Hizo takwimu hazithibithi uwepo wa uchawi mkuu. Nimekulia Mbeya ila sijawahi ona mchawi au tukio la kichawi hata siku moja nasikia story tu kama unavyoweza sikia story mtu kaenda mbinguni na kurudi Nimefika Sumbawanga, Tanga, Kigoma ila sijaona kiashiria chochote cha uwepo wa uchawi maeneno hayo Kama kuna mtu anajua wapi naweza thibitishwa uchawi au kuniroga naomba anicontact tafadhali
mkuu ujue unanishangaza sana! kwa hiyo wewe kushuhudia tu ndio hujawahi! ila matumizi ya vitu kama hirizi ushawahi sikia ama kuona ama kutumia kabisa?? Tanga kama uliishia mjini, unaweza usione matukio kama haya,,,.. hebu jaribu kwenda korogwe, tembea vijijini kule kwa shambalai na maji marefu, huko hakika utakuja kutana na viumbe vinaitwa VIBWENGO! hahahaaaa!! nakwambia utatoka mita vibaya sana na bado hautoviacha mbio ndugu yangu!! mimi nilishawahi shuhudia kwa macho yangu hivi viumbe! enzi nikiwa Korogwe vijijini kule miaka ya 2000 nikiwa shule ya msingi, nilishawahi pigwa zongo kwenye maziwa ya ng'ombe na yakashindwa kutoka kwenye kidumu.. basi tu ilibidi yatupwe...
ndugu yangu, mwalimu wangu alikuwa na mtoto wa miaka mi3 hivi kama sijakosea, mtoto huyo alionekana akila tunda fulani akiwa nje ya nyumba yao, alichofanyiwa ni kitu kibaya sana!! mtoto alipigwa zongo (nadhani watu wa tanga na wenyeji wa pwani wanaelewa sana hili), mtoto alivimba tumbo kama wiki nzima, kila wakati linabana tu masikini, kwenda hospitali, hawaoni ugonjwa wowote...! solution ilikuwa ni kwenda kwa waganga kumgangua.. kweli akapona na kurudi kwenye hali ya kawaida..!! shule ya msingi niliyokuwa nasoma 14 years ago, ilikuwa ikishafika saa 12 jioni, ilikuwa haiwezekani kukatiza maeneo ya shule kutokana na kugubikwa na uchawi wa majini na binadamu! wenyeji tu ndio walikuwa wanawezana na hayo mambo!! mtoto yeyote katika kijiji kile, kwa mtu ambae ni mgeni, kupewa kitu ukala hivi hivi ilikuwa ni ngumu sana, otherwise muwe mnajuana kiundani, imagine maziwa tu yalikuwa yanafunikwa na kufichwa sana ili yasitambulike, otherwise yanapigwa zongo na kuharibika...!
ndugu yangu mimi nilishashuhudia jini (kKIBWENGO) kikiwa kinatembea kwa mguu mmoja (mguu wa kwato ya ng'ombe!) kibwengo akitembea si hatua ya kawaida kumbuka, si hatua ya kibinadamu, ni hatua moja kwa mita mia na zaidi kulingana na umbali anaotaka kwenda.. kama ni short route basi atabadilisha speed mwenyewe! ndugu yangu bado tu unaamini uchawi haupo?? Tanga nimeishi kwa miaka minne japo nilikuwa mdogo, lakini niliweza kutambua baya na jema! waulize wenyeji wa Tanga watakuambia hadithi za
Majimoto... korogwe vijijini ndani, kuelekea makangara na magoma sekondari! huko ndiko uchawi uliko lala! hayo mazingira si ya kawaida! ukisikia mtu anauza karanga akiwa uchi saa nane mchana, halafu karanga zenyewe ni mavi ya mbuzi... basi ndio huko! UCHAWI UPO NA UNAANGAMIZA WENGI! cc..
utafiti for further knowledge increase..