Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,271
- 2,401
Nauliza hivi kwa mshangao sana. Ni kuhusu suala la maji. Yapo maeneo maji wanapata kila siku. Kuanzia Bima kwenda hadi relini kule maji ni kila wakati. Mshangao kwao ni maji yakikatika.
Maeneo ya Segerea kuelekea Kisukuru na Bonyokwa huko kuna changamoto sana ya maji. Huku yakitoka inabidi tushangae. Kwa nini? Au mifumo ya kuleta maji katika maeneo hayo tajwa ni miwili tofauti?
Kwa nini basi pasifanywe mgao kati ya maeneo haya? Huku tunanunua maji ya magari. Ni ghali kweli wakati mabomba tumefungiwa na dawasa. Msimu huu wa mvua tunaponea ya mvua. Mbunge na madiwani mnafanya kazi gani?
Au hayo magari ya kusomba maji ni miradi yenu? Tunahitaji na tunataka maji ya uhakika kama maeneo mengine