Hivi lengo la binadamu duniani hasa ni nini??

Hivi lengo la binadamu duniani hasa ni nini??

Binadamu kaumbwa awe msimamizi wa kila kinachomzunguka , lakini atumie muongozo wa Muumba katika usimamizi huo ili waishi kwa furaha. Bahati mbaya baadhi ya binadamu wametunga nadharia za kupinga muongozo wa Muumba ili wapate kuzimiliki akili za binadamu wenzao .Matokeo ndo haya kutohurumiana. Vita, ufisadi, kukopeshana kwa riba, kujamiiana na kila kiumbe( mkeo na asiye mkeo, mume kwa mume, binadamu na wanyama na kuzusha magonjwa makubwa.
 
Hivi lengo la binadamu duniani hasa ni nini??
Watakujibu Kumtumikia Mungu. Maisha ya duniani ni mtihani tumepewa atakae faulu anaenda mbinguni/Peponi ambapo kutakuwa na mabikra 72 na mito ya pombe au kutakuwa hamna kula wa kuzaliana huko ni kumsifu na kumuabudu Mungu tu. KWA KIFUPI MAISHA NI MTIHANI WENYE LENGO LA KUKUTANISHA WEWE NA MUNGU WAKO ENDAPO UTAUSHINDA MTIHANI WA HAPA DUNIANI NA UKIFELI UNAENDA MOTONI TENA MILELE. SO, DUNIA NI CHUMBA CHA MTIHANI NA MAISHA NDO PEPAR YAKO NA MASWALI NDO JUMLA YA MATUKIO/MATENDO YAKO YOTE UFANYAYO DUNIANI. Uko chumba cha mtihani mkuu,kaza usipate sifuri ukaenda motoni🤠🤠Kwa mujibu wa watu wa Dini.
 
Infact hamna maana halisi ya maisha. Amua wewe
Wapo wanaosema maisha hayana maana ila wewe mwenyewe ndo unayapa maana. Jinsi unavyoendesha maisha yako ndo mtizamo wa maisha ulivyo kwako. Maisha bhana!
 
Main purpose: Angalia kile kitu universal, kila mtu anafanya bila kujali yeye ni masikini au tajiri, Race yoyote, kila mtu ana access nacho, hilo ndio lengo la maisha.

Mengine yote ni ziada.
 
Back
Top Bottom