hiyo ni kweli.. kwamba kila baya lina mwisho wake..
lakini je, unaamini kuwa uchawi upo masomoni?
mkuu sasa kwanini watu hawataki kuamini uchawi kuwa uchawi upo katika elimu???
ngoja niombe maoni zaidi... Arushaone, Lady doctor, MziziMkavu, mwekundu, Mtambuzi, Mr Rocky, Palomaaaaa!! (lols, you know why i called you so!) Mlachake, sosoliso, uran, kiwatengu, shansarie, amu, Preta, ram, lusungo, Dinazarde, JERRY msigwa, bily, farkhina, Mshinga, mpigamsuli, Dr. mo, Mr Rocky..
hoja inayojadiliwa hapa ni kwamba...
je, uchawi upo katika elimu/masomo?
mwanafunzi anaweza kufaulu kweli kwa kutegemea uchawi?? inawezekana vipi akili ya mwanafunzi ihamishwe kimazingara na kuwekwa kwa mwanafunzi mwingine?? je mnaamini haya kama yapo ama hayapo??
je, katika mazingira yenu mnayoishi, ama kwa jirani, ndugu na jamaa, vitendo kama hivi vilishawahi tokea?
karibuni wakuu...

samahani lakini shansa, umesomea shule za aina gani since primary?
nimesoma bording kijijini marangu
mkuu ujue unanishangaza sana! kwa hiyo wewe kushuhudia tu ndio hujawahi! ila matumizi ya vitu kama hirizi ushawahi sikia ama kuona ama kutumia kabisa?? Tanga kama uliishia mjini, unaweza usione matukio kama haya,,,.. hebu jaribu kwenda korogwe, tembea vijijini kule kwa shambalai na maji marefu, huko hakika utakuja kutana na viumbe vinaitwa VIBWENGO! hahahaaaa!! nakwambia utatoka mita vibaya sana na bado hautoviacha mbio ndugu yangu!! mimi nilishawahi shuhudia kwa macho yangu hivi viumbe! enzi nikiwa Korogwe vijijini kule miaka ya 2000 nikiwa shule ya msingi, nilishawahi pigwa zongo kwenye maziwa ya ng'ombe na yakashindwa kutoka kwenye kidumu.. basi tu ilibidi yatupwe...
ndugu yangu, mwalimu wangu alikuwa na mtoto wa miaka mi3 hivi kama sijakosea, mtoto huyo alionekana akila tunda fulani akiwa nje ya nyumba yao, alichofanyiwa ni kitu kibaya sana!! mtoto alipigwa zongo (nadhani watu wa tanga na wenyeji wa pwani wanaelewa sana hili), mtoto alivimba tumbo kama wiki nzima, kila wakati linabana tu masikini, kwenda hospitali, hawaoni ugonjwa wowote...! solution ilikuwa ni kwenda kwa waganga kumgangua.. kweli akapona na kurudi kwenye hali ya kawaida..!! shule ya msingi niliyokuwa nasoma 14 years ago, ilikuwa ikishafika saa 12 jioni, ilikuwa haiwezekani kukatiza maeneo ya shule kutokana na kugubikwa na uchawi wa majini na binadamu! wenyeji tu ndio walikuwa wanawezana na hayo mambo!! mtoto yeyote katika kijiji kile, kwa mtu ambae ni mgeni, kupewa kitu ukala hivi hivi ilikuwa ni ngumu sana, otherwise muwe mnajuana kiundani, imagine maziwa tu yalikuwa yanafunikwa na kufichwa sana ili yasitambulike, otherwise yanapigwa zongo na kuharibika...!
ndugu yangu mimi nilishashuhudia jini (kKIBWENGO) kikiwa kinatembea kwa mguu mmoja (mguu wa kwato ya ng'ombe!) kibwengo akitembea si hatua ya kawaida kumbuka, si hatua ya kibinadamu, ni hatua moja kwa mita mia na zaidi kulingana na umbali anaotaka kwenda.. kama ni short route basi atabadilisha speed mwenyewe! ndugu yangu bado tu unaamini uchawi haupo?? Tanga nimeishi kwa miaka minne japo nilikuwa mdogo, lakini niliweza kutambua baya na jema! waulize wenyeji wa Tanga watakuambia hadithi za Majimoto... korogwe vijijini ndani, kuelekea makangara na magoma sekondari! huko ndiko uchawi uliko lala! hayo mazingira si ya kawaida! ukisikia mtu anauza karanga akiwa uchi saa nane mchana, halafu karanga zenyewe ni mavi ya mbuzi... basi ndio huko! UCHAWI UPO NA UNAANGAMIZA WENGI! cc.. utafiti for further knowledge increase..
dada hujawahi sikia mtu anashindwa kuona maandishi kwenye karatasi anapoingia kwenye mtihani?
macho na kichwa kuanza kuuma immediately baada ya kushika daftari kwa lengo la kujisomea, hiyo nayo bado??
na bado akienda kwa professional doctors wanashindwa kugundua tatizo?
mkuu inakuwaje sasa mtu anatulia tu kando ya mwanafunzi mwenzie, kila kinachofanyika kina-divert kwenda kwake??
nimeshajiuliza sana.. hii dhana inakuwaje?? maandishi yanatoka vipi kwa mwanafunzi mmoja kwenda mwingine??
Mkuu Excel kwanza samahani kwa kutoitikia wito wako haraka.
Back to the topic, kama uchawi upo au haupo ktk masuala ya Elimu nina vivid example . Kwanza nakumbuka kuna jamaa tulikua nae Class na alikua kichwa kweli ila kilichotokea ni kurogwa na mwanafunzi mwenzake hadi macho yake yakawa haiwezi kuona tena na hili ilimfanya jamaa ahame shule na atoke mkoa ule kwenda mkoa mwngne Arusha to Mbeya.
Sasa je nini ilikua dhumuni la yule jamaa kumroga mwenzake? Aim yake ilikua yeye aongoze lile darasa Mkondo A na km nakumbuka kipindi hicho ukipasua njia ya kwenda Turkey,China,Korea na Japan ilikua nyeupe sn, sasa je jamaa alifanikiwa ? Hapana akufanikiwa hii ni kwasababu wanafunzi walimtenga sn na alijisikia na kujiona yeye si mtu wa kukaa pale shuleni ikabidi aondoke. Sasa kwa maoni yangu mambo hayo yapo pia inategemea na kichwa cha mtu leo sidhani mtu ajui chochote darasani then a expect miracles in his/her performance. Asante sn mtoa mada.
Excel......................mhh sijajua why umeniita hivyo..............njoo basi uniambie!!!mkuu sasa kwanini watu hawataki kuamini uchawi kuwa uchawi upo katika elimu???