Hivi mapato ya mwezi Mei ni kiasi gani?

amsha

Member
May 22, 2015
15
15
Tulizoea miezi ya nyuma kutangaziwa mapato na matumizi toka awamu hii imeanza lakini sasa hali imekuwa tofauti hayatangazwi tena je nini kimetokea ?

Au mapato yameshuka isivyo kawaida maana tuko gizani hatujui ni kiasi gani kinakusanywa.

Je athari za kupungua kwa meli bandarini inaweza kuwa ni sababu karibuni tujadili wenye taarifa za kina
 
Waje wakina Mzee Mwanakijiji na wenzie ambao kazi yao kumsifia mfalme waje watoe ufafanuzi juu hili maana kwa serikali hii ya kupenda sifa kama mapato yangekuwa yanaongezeka haraka sana tungetangaziwa ili kuonesha ni namna gani serikali yetu tukufu ilivyofanikiwa kuongeza mapato.

Hakika huu ukimya unamaanisha hali si shwari maana hata wafanyakazi mwezi uliopita wamechelewa sana kupata mshahara hii serikali huenda ikafeli kwa kila kitu ni suala la muda
 
amsha, waache bwana!
Watu wana halimbaya acha.
Yani ngosha alikuwa anataka kutengeneza cocktail mpya ya pombe, akaweka bia ya safari,red wine,ugoro,kiroba,panadol,grisi,uji... Sasa akiiangalia haielewielewi, hajui aweke nini tena!
 
Hii ni serekali iliyojinasibu ya kuwa na uwazi
Naona watakuwa wamesikia na wataleta majibu
 
Sijui kwa nini wanafanya siri....au kamishna wa TRA kaenda akarudi na sanduku tupu la fedha? Bado kuna mgogoro unakuja wa machine za TRA kariakoo......Tanzania ya viwanda tutaipata kwenye maombi....sio kwa Sera za serikali hii
 
"we yanakuhusu nini??"
Hili jibu nalitegemea sana katika uzi huu

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
amsha, waache bwana!
Watu wana halimbaya acha.
Yani ngosha alikuwa anataka kutengeneza cocktail mpya ya pombe, akaweka bia ya safari,red wine,ugoro,kiroba,panadol,grisi,uji... Sasa akiiangalia haielewielewi, hajui aweke nini tena!
Na ule ukurupukaji wake anaweza tia ata kinyesi kwa kuzidiwa na sifa zaidi.
 
Back
Top Bottom