Hivi MBA bado ina soko?

Hivi MBA bado ina soko?

JAMBONIA LTD hali yako mkuu samahani natafuta jinsi ya kukuPM ila nashindwa niko hewani kwa simu...naomba kujua kuhusu iyo masters hapo open university
Nimeupata ujumbe wako chek inbox
 
Kwanini sisi watanzania kucha kuchwa tunafikiria kusoma tuwe watumishi? Hii mentality mbona haitoki akilini mwetu?

Unasoooooma weeee, baadaye unasaka ajira. Ukiambiwa mshahara laki nne kama Viettel unaanza kulalama eti kamshahara kenyewe kaduchu mpaka waanzisha thread JF!!! Kwani wewe hao waajiri walikutuma ukasome hiyo mikozi yako? Mliagana nao? Fikiria nje ya boksi.

Kusoma si sawa na ajira. Soma ikusaidie kuelimika, kuongeza ujuzi, kuweza kupambana na mazingira. specialist88 katoa ushauri mzuri kwamba mtu ambaye kaajiriwa ndiyo anaweza kwenda kusoma MBA ya kitu fulani. Ni sahihi kabisa.

Sasa wakuta mtu kamaliza bachelor, kakosa ajira anaenda kusoma masters, wengine wakikosa ajira wanaenda kusoma phd, thubutu, nani akupe kazi na li masters lako wakati umejaza mi theory kichwani. Hata mtumishi mwenye certificate tu atafanya kazi nzuri zaidi ya wewe mwenye midigrii yako.

Usisome ili kuwa mtumishi, soma uongeze ujuzi wa kile ufanyacho. Sasa ukisoma hicho ukarudi mtaani na kukosa ajira utaenda kusoma nini? Soko la ajira labadirika kila mwaka. Usiseme kitu fulani kila soko kina soko, kina soko wapi hicho mnachosema kina soko. Tujifunze kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kaskazini, wanasoma MBA iwasaidie kwenye biashara zao, sio ili wakasake ajira...
 
Last edited by a moderator:
Vip kuhusu logistics and transport
Kaka usipoteze muda wako kwa kusoma kwa style hiyo. Hiyo logistics and transport umeona lini ajira yatangazwa hata kwenye gazeti tu? Unataka uende Sumatra? Nawajua wafanyakazi wa Sumatra ambao wapo kazini na wanasoma hayo mambo mlimani. Unataka uende NIT? Au unataka uajiriwe wapi? Siamini katika kusoma kwa ajili ya kutafuta kazi. Napenda ukisoma hata ukiwa nje ya kazi uweze kujiajiri. Halafu ukumbuke pia unavyokuwa specialist katika elimu ndivyo inakuwa ngumu kupata ajira sehemu nyingine. Unahitaji kuwa generalist, then ukiingia kazini unatanua ufahamu wako kwa kusoma lile eneo linalokuhusu. Sasa hujajua hata uajiriwa wapi unaanza kutafuta shule, tena shule zenyewe ndiyo hizo za Open University, ambao zamfaa mwajiriwa...
 
Ahsante mkuu nimekupata, umegonga mule mule, kwa bahati nzuri kwa sasa mimi ni mwajiriwa na baadae nna mpango wa kujiajiri....
 
Mkuu JAMBONIA LTD vipi maendeleo yako. Tunaomba mrejesho ili tupate la kujifunza wanaJF wenzako.
 
Mkuu JAMBONIA LTD vipi maendeleo yako. Tunaomba mrejesho ili tupate la kujifunza wanaJF wenzako.
Ha ha aisee mkuu upo vizuri, umefukua kaburi...e bwana wee kipindi hicho nilipata ajali nikasota sana kitandani miaka na miaka hivo sikwenda shule kwa wakati huo nimeona juzi juzi tu na namalizia kozi nyengine ya Afya MSc.
 
Ha ha aisee mkuu upo vizuri, umefukua kaburi...e bwana wee kipindi hicho nilipata ajali nikasota sana kitandani miaka na miaka hivo sikwenda shule kwa wakati huo nimeona juzi juzi tu na namalizia kozi nyengine ya Afya MSc.
Mkuu JAMBONIA LTD JF ni database ya maarifa, ndio maana makaburi yanafukuliwa kama hivi.
Aisee pole sana kwa masahibu yaliyokupata, yote maisha.
Nlikuwa naifikiria MBA marketing, ikanibidi nisearch hapa, ndo nikakutana na uzi wako. Ikabidi niombe mrejesho ili tupate wenye experience.
 
Ha ha aisee mkuu upo vizuri, umefukua kaburi...e bwana wee kipindi hicho nilipata ajali nikasota sana kitandani miaka na miaka hivo sikwenda shule kwa wakati huo nimeona juzi juzi tu na namalizia kozi nyengine ya Afya MSc.
Mkuu ebu nifungue kidogo kuhusu hyo kozi ya afya MSc
 
Back
Top Bottom