Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,323
- 1,113
ABBAS MTEMVU AWAONYA VIONGOZI WASIOFANYA KAZI ZA ILANI
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar Es Salaam Abbas Mtemvu, amesema Diwani yoyote wa chama cha Mapinduzi katika Mkoa huo na Mbunge asiyetekeleza Ilani ya chama afai kwa uongozi .
Mwenyekiti wa CCM mkoa Abas Mtemvu, alisema hayo katika mkutano wa hadhara Jimbo la Segerea wa utekekezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Bonnah Ladslaus Kamoli .
"Diwani aliyopo madarakani na Wabunge wao asiyefanya kitu kwake katika utekekezaji wa Ilani ya chama na kuwatumikia Wananchi hawafai kuchaguliwa " alisema Mtemvu .
Mtemvu amewataka viongozi waliopo madarakani ambao wanatokana na chama CCM kuwatumikia Wananchi katika shughuli za kijamii na kutatua kero kwa utekekezaji wa Ilani ya chama ikiwemo kusimamia miradi ya Maendeleo ambayo imetelekezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Rais Samia Suluhu Hassan .
Aliwataka vijana ,Wanawake na Watu wenye ulemavu kila Kata kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kuunda vikundi Ili waweze kupata mikopo ya asilimia kumi ambayo aina riba inayotolewa ngazi ya Halmashauri .
Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM mkoa Abbas Mtemvu, alitumia fursa hiyo kutatua kero za Wananchi wa Jimbo la Segerea, Kata ya Bonyokwa na Kinyerezi katika maeneo yaliokosa maji ya Dawasa kwa kuongea na Eng ,Mkuu wa Dawasa Makao makuu na kukili ni kweli maeneo ya Msingwa na Kifuru maji hayafiki kutokana na presha ndogo DAWASA imechukua changamoto hiyo sasa hivi mradi mkubwa wa maji unajengwa wa shilingi bilioni 41 mradi utajengwa Bangulo Hali ya hewa na utasambaza maji maeneo yote mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia Mwezi Agosti mwaka huu mkataba utasainiwa rasmi alisema Eng Mkuu wa Dawasa kwa njia ya simu .
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, alisema mkutano huo ni wa Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ambapo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuwatumikia Watanzania na Jimbo la Segerea kwa ujumla.
Mbunge Bonnah alieleza baadhi ya Barabara zinazojengwa Jimbo la Segerea na Rais ikiwemo Bonyokwa Segerea Tanrods ,Kisukuru Bonyokwa ujenzi umeanza maji chumvi.