Je, kuna mkono wa Serikali katika kuongeza bei ya vifurushi? Serikali kuja na mfumo wa kudhibiti simu za WhatsApp

w0rM

Member
May 3, 2011
68
163
Siku chache zilizpita Kampuni za Simu za Tanzania; Vodacom, Tigo na Airtel n.k ziliongeza bei za vifurushi na kusabisha taharuki kwa watu wengi kwa bei hizo zilipanda maradufu.

Serikali na Taasisi zake zilisubiriwa sana kuja kuzungumzia suala hilo, badala yake TCRA ikaja na chapisho la kuonesha kuwa makato cha simu kutoka 2018 hadi sasa yamepungua kwa kiasi fulani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Zainab Chaula alisema wizara inafahamu mabadiliko hayo na inaendelea kuyafanyia kazi. “Tunafahamu na tunaendelea kufanyia kazi,” aliongeza Dk Chaula

Leo, Serikali kupitia kwa Waziri mwenye dhamana ya Taknolojia anasema wanaandaa mfumo wa kuzuia watu kupiga simu kwa kutumia WhatsApp kwani wamegundua inahusika katika kupunguza mapato ya simu za kawaida kwa Serikali

Je, Serikali ihusika katika kupandisha bei ya vifurushi vya simu ikiwa ni njia moja wapo ya kupunguza watu wanaotumia mtandao?

6AFBB030-7A4F-424D-8596-B7BA47FBC0AC.jpeg
 
Serikali sikivu ya wanyonge iko mbioni kufuta nchini huduma za kupiga simu kwa njia ya mtandao, mfano WhatsApp call, I na kadhalika.
Hayo yamesemwa na waziri mwenye dhamana ya sayansi na teknolojia bwana Faustine Ndugulile

Siku chache zilizopita bwana Ndungulile alikaririwa akisema kuanzia siku chache zijazo MB 1 itauzwa kwa shilingi tisa.

Screenshot_20210310-094845.png

Screenshot_20210310-094854.png
 
Watsap call zinapunguza gharama kuwapigia ndugu na jamaa waliopo nje ya Tanzania..
Na upata wasaa wakuona pia

Doh

Viongozi wetu., kama wizara imekosa majukumu mama ifutwe tu.
 
Sisi mbona hatulalamiki data zipo juu, m-pesa, tigo na Airtel Money ninaetuma nakatwa anayepokea anakatwa. Mbona kuongea gharama zipo juu? So mtazuia whatsapp call vipi viber, Facebook messenger, telegram, Zoom??Mtake msitake technology ndio inaelekea huko.
 
Mkuu na mdau umejiandaaje kununua GB1 kwa shilingi elfu tisa?
inbound2622120093940994777.jpg

Mitano tena🤜.
 
GB 1 Kwa Tsh 9000 hiyo haipo.....!!! Tushawah nunua Tsh 500 Kwa mb 70 Ila sa hivi tunanunua TSH 500 Kwa mb 500.... Hizo ni propaganda tu
 
GB 1 Kwa Tsh 9000 hyo haipo! Tushawahi nunua Tsh 500 Kwa mb 70 Ila sa hv tunanunua TSH 500 Kwa mb 500. Hizo ni propaganda tu
Ndio sheria hiyo inakuja kuanzia April

Mb 1 itauzwa kati ya sh. 2 hadi 9
 
Back
Top Bottom