua contents hizo na kuzitumia katika kufundisha Akili bandia bure bila kulipa hizo platforms ambazo contents zake zinatumika. Reddit inalazimika kuzuia API yake isiwe rahisi kuipata ili kuzuia Akili Bandia zisitumia contents zake. Hali hii pia iliikuta Twitter mwaka huu na kulazimisha Twitter iongeze gharama zake.

Subreddits kubwa hazipatikani na Moderators wanatishia kuacha kuweka contents kwenye mtandao wa Reddit. Wengi wanahisi mabadiliko haya yataharibu mfumo na biashara ya Reddit. Bado mgomo unaendelea na Subreddits kubwa bado hazipatikani na moderators wamegoma kuendelea kuweka contents kwenye mtandao huo.

Taarifa nzuri
 
Asante saana
 
Back
Top Bottom